Ndoa nzuri na yenye raha mustarehe

Ndoa nzuri na yenye raha mustarehe

Hayuko sahihi
Ni kosa ndugu wa mke kumuingilia mke kimaamuzi
 
Nilikuwa naongea na jamaa yangu kuhusu masuala ya ndoa na changamoto zake, jamaa ameniambia ndoa nzuri na yenye raha mustarehe ni ile ambayo Wakwe wamefariki. Anasema alikuwa anapata changamoto kadha wa kadha hapo zamani lakini baada ya wazazi wa mwenza kufariki saivi anaishi kwa raha mustarehe na anafurahia ndoa yake masikilizano yapo, akitoa oda mambo yanatekelezeka, akifoka anasikilizwa.
Huyo ni mnyanyasi nimemkumbuka Me too my love
 
Nilikuwa naongea na jamaa yangu kuhusu masuala ya ndoa na changamoto zake, jamaa ameniambia ndoa nzuri na yenye raha mustarehe ni ile ambayo Wakwe wamefariki. Anasema alikuwa anapata changamoto kadha wa kadha hapo zamani lakini baada ya wazazi wa mwenza kufariki saivi anaishi kwa raha mustarehe na anafurahia ndoa yake masikilizano yapo, akitoa oda mambo yanatekelezeka, akifoka anasikilizwa.
Hii labda kwake tu. Mi wakwe wapo wala hamna shida. Halafu aache ufala hayo sio maneno mazuri.
 
mawazo ya waturutumbi haya.mzazi wa mwenzio afe kisa ndoa yako iwe na amani?
kwani ulishikiwa bunduki kumuoa huyo mwanamke?
 
Huyo hayupo sawa kiakili, anahitaji matibabu. Unawaombeaje kifo waliokuzalia/kulelea unayemwita Mkeo au Mumeo?.
Kama siyo matibabu basi anahitaji Maombi, tena ya kufunga kabisa.
 
hahaha, huyo rafiki ako ana tatizo
sio baba wa familia kumbe wakwe zake ndio walikuwa kichwa cha familia, kafurahi paka wameondoka ndio panya anajipa kichwa
 
Back
Top Bottom