Ndoa ya mama PHD na baba standard seven

waoane tu, mwanaume anaweza kujiendeleza kimasomo la sivyo wanaweza wakaishi vizuri tu.
 
Kwa nini...mbona ni very possible....32 miaka mingi sana kwa anayesoma moja kwa moja....


 
Mimi sioni tatizo...kama wanapendana waendelee...kwa sababu ndoa zenye matatizo ni nyingi sana...unless tuseme matatizo ya ndoa yanatokana na mke kumzidi mume elimu....which is not true kwani nyingi za hizi zenye migogoro elimu ni sawa au baba amezidi elimu...

Mwache ajaribu bahati yake...utashangaa wanakuwa mfano. ndoa kutodumu hakuna formular ambayo ni absolute ingekuwepo baaasi watu wangeifuata na wasingetengana kamwe. Tunachofanya ni guess work tu...
 
Kwa kweli itategemea sana na busara ya mwanamke. Na kama yeye mwenyewe ameishaanza kuwa na wasiwasi kuwa huenda hapo baadae wanaweza kuwa na reasoning/understanding tofauti katika mambo kutokana na tofauti kubwa ya elimu zao plus possible inferiority complex kwa upande wa mume, ni bora wasioane.

Classmate wangu chuo kikuu alikuja chuoni akiwa ameolewa na kijana aliyesoma mpaka form IV tu na walikuwa na mtoto 1. Tulipofika second year mdada akadai talaka kwa madai kuwa hawezi ku-reason na mumewe. Ila pia alikuwa amepata boyfriend wa chuo ambaye walioana walipomaliza chuo.
 
Sometimes ukweli ni mchungu lakini hauna budi kukubalika.... Mwanzoni wataona rahisi lakini kuna kile kipindi cha kuvutana mashati in the fourties!!!!!
 
Enyi mpendanao oaneni kwa raha zetu na muishi kwa amani hiyo inferioirty na superiority ni hakuna kitu maana kama mnajuana elimu zenu za sasa na mmezikubali shida haipo. kama mnadhani elimu ni kikwazo kwenu ninyi ni sawa ila si kwa kile watu wanachangia eti.
 
yoote semeni ila msingi wa ndoa ni upendo hata akiolewa na PHD mwenzake kama hakuna upendo ni zero.
 

Tofauti kubwa mno...haifai! Hata kwa mwanaume mwenye PHD na mke darasa la saba ni tabu....
Uhusiano una kitu kinaitwa compatibility! Hawa sio compatible, hawawezi kuongea na kuelewana kwa amani.
Nadhani huyo dada yuko desperate kuolewa, so she will take anything!
 

Ishakuwa jioni Limited Access, wewe unataka kumshauri jambo tofauti na kuolewa? Kwa umri alionao na mtoto 1....kama kweli anampenda huyo jamaa nae anampenda kwa dhati "Elimu itabakia Juu jamaa atafaidi Chini"....Kuna wanawake walioolewa na wanaume wa namna hii na wanaishi vyema kabisa, muhimu mwanamme ajiamini na mwanamke asitumie elimu kama fimbo.
 
Huyu ana PHD anashindwaje kuamua case ndogo kama hii!
 
Kinachotakiwa na kila mmoja kusoma strengths za mwezie na kuzi-appreciate! Kuwa na Poor hair Distribution (PhD) siyo issue sana ilimradi hiyo elimu iwe mbele katika kila jambo. Kuna mambo yanahitaji tu elimu ya kuzaliwa (common sense) na siyo PhD wala STD 7!

Inawezekana sana wamtangulize MUNGU kama wana imani inayofanana.....
 
Kwa mwanamume aliyesoma mpaka darasa la saba na "kuridhika", sidhani kama anaweza kufikiri hata "kuoa"...!
 

How did you sort this? What happened? Je walioana?
 
ushauri wa maana huu.

 


Ndoa ni taasisi inayojitegemea,hela,shule,miaka etc haviwezi kuzuia watu kupendana na kuoana,heshima,kuvumiliana na maelewano ndio siri kubwa ya mafanikio katika ndoa
 
Mhhhhhhhh...nnachojua heshima ya mume iwekwe mbele kama tai,sasa hyo disparity ya kielimu,mhh sijui
 
ndio maana ndoa zinakufa sababu ya kuthamini elimu badala ya upendo ndoa si pesa wala elimu mbali ni maelewano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…