Ushauri mzuri siku hizi watu hawapigi tena wake zao, kuna sheria inalinda sana wanawake, suala la kurudi usiku wa manane au hata asubuhi kama umemuuliza bado hajirekebishi, umempeleka kwa wazazi, ndugu na bado hajirekebishi, kikubwa cha kufanya ni maombi tu, usimuulize tena chochote, mpe huduma zote kama mume, mwachie chakula kama kawaida hata kama hatokula, funga na omba kwa ajili ya Mungu ambadilishe mume wako, maana katika maandiko matakatifu yanasema 'Mwanamke atamlinda mume wake', na nina amini ukimwomba na kumlilia Mungu ukiwa umesimama (hapa hakuna cha kuwa na kidumu cha kukupooza moyo, kidumu chako kiwe ni Mungu na Maombi) nina hakika atajirekebisha tu. Mungu ni mwaminifu siku zote atakurudishia mume wako tena akiwa amebadilika, au Mungu atamchapa kiboko ambacho kitamfanya ajute aliyokuwa anakutendea. Kikubwa kwa wanawake usilipize kwa kuwa na spare tyre, hii itamfanya akimbie zaidi badala ya kurudi asubuhi basi atarudi baada ya wiki au hata mwezi tena kuja kubadili nguo tu. Ushindi katika maisha ni maombi tu. Nimeongea hivi maana nipo kwenye ndoa huu mwaka wa 19. Milima nilipanda, mabonde nilishuka lakini kwa maombi sasa hivi nipo kwenye tambarare kama vile ndo tunachumbiana, ila kitu kizuri kina gharama, ili ndoa isimame na iwe tamu ni kwa maombi, wanawake tusimame kwenye zamu zetu sawasawa, hawa waibjai wa ndoa za watu hawatomwona mume wako. Ni ushauri tu nimetoa.