Ndoa na mkono wa sweta

Ndoa na mkono wa sweta

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
18f9b5e916e85e24a8f6c5d680f83297.jpg

Nimezaliwa katika jamii ya wafugaji

Utamaduni wa jamii yangu hapakuwa na mtu aitwae Ngariba

Makuzi yangu hayakuwahi kunifahamisha kuwa binadamu akishazaliwa kuna fundi ambae uyarekebisha maumbile sahihi ya Mungu kwa kudondosha mkono wa Sweta. Elimu yangu ya kidato cha kwanza pale Mirambo secondary ilikutanisha na viumbe wa sayari nyingine kabisa katika maisha yangu hasa pale tulipojumuika bafuni kila mmoja alinishangaa mimi kwa jinsi sehem zangu siri zilivyokuwa. Mbali na kunishangaa wengine walinikebehi kwa kuniita jina baya la mzee wa Zunga.

Jambo la kuonekana wa pekee pale shuleni mwanzoni lilinikera sana hadi siku moja niliporudi likizo nilitaka kuacha kurudi school kutokana na kebehi za wadau wa pale shule. Japo nilikuwa na uhakika katika masomo yangu pale shuleni sababu wale walionikebehi darasani waliniomba msaada maana uwezo wa kielemu haukujali Jando au kutokwenda Jando.

Baada ya kuhitimu form four matokeo yalipotoka nilikuwa nimepangwa shule ya secondary Pugu ni rafiki yangu Chacha ndio tuliofanikiwa kujiunga nae pale Pugu secondary kwa masomo ya kidato cha tano.

Japo tatizo langu la kuwa na mkono wa sweta nilikwisha lizoea sikujali chochote lakini sikuhitaji kadhia ya kidato cha kwanza nililazimika kuoga peke yangu siku zote ili my secret isivuje daima.

Siku moja nikiwa mtaa wa Msimbazi nilimsikia bwana mmoja akiuza dawa ya nguvu za kiume na kutokana na matangazo yake nilivutiwa na kumsogelea baada ya kuelewa kile alichokuwa anahubiri nilijenga hisia moyoni na kuamini kuwa mtu akidondosha mkono wa sweta basi nguvu zake za kiume zinapotea.

Sikutamani milele kufanyiwa tendo hili kwanza nilianza kuwaona wale waliofanyiwa kama wakosefu mbele za mungu sababu tendo lao nilihisi lilikuwa ni tendo la kumdharau Mungu kwa kuondoa sehemu ya uumbaji wake
nilijiamini nakujiapisha kuwa endapo ningekufa na ukamilifu wangu Mungu angeniteua katika kuwaadhibu wale waliopunguza kile alichowatunuku katika miili yao.

Siku moja nikiwa likizo nilianzisha mada mbele ya kaka zangu kuhusu vijana wa mjini na tabia yao yakukata sehemu ya mwili wao eti ndio tohara. Kaka zangu waliwacheka sana wakaniambia mtu anaekata hizo sehem anakuwa mswahili na waswahili hupenda kukutana sana na wanawake lakini nguvu zao zinakuwa ndogo kwa sababu ya wao kutoa ile ngozi ndipo nilipomkumbuka yule tabibu wa mtaa wa Msimbazi na dawa zake za nguvu za kiume.

Hakika kutokudondosha mkono wa sweta kulinifanya kuwaogopa wasichana niliowapenda hasa baada ya kukutana na baadhi ya warembo wa fikra zangu nao baada ya kugundua udhaifu wangu wengine walinigomea kuduu nao na hata wengine kunitoroka ktk vyumba gest baada ya mimi kuwaonyesha urijali wangu wakutunza tunu ya Manani.

Umri wangu wa kuoa ulikuwa ukikimbia kwa kasi huku binti wakikubali umbile langu la mkono wa sweta nikiwa simpati japo niliwapata mabinti walevi wao hawakujali bali walijali pesa na pombe lakini nilipowarudia Mara ya pili waliishia kunidhalilisha sikuweza kuwatamani tena mabinti wa mjini.

Nirudi kijijini na kuwaeleza wazazi juu ya dhamira yangu ya kuoa pale kijijini hakuna binti ambae angenikatalia kwa hadhi niliyokuwa nayo kila familia ilinijua kutokana na usomi wangu. Nilikuwa mtu maridadi nikivaa suti za bei japo usingeweza kujua ustarabu wangu niliouhifadhi katika suruali yangu ya gharama.

Baada ya juhudi za familia yangu nilibahatika kumpata binti wa kijiji cha jirani baba alipeleka mahari ya ng'ombe 30 ndipo nilipokabidhiwa mke. Mwanzoni mke wangu hakujali mimi kuwa katika hali ile lakini baada ya miaka sita ya ndoa mke wangu alianza kudai kuwa na mkera kwa kuwa mimi nina mkono wa sweta.

Kwa kuwa jamii yetu mwanaume hakusifiwa kwa kudondosha mkono wa sweta niliamini kuwa mke wangu alikuwa amempata mswahili na kumuonjesha iliomenywa. Japo sikumwambia hisia zangu lakini kadri siku zilivyokwenda tendo la ndoa kwangu nilianza kulisoma kwenye magazeti, nilijitahidi kumuasa mke wangu kuhusu tabia yake hiyo lakini haikuwa rahisi kunielewa na hatimae aliondoka na kuniambia kama nampenda nikadondoshe mkono wa sweta.

Kwa umri wangu huu miaka 48 naona ni kujidharilisha mbele ya Dr
kiukweli napata shida sana katika hisia zangu naamini kupitia Uzi huu kuna wadau ambao nao walichelewa kushusha japo wengi huduma hiyo uipata kutoka kwa walezi wao hadi wanakuwa watu wazima hawajui nini kilifanyika hadi wakawa hivyo lakini naamini kuna idadi kubwa tu ya watu ambao wanaishi kwa mfano wangu je nao nini ambacho ukumbana nacho.

By R.Nzagamba
 
Hakuna kitu kinaumiza kama kukataliwa na binti kisa una mkono sweta[emoji53] ila kwa umri ulionao unaweza kutahiriwa japo utahisi kama fedheha mbele ya nesi au daktari Ila jikaze mpaka hospital ukifika pale toa fikra ya aibu na jivike ugonjwa siriazi utahudumiwa vizuri kabisa[emoji114]kila la kheri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushauri nenda kituo chochote cha afya ambapo unadhani huduma hii hutolewa , secretly muone nurse yeyote Wa kiume mweleze tatizo lako atakufanyia huduma hii hata nyumbani kwako ikiwezekana kikubwa makubaliano matakayo afikiana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda hospital ongea na dr mwambie akufanyie hata nyumbani maana kama ni hospital lazima nurse atakuwepo mkuu si una gari nenda na mkeo unafanyiwa kisha huyo kwenye gari kwani hapo hospital watakukalili mficha uchi hazai wewe sio wakwanza, pole sana mkeo naye tatizo analikimbia ushamba tu kaja mjini kawa kwale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo makala sijaisoma, ila sipo mbali na wachangiaji waliotangulia. Muite dokta aje kwako alikate, wiki moja tu ushapona. Uli ho nkoi.
 
Kuna jamaa mmoja wa Mbeya alifanyiwa pale the Hill/ Mlimani tatizo alikuwa analia sana na utu uzima wake na usomi wake wote but alipona mpaka sasa ni mheshimiwa sana . Nenda katoe govi mkuu usiogope mkeo kakuvumilia sana usije ukaanza kumnyanyasa kwa akina gigy money.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom