Mithali 14:1 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe
1. Hudharau hekima na ushauri.
Mithali 1:7Kumcha BWANA ndiyo chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. 2. Huchukia maarifa ya kiMungu.
Mithali 1:22 "Enyi wajinga, mtang'ang'ania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha na wapumbavu kuchukia maarifa? 3. Humhuzunisha mama yake.
Mithali 10:1Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. 4. Mkamilifu machoni pale mwenyewe.
Mithali 12:15Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza shauri. 5. Hukasirika upesi.
Mithali 12:16 Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara, bali mtu wa busara hupuuza matukano. 6. Hapendi kuachana na uovu.
Mithali 13:19 Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya. 7. Mdanganyifu.
Mithali 14:8 Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. 8.Mkorofi na asiyejali.
Mithali 14:16Mtu mwenye hekima humcha BWANA na kuepuka mabaya, bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe. 9. Huwakasirisha wengine kwa maneno yake.
Mithali 18:7Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake na midomo yake ni mtego kwa nafsi yake. 10. Mgomvi.
Mithali 20:3 Ni kwa heshima ya mtu kuepa ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. 11. Hutapanya mali.
Mithali 21:20 Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo. 12. Hawezi kutatua migogoro yake.
Mithali 29:9 Kama mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani. 13. Huichochea hasira yake.
Mithali 29:11 Mpumbavu huonyesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia. Je ni wewe? Jihoji.