Ndoa inayumbisha uchumi wa vijana

Ndoa inayumbisha uchumi wa vijana

Newera

Senior Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
132
Reaction score
202
Nilipooa ndipo nikagundua kipato changu hakitoshi.

Kuoa kunahitaji kujipanga sana, baada ya kuoa maisha yangu kiuchumi yalibadilika sana. Kuna mambo yalikuwa yanaenda poa kwa sababu nipo single, nikaoa mambo yakabadilika.

Kodi ya nyumba kutoka double hadi kwenye apartment, mdada wa kazi, bajeti ya chakula si mtu mmoja tena bali familia.

Niliumia kwa mwaka hadi kuanza kuhangaika nje ya kipato changu cha kawaida. Utanashati wangu uliisha kabisa, kununua nguo kila leo kukaisha, nikajifunza kuwekeza, kusave na kuishi kama mtu mzima.

Tuwaheshimu sana wanaume wanaomudu familia zao, tuwapongeze wazazi kwa kutulea. Usimlaumu aliyeshindwa mambo si mepesi, wanaume tupambane sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzako wakioa wakachanganya akili za wawili wanang'ara+vitambi wewe unachuchuka? Pole kwa kubeba mzigo wazazi wake wapumue.

Sent using Jamii Forums mobile app
Madame Mwajumaaaaaa..... mimi nilioa Housewife kabla ya kuoa nilikuwa na kilo 67 ndani ya mwaka nikafika 78 nikaanza kupiga na Gym, nilikuwa nimechoka sana hata ukiniangalia usoni unaona kabisa huyo broo kachoka. Baada ya kuoa nikawa full handsome. Nilikuwa nafanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana ambao sijawahi kuwa nao. Mabosi wangu walinielewa kwa utendaji kazi wangu wakanioa na cheo na mshahara ukawa double. Wafanya kazi wenzangu maofisini kila mara walinishangaa utendaji wangu. Wengine walidhani labda natumia Ndumba. Nilikuwa nang'aa kupita maelezo kuanzia mavazi unywele hadi unyayo. Kiufupi nikawa mtanashati. Mafisi( mademu wasangaji) wakaanza kunivizia kila mara ofsini na mitaani ilikuwa gumzo. Mafanikio yakaja haraka sana kuanzia kipato, kijamii, na kiprofessional.

Nilianza kufurahia maisha kuliko mwanzo. Mke wangu hakutaka kusikia H/girl ndani ya nyumba yake kwa kuwa nikuongeza gharama za bure wakati yeye ni H/wife.

Nilimpenda mke wangu kwa uchapakazi na mahaba aliyokuwa ananipa maana yameniletea mafanikio makubwa.

Wengi hawaelewi nilimpata vipi. Vijana wenzangu wakija kwangu wananiuliza eti vipi ulipataje Zali hivi ukapata mke huyu. Nikawambia sina fomula ni bahati tu. Lakini usije ukaoa na wew h/wife ukadhani ndio utafanikiwa , oa yeyote mwenye mapenzi mema utafurahia uumbaji wa Mungu duniano. Hapo sijataja neno lolote kuhusu mambo yaleeeeeee ya akina Madam Mwajuma.
 
Nilipooa ndipo nikagundua kipato changu hakitoshi.

Kuoa kuna hitaji kujipanga sana, baada ya kuoa maisha yangu kiuchumi yalibadilika sana, kuna mambo yalikuwa yanaenda poa coz nipo single, nikaoa mambo yakabadilika kodi ya nyumba kutoka double hadi kwenye apartment, mdada wa kazi, bajeti ya chakula si mtu mmoja tena bali familia.

Nliumia kwa mwaka hadi kuanza kuhangaika nje ya kipato changu cha kawaida, utanashati wangu uliisha kabisa, kununua nguo kila leo kukaisha, nikajifunza kuwekeza, kusave na kuishi kama mtu mzima.

Tuwaheshimu sana wanaume wanaomudu familia zao, tuwapongeze wazazi kwa kutulea, usimlaumu aliyeshindwa mambo si mepesi, wanaume tupambane sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio maana wadada wengi siku hizi wanatupenda sana sisi vijana wenye pete. Wanajua kabisa kwamba sisi ni watu makini, tuna vifua na tuna uwezo wa kupambana na maisha!!😉

Mimi siku zote hua nasema: Ukijiona una hela.. yaani kila ukienda benki unakuta salio kwenye account, hela ya matumizi, starehe nk haikupigi chenga.. basi ujue bado hujaanza kufanya mambo ya maana! Pindi utapoanza kufanya mambo makubwa kama kuoa, kujenga, kuwekeza nk utashangaa huoni tena senti tano kwn account.
 
Hapo ndo utagundua nidhamu ya pesa inahitajika,

Vijana tutulie kwanza haya sio kukurupuka.

Nna jamaa angu ushalobalo kwisha kabisa ameenyooka kishenzi

Mie bado niponipo kwanza,, nikiweza kumhudumia mrembo kwa 100% ndo nitaoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom