Ndoa nyingine wanaishi kama 'hostel'

indelible

JF-Expert Member
May 2, 2015
652
299
Salam wakuu,

Leo nimemkumbuka mwalimu wangu wa somo la siasa enzi hizo kabla ya kubadilishwa na kuitwa uraia. Alikuwa ananiambia 'Doa' tamaduni mbili zikikutanishwa moja yenye nguvu huimeza iliyodhaifu.

Ili imezwe lazima mmoja aidharau yakwake na kuitukuza ya mwenzie akaniambia wazazi wako na babu zako walishikilia sana tamaduni zao, kuanzia lugha, mila na desturi lakini ninyi mmeanza kuruhusu kumezwa.

Hoja yangu ni ipi haswa.Kwa sasa ndoa zetu zipo mashakani kufikia umri wa ndoa za waliotutangulia hasa wazazi (wenye ndoa) waliishi kwa kuelewa ndoa ililindwa na utamaduni wao wakauenzi

Kwa sasa wanandoa wanaishi nyumba moja kama wako hostel tu na sio familia. Kisa wameruhusu umagharibi kuumeza utamaduni wao.

Mama anadai haki zote za ubaba, na kinyume chake. Hakuna kiwiliwli wote wamekuwa vichwa.

Tafakari.
 
Ulimwengu wa Kambare kila mtu ana masharubu,mi sishangai sana nnavyoona wanaume tunaoa sio kwa kupenda bali kwa kuridhishwa kwa muda mfupi na vijitabia vya mchumba ili umuoe,na wengi tunaona ufahari sana kutangaza ndoa maana sio mchezo hiyo attention yake ukweni we ndio unakuwa topic+na mchumba ndio kama mlenda na tonge kwa ufupi ndoa siku hizi ni kama hobi tu.Hazina muelekeo wa kimaisha.
 
Na kipindi kile cha zamani mali zote zilikuwa chini ya baba, mashamba wakina mama wanaenda shamba kulima yakifikiwa kuvunwa mama hana chake ni ya baba kwa maana ingine uchumi ulikuwa ukimilikiwa kwa asilimia yote na wanaume na ukijumlisha na maadili ya enzi zile basi baba lazima awe kichwa cha familia tu...Sasa hivi hata sisi wanaume tunachangia kuporwa haki yetu ya kuwa kichwa cha nyumba..Mwanaume huna na hutaki kazi unalelewa tu na mwanamke uchumi wa familia anaushikilia mama wewe unabaki kumpeleka kazini then unazunguka tu na gari la wife mtaani hadi pesa ya nguo za ndani ni yeye anakupa...Hii tabia ya umarioo inatuaribia sifa zetu sana..Mwanaume umepaka rangi na umefuga kucha..Halafu uitwe kichwa cha familia...
 
Umeongea point sana... ndio umezwaji wenyewe

Yote hayo ni kwa sababu ya kuupoteza utamaduni sasa kama kijana katahiriwa na mama yake kwa nini asiwe marioo? Huwezi kukuta mwanaume alie enda jando na kula kisu bila ganzi akawa marioo
 
Kuna kabinti fulani kaliolewa haraka haraka kisa kumwonyeshea ex bf alieoa kwamba na yeye anaweza kuolewa... ndo najiuliza hiyo ni ndoa au kisasi? Na nini msitakabali wake?
Ulimwengu wa Kambare kila mtu ana masharubu,mi sishangai sana nnavyoona wanaume tunaoa sio kwa kupenda bali kwa kuridhishwa kwa muda mfupi na vijitabia vya mchumba ili umuoe,na wengi tunaona ufahari sana kutangaza ndoa maana sio mchezo hiyo attention yake ukweni we ndio unakuwa topic+na mchumba ndio kama mlenda na tonge kwa ufupi ndoa siku hizi ni kama hobi tu.Hazina muelekeo wa kimaisha.
 
Swala la kuongeza familia ni swala la kujadiliana sio we unaamua then Mumeo anageuka mpewa taarifa tu!
Mwanamke anapata mimba mda wowote provided the right conditions ( maturity, egg, sperm, balanced hormones) utamlaumuje kwamba kaamua... Wewe si ungetumia condom au ufanye vasectomy basi kama unataka kujihakikishia hazai.
Mwili wa mwanamke huweza kupata mabadiliko ya vichocheo muda wowote kutokana na stress, mazingira na lishe hivyo unapolala na mwanamke hesabu mtoto maana anaweza kutokea hata nje ya hesabu ya siku za hatari zilizo-zoeleka.
 
Back
Top Bottom