Hawa wanandoa wameoana toka 2017 kipindi hicho mapenzi yalikua mubashara, (hadi nikatamani kuolewa

)ila 2018 baada ya kubarikiwa mtoto wao wa kwanza cousin yangu akaanza kukipata cha mtema kuni.
Mwanaume alibadilika kwa kasi ya 4G, harudi nyumbani, ulevi kupitiliza, mara mida ya kurudi ikawa saa nane au hata kumi na mbili, siku nyingine saa nne asubuh ndo jamaa anapatikana, na vipigo juu.
Huyu cousin wangu mara nyingi nipo nae tumekua pamoja, mambo yake mengi ananiambia,so do l.
Kuna kipind hata wakishiriki tendo la ndoa jamaa anamuita jina la mchepuko, ila kwa sasa huyo mchepuko kaachwa, kapata mchepuko mwingine MKE WA MTU.(cjui mumewe atakua ni member huku)sasa penzi ndo limedamshi, kurud nyumban ni mida mibayaa saa saba hadi kumi, alishampiga ndugu yangu kisa alimuonya kuachana na mke wa mtu, haambiliki haskii, cousin aligundua haya baada ya kushika simu ya mumewe na kukuta charting wanavyoelezana wanavyopendana, mara guest na lounge wanazoendaga, na miamala wanavyotumiana hela,
Hapo ndoa bado mbichi kabisa, mke analalamika mumewe akishanunua chakula basi tena kwa kusumbuana sana, mahitaji yake muhimu hana mpango nayo, kila siku hana hela(huwa najiuliza iweje shemeji alewe kila siku, kwenda guest na kumuhudumia mke wa mtu, afu nyumbani kwake aseme hana hela?)
Me nilichomshauri ajitafutie mchepuko tu ajiliwaze, cyo kwa stress hizo kukesha usiku kusubiri mtu hujui kama atakuja au analala huko, ila akiwa na mpango wa kando atamliwaza.




Wanajamvi, mnamshauri nini huyu.