Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,684
- 8,761
^^
miss neddy tukio hili lililoripotiwa halina tofauti kabisa na ule ukatili aliofanya mwanaume mmoja mwaka jana kwa Bi. Rehema (rejea mada ya Ablessed) tukio lile lilipoletwa hapa jukwaani, asilimia kubwa ya wachangiaji wakiwemo hawa wanaonikana leo, walilaani wanaume na kuweka wazi mwanamke ni mwenye huruma hawezi kufanya ukatili kama huo! Niliwabishia sana,, Leo mmejionea! Na kwa kuwa ni mwanzo wa kutafuta haki zenu (bila kujali ni halali au vinginevyo kama ambavyo wanaume wanavyowa humiliate kwa madai yenu) huoni kuwa huu ni ushindi kwenu?
^^
kuna mtu alishatetea wanawake kudai haki za mali kwa njia ya kufanya vitendo vya kinyama, humu ?
Au tatizo lako haswa lipo kwa wanawake kudai haki zao za kumili nyumba na mali? Ila unatafuta njia ya kuchafua hilo kwa kulink na vitendo vya kikatili?
ushindi gani ??????? wa kumwagia mumeo mafuta kisa nyumba tena mume alikuwa na mikakati ya kumjengea yake
staki unilazimishe kuamini huu ni ushindi ni zaidi ya ukatili Himidini mbona unataka kutulazimisha tushangilie ukatili kisa aliefanya ni mwanamke anaedai haki ambayo hata mimi nisiejua sheria kwa undani naona haimuhusu
^^
Tatizo ni kuwa natumia simu,, hoja yangu ni kuwa wanawake humu jukwaani wamekuwa wakiona kuwa wanaume pekee ndio viumbe katili na wao ni viumbe wema! Nenda kwenye mada alizowahi kuanzisha Ablessed kuna mada ya issue ya Bi Rehema
utajua nalozungumza
^^
mwenzetu na kina nani
at the end of the day kila mtu atabeba msalaba wake mwenywe
and me i dont see any reason as kwanini nishangilie....why should I!!!!!!!
^^
Hamkawii kugeuka! Leo ndo mnasema huwa hamtetei wanawake wenzenu??
I can't believe this
^^
Vitendo vya kikatili haviendi na jinsia. Ingawa mara nyingi kwenye jamii zetu wanawake ndio wamekuwa wakiwa victims.
Ila hilo halimaanishi kuwa hakuna wanawake ambao wanafanya vitendo vya kikatili.
Anyhow, vitendo hivi havina ushabiki, hapo ndio unapokosea.
Vitakemewa kama vitendo vya kikatili, bila kuangalia jinsia iliyotenda.
^^
Haya ni matokeo ya jitihada zenu dhidi ya mfumo dume! Yakubalini japo leo mnayabatiza jina la ukatili.
^^
mhh kutetea haki doesn not mean mtu atumie abusive ways kama hizo
we can still advocate our rights but through peaceful ways
^^
Vinapokemewa vikaleta matokeo haya, tuviite ukatili?
^^
Mkuu pole sana, on behalf of huyo mwanamke naomba nimuombee msamaha kwako.
Naona amekuchafua mnoo mpaka ukashindwa kuwa reasonable.
Im sure haki itatendeka mkuu, atachukuliwa hatua za kasheria.
^^
Hakunichafua ila tu najifunza kupokea matokeo ya mfumo wetu dume, napopokea matokeo haya kwa huzuni, nyie furahieni kisasi dhidi ya mfumo dume
^^
Hatuwezi kufurahia hiko kitendo kamwee, acha kujishtukia.
^^
Nijistukie ili iweje? Kwa faida ipi? Mwanaume unapoishi na mwanamke ndani lolote laweza kutokea (na kinyume chake)
Akuwaniae uovu haji kweupe, na atimizapo haja yake, anastahili pongezi. Hii ni vita kati ya wanaume na wanawake, na upande upatao ushindi wa hatua fulani, nini kizuie furaha yao?
^^
Hamna vita mkuu. Acha kututisha bwana. Mbona tunaishi vizuri tu na nyinyi?!
Yaani hili ndio linakufanya uongee yote haya?
^^
We unaona hili tu !!
Mbona nyinyi tukifanya haya mnakuja juu? Mimi nimekubali kuyapokea matokeo. Usikatae kwamba hakuna vita. Penye moshi pana moto
^^
Hamna vita mkuu. Just take it easy. Huyu mama atashughulikiwa kulingana na matendo yake.
Ni shetani tu alimpitia.
Mfumo dume kuna taasisi kabisa za kideal nao, sio mafuta ya moto.