Ndoa ya miaka 16 ipo hatarini kuvunjika kisa mtoto wa nje

Mwanaume kukosa msimamo ni hatari sana kwa afya ya ndoa.

Uyo mwanaume kiazi sana.

Uku kwetu,
Taratibu na mila zinasema ukija kuoa mke upate ruhusa kutoka kwa mke mkubwa.

Ila Babu zetu enzi hizo walikua wanatoa tu taarifa kwa wake zao kua
"wiki ijayo naongeza mke"

Hiyo inakua ni taarifa na sio anaomba ruhusa, Na ni haina discussion.

Ukiona hautaki mke mwenzio, kung'uta matako urudi kwenu.

Na unalazimishwa kabisa kuhudhuria, na kushiriki shughuri zote za kusherehesha ndoa ya mumeo kuongeza mke mwingine.

Sasa,
Sijui wanaume wa sikuhizi wanafeli wapi kwenye suala zima la kuonesha misimamo .

YAAN Mwanaume unakua laini laini utadhani wewe ndio umeolewa.

HII NI AIBU SANA KIUKWELI.
Umeandika enzi inzo sio sasa ni 50/50
 
Huyo mwanamke ana shida, yani waachane kwa kijana anayeiingia chuo? labda ana issue nyingine amepata sehemu ya kutafutia sababu.
 
Umeandika enzi inzo sio sawa ni 50/50
Hizo harakati zenu za 50/50 beijing ndo zimetuletea kizazi cha wanaume wa ovyo kama uyo rafiki yake mtoa mada.

Usikute nae anafuata mambo ya 50/50 mke nae analetaga chakula ndani.

Kwanza,
Hayo mambo ya 50/50 hayawezekani as long as mwanaume anatimiza wajibu wake 100%.

Kwakweli mnatuharibia sana vijana.
 
Alichofanya huyo Mwanaume kumficha mke wake unaona sahihi
Kakosea sana kumficha,

Maana kumuogopa mkeo unaemwinamisha na kumgeuza kila mkao, tena kila siku ni ULOFA ulopitiliza.

Ila
Kumficha huenda ni matokeo ya tabia mbovu za Ubinafsi, roho mbaya na ukatili za uyo mwanamke anazoonesha kwa mumewe.

Jamaa akaona isiwe tabu,
Mwanangu Akalelewe tu uko kwa dada angu, huenda atanyanyasika hapa.

Kwaiyo,
Isitoshe kusema tu uyo jamaa TAYAR KASHALISHWA KICHWA CHA KAMBALE.
 
Umeandika enzi inzo sio sasa ni 50/50
Ayo mambo yenu ya 50/50 ndio yametuletea kizazi cha wanaume laini laini kuomba omba ela kwa wanawake.

Kizazi cha wanaume kuvaa visuruali vya kubana,

Kizazi cha wanaume kujichubua ngozi,

Kwakweli mnatuharibia sana vijana.
 
Rafiki yangu alinihadithia mgogori kwenye ndoa yake japo chanzo nilipata kukijua miaka mingi iliyopita! Wakati rafiki yangu akiwa na miaka 19 alipata mtoto na msichana wa mtaani dogo enzi hizo alikubali lkn kumbe yule dada alikua na kadi mbili za clinic.

Mwanaume ni mpuuzi sana. Kama mtoto alimpata kabla ya kukutana na mkewe sioni sababu ya yeye kumficha mkewe.

Ukweli unamuweka mtu huru hata kama ni chungu.

Mwanamke pia atakuwa boya kuliko. Maana jamaa kwa hofu ya kumpoteza mke wake au kuepusha Shari aliamua kumficha ili wafaidi ndoa yao kwa amani. Ndoa hiyo ikivunjika kwa sasa naona mwanamke atakuwa bonge la ndezi.
 
Kakosea sana kumficha,

Maana kumuogopa mkeo unaemwinamisha na kumgeuza kila mkao, tena kila siku ni ULOFA ulopitiliza.

Ila
Kumficha huenda ni matokeo ya tabia mbovu za Ubinafsi, roho mbaya na ukatili za uyo mwanamke anazoonesha kwa mumewe.

Jamaa akaona isiwe tabu,
Mwanangu Akalelewe tu uko kwa dada angu, huenda atanyanyasika hapa.

Kwaiyo,
Isitoshe kusema tu uyo jamaa TAYAR KASHALISHWA KICHWA CHA KAMBALE.
Alimficha mkewe kwa sababu alikuwa anapasha kiporo kwa huyo mzazi mwenzie huo ndio ukweli.
 
19 + 22 = 41.
41 - 16 = 25.

Mwambie rafiki yako nimegundua miaka aliyoishi nje ya ndoa ni mingi kuliko aliyoishi ndani ya ndoa.
Kwa umri walionao wala usihangaike kuwashauri muda utakuwa mwalimu mzuri kwao, wasipoyamaliza wenyewe kuna kitu watajifunza.
 
Mwambie huyo fala awe mwanaume...Anamuogopaje mkewe kwa kitu ambacho wala sio kosa,asimame upande wa mtoto wake huyo mwanamke hataondoka anatikisa tu kiberiti kupima upepo.
 
Tatizo ni mwanaume muongo asingemkana mwanae maana alipatikana kabla ya ndoa
 
Na vipi kwa wanaume wasiotimiza wajibu wao 100%? Yaani yeye akiweka mezani laki mke naye aweke laki yeye akilipia bill ya umeme mke alipie bill maji hiyo imekaaje hapo?
Uyo atakua sio mwanaume wa kiafrika,

Ukiona mwanaume anaendekeza uzungu na kuutelekeza uafrika.

Mwache apambane na hali yake uko mbele ya safar.
 
Nimepitia maoni ya watu hapa wengi wanaona kama mwanaume anatatizo au kipato hana! Sio kweli income ya rafiki ya gu ipo vzr tu na huyo mtoto hakusoma hata shule moja ya kayumba amekua bording Hadi anamaliza form six. Likizo tu Ndio anaenda kwa sister wake na pamoja na hayo familia yake ipo vzr. Kabla ya corona mkewe birthday alipelekwa Paris Wiki nzima!kiufupi wapo vzr. Sema rafiki yangu uzungu mwingi! Na mke anaona Mali zitagawika sana endapo itatokea kifo!
 
Namshauri akubali kuwa ana mtoto, amtambulishe kwa wadogo zake halafu amruhusu mkewe aamue litakalompa furaha hata kama ni kuivunja ndoa ila baada ya kumuomba samahani kwa kumficha maana hakupaswa kuficha....
 
Huyo mwanamke ameichoka hito ndoa. Kuna namna anaona hakuna jipya miaka nenda rudi. Baada ya kutokea hili kosa .... anashikilia hapo moja kwa zote. Mwanamke tayari ana Plan B baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom