Ndoa nyingine wanaishi kama 'hostel'

Ndoa nyingine wanaishi kama 'hostel'

Uko sahihi maana dhana hii kwa sasa imechukuliwa juu juu tu imefanywa kama fasheni.. wakati inamaana pana sana kiutamaduni, kisheria na kiimani.
inabidi vijana waelezwe kwa undani maana ya ndoa .. sababu kwa sasa imekuwa kama mashindano vile fulani kaolewa au kuoa na mimi nataka kufanya the same huku wakiwa hawajajiandaa... wengine hudhani wakiolewa ndiyo matatizo yao yataisha au ndiyo watapata uhuru kumbe kuoelewa ni familia nyingine yenye matatizo yake mapya yanahitaji uangalizi wa namna yake .. Mungu atusaidie vijana kwa kweli
 
Inachosha kugeuka mwalimu wa kila siku, ubishi na ujuaji wa wanawake wa siku hizi unakatisha tamaa katika kufikia makubaliano y pamoja.
Wewe ulitaka kujua kipi, sababu ziko wazi... zimewekwa wazi, huna namna zaidi ya kukubaliana na mwenzi wako mnaishije katika utandawazi
 
Yote hayo ni kwa sababu ya kuupoteza utamaduni sasa kama kijana katahiriwa na mama yake kwa nini asiwe marioo? Huwezi kukuta mwanaume alie enda jando na kula kisu bila ganzi akawa marioo
Kweli kabisaaa 100%
 
Sifa za kichwa cha nyumba mmeipoteza wanaume wengi, unaishi kwenye nyumba hujui pango ni bei gani, unafungua fridge unatoa beer hujui mke wako ametoa wapi pesa. Hata wife akikwambia anakwenda seminar huna hata nguvu ya kuuliza utakaa muda gani.
 
Inachosha kugeuka mwalimu wa kila siku, ubishi na ujuaji wa wanawake wa siku hizi unakatisha tamaa katika kufikia makubaliano y pamoja.
Utashindwa iwapo unataka mwanamke asiyehoji kitu, wa kusema ndio baba kwa kila neno unalosema... mwanamke wa sasa amekuwa exposed kwenye mambo tofauti na wa zamani, kuanzia watoto wadogo wanavyolelewa sasa wanapewa uhuru wa kuamua vitu na wazazi wanatekeleza, haiwezekani ukubwani akubaliane kirahisi kuamuliwa mambo.
Muelewe tu huyo mwenzi wako kama hutaki headache
 
Lakini pia zamani, ndugu zako wa kijijini ulikuwa unawatumia pesa kwa TMO inachukua mwezi mzima. Siku hizi, kwa M Pesa ni sekund kadhaa tu. Zamani, Dar - Mwanza ulitumia reli ya kati kwa siku 3, siku hizi ni masaa 12 tu kwa basi uko Mwanza. Zamani hakukuwa na Whatsaap, radia ilikuwa moja, gazeti la chama na serikali. Siku hizi taarifa zote unazipaata papo kwa papo kupitia Whatsapp na mitandao mingine ya kijamii. Tena haijalishi, aliye Kasulu, Tandahimba, Mererani, Dar, Tanga, Nairobi, New York, Tokyo au Madrid, as long as wote mko group moja la mnapata taarifa kwa pamoja.

Kifupi ninachotaka kusema ni kwamba, zama zimebadilika sana. Angalia maisha ya zamani, ukitaka kumtongoza mwanamke, inabidi umvizie anaenda kisimani, au dukani. Lakini siku hizi watu wanatongozana hata kama hawajawahi kuonana, ni kwa sababu ya mawasiliano kuwa rahisi. Wanandoa zamani ilikuwa vigumu ku cheat kwa kuwa ni ngumu kupata mawasiliano na mke au mume wa mtu. Na ukienda naye guest kila mtu atajua kwa kuwa watu walikuwa wachache. Siku hizi hayo yote yamerahishwa.
Kwani huo utandawazi umeanzia tanzania pekee? Nigeria hakuna? lesotho hakuna? afrika kusini hakuna? Mbona hao wanaheshimu utamaduni wao na pia wameushikilia?
 
inabidi vijana waelezwe kwa undani maana ya ndoa .. sababu kwa sasa imekuwa kama mashindano vile fulani kaolewa au kuoa na mimi nataka kufanya the same huku wakiwa hawajajiandaa... wengine hudhani wakiolewa ndiyo matatizo yao yataisha au ndiyo watapata uhuru kumbe kuoelewa ni familia nyingine yenye matatizo yake mapya yanahitaji uangalizi wa namna yake .. Mungu atusaidie vijana kwa kweli
Cha kushangaza zaidi watu wenye maarifa zaidi ya ndoa ndio ndoa zao zenye shida zaidi
 
Kuhoji we hoji ila kunavingine ubishi tu unaambiwa hivi usifanye unajiti ujuaji maandazi mwisho wa siku jambo linaharibika, ukisema bado ubishi tu ooh ni bahati mbaya hata kule kujishusha kwamba kweli hapo nilichemsha hakuna. Then unalalama ooh sisikilizwi!
Utashindwa iwapo unataka mwanamke asiyehoji kitu, wa kusema ndio baba kwa kila neno unalosema... mwanamke wa sasa amekuwa exposed kwenye mambo tofauti na wa zamani, kuanzia watoto wadogo wanavyolelewa sasa wanapewa uhuru wa kuamua vitu na wazazi wanatekeleza, haiwezekani ukubwani akubaliane kirahisi kuamuliwa mambo.
Muelewe tu huyo mwenzi wako kama hutaki headache
 
Hahaha Ndio maana tunaogopa kuoa na kuamua kuishi kisela tu.
 
kwani mlipokuwa mnalalana ulikuwa hujui ataconceive, upewe taarifa gani? ndo nyie mnaowatoa mimba wake zenu wa ndoa.
Mtani, swala la kutafuta mtoto ni la kukaa na kujadiliwa na wote. Mkikubaliana kuwa "it's time to conceive", ndio muanze mchakato.
Sitamuelewa wife akisema yupo pregnant wakati hatukujadili, wakati I do keep track of her cycle.
 
Tartibu jamani!, watu tunataka kujisajili rasmi ktk zizi mwaka huu
 
Back
Top Bottom