Bradha
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 8,786
- 45,268
Habari wana JF
Nimekua nikitafakari namna ambavyo baadhi ya mambo yamekua yakifanywa na wanandoa au marafiki zao licha ya kuwa mambo hayo ni
kinyume na matakwa au ustaarabu wa ndoa.Baada ya tafakuri hiyo nimejikuta nikikumbuka maneno haya ambayo tumekua tukiyasikia
sana tuu,"Ndoa na iheshimiwe na watu wote".
Inawezekana leo wewe ni mme/mke wa mtu na bahati mbaya ulishawahi kuwa na mahusiano kabla.Tafadhali, usiendeleze mahusiano au mazungumzo ambayo ni kinyume na matakwa ya ndoa.Kuwa wa kwanza kuiheshimu ndoa yako.Sio sahihi kuendelea kuitana majina yale ya kimahaba, kuzungumza mahaba hata kama mnatumia codes ambazo mnaelewa ninyi wenyewe.Jumuika na jamii(marafiki, wafanya kazi wenzako, majirani n.k) ukiwa kama mme/mke wa mtu.
Inawezekana una rafiki yako ambaye sasa hivi ni mme/mke wa mtu.Pengine ulikua unamshirikisha katika mambo ambayo unajua sio sahihi kuendelea kumshirikisha kwasababu ameshafunga pingu za maisha na mwenzi wake.Naomba kukuomba kuwa usimshirikishe tena.Ndio, ni mtu mzima na ana uwezo wa kukataa mwenyewe pale utakapomshirikisha ila nnachokuomba ni umpunguzie majaribu, usimshirikishe katika mambo unayojua mke/mme wake akijua ataumia kwamba kakosewa heshima.Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Mkuu inawezekana mahusiano uliyonayo saivi ni mahusiano na mke/mme wa mtu.Pengine uliyaanzisha kwa kujua kua huyo ni mme/mke mtu au pengine hukujua na umekuja kujua hivyo baada ya kuwa naye kwenye mahusiano.Ninachokuomba leo ni ujitafakari na uchukue maamuzi sahihi.Usikubali kuwa chanzo cha huzuni kwa mke au mme wa mtu.Kama unampenda huyo mke/mme wa mtu basi iheshimu ndoa yake na ukae mbali.Ni ushauri tuu.
Inawezekana kwa bahati nzuri au mbaya umefanikiwa kujua siri za ndani za ndoa ya rafiki au ndugu yako.Pengine alikuamini akakuambia matatizo yake au mapito wanayopitia katika ndoa yao.Tafadhali, usiwe wa kwanza kwenda kuwasema pembeni na kuwakejeli na badala yake angalia kama kuna namna ya kuwasaidia.Ndio, inawezekana anaibiwa mme/mke wake lakini kwanini unashangilia na kumcheka.Nyumba kubwa akisikia mchepuko mtaani anasifiwa atajisikiaje?Inakufaa nini kuyaweka matatizo ya mwenzako hadharani?Iheshimu ndoa yake na ujitahidi kuwa sehemu ya ufumbuzi kwa kadiri utakavyoweza.
Wakuu tupendane.Tusiishi kwa kunyoosheana vidole, haitatufaa kitu.Tujitahidi kujali wanaotuzunguka na kutenda kwa wema kwa kadiri Mungu anavyotujalia.Ni kweli, duniani tupo watu wa namna mbalimbali ila mimi na wewe tunaweza kusaidia kwa kuwa wema.
Nawatakia wiki njema.
NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.