Ndoa ni kujitoa Sadaka na Uvumilivu

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,704
Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke, mkewe akakataa. Akamwambia baba yake akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa zina mengi. Akawa kila siku analalamika kwa babaake, mwisho babaake akamwambia basi nitakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi hujiwezi halafu nitakuonesha jawabu!

Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha kikao cha ndugu wote pande 2, Mzee akaanza kueleza jamani kijana wetu anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital zote imeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga wa jadi amenipa dawa na ina masharti. Inatakiwa atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye ndoa ambaye hajawahi kutoka nje ya ndoa tangu alipoolewa ndio kijana wetu atapona. Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii kwa sababu tukimpa kijana wetu watakufa wote.

Je, kina mama nani ataandaa? Walitoka nje wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana, mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia wanaume peke yao.

Mzee akamwambia mwanangu umeona hali za ndoa zilivyo? Acha kujisumbua tulia na mkeo nadhani umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako. Kijana akazimia!
 
Tafuta pesa kijana, mpe pesa mkeo! Mpe pesa, yaan akigeuka pesa halafu chumbani hakikisha mkeo hana nguvu ya kuita maji!! Aite mma!!

Akichepuka hapo, zimia!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom