Ndoa inanishinda, naomba mnishauri kisheria

Uko sahihi wanataka kufanya watoto kuwa kitega uchumi cha yeye na wazazi wake!
Wewe muulize kwa meseji mzee unachotaka nifanye ni nini?
Akisema anamtaka mwanae muulize je na hawa watoto wadogo unawafikiriaje?
Akikujibu vyovyote tunza meseji.
Halafu waache waende zao using’ang’anie
We jamaa una ukili.
 
Ndoa ndoano acha wengi wastuke siku hizi kwenye hii issue ya kuoa.

Mkuu haya mambo ya migogoro ya ndoa Ninayoyashuhudia kwa marafiki hayanipi hamu kabisa ya kuoa...but ikitokea nimeoa mke wangu akaniambia kauli Kama ulivoambiwa..." Mama yako ni mke mwenza wangu" sijui sijui kitakachotokea.............
 
Pole kwa changamoto na hongera kwa kuliweka mezani maana penye wengi hapaharibiki neno. Maelezo uliyoyatoa hayajitoshelezi hivyo itakuwa vigumu kupata ushauri uliojitosheleza. Itakuwa vigumu kukupatia ushauri mzuri kwani inaonekana kuna baadhi ya maelezo hujayaweka wazi. Kila atakayekupa ushauri atakupa ushauri kwa kutegemea taarifa pungufu ulizotoa. Yawezekana una sababu za msingi za kutoweka bayana taarifa zote za chanzo cha tatizo lako.

Haingii akilini mwanamke uliyeoana naye kwa mapenzi na hadi mkapata watoto leo aende kazini kwako kudai mshahara!
Haingii akilini wazazi wanaompenda binti yao ghafla wamshawishi aachane na wewe hadi kufikia kukupeleka mahakamani!
Haingii akilini tena from nowhere mkeo atamke kwamba 'Mama Mkwe wangu ni kama mke mwenza kwangu'

Kauli ya kwamba 'Mama Mkwe ni Kama Mke Mwenza' inaashiria kwamba umeshindwa kuweka usawa kati ya mama yako na mkeo, kila mmoja wao ana nafasi muhimu kwako - mama ana nafasi kwako kama mzazi na mlezi na pia mkeo ana nafasi yake kama mweza wako wa maisha.

Kwa kuwa wewe uko katikati ya sakata hili ambalo upande mmoja ni mkeo, wakwe zako na mama yako wewe ndiwe pekee wa kuliweka sawa jambo hili. Tambua kuna gharama kwa kila maamuzi tuyafanyayo hivyo tafakari kitu ni muhimu kwako na uko tayari kulipa gharama kiasi gani. Chochote unachoamua hakikisha unaweza maslahi ya watoto mbele kwanza kuliko chochote. Ubishi na ushindani kati yako wewe na mkeo au wakwe zako hautakusaidia - angalia maslahi ya watoto yameangukia wapi. Kwa maslahi ya watoto kama inawezekana jaribu kumshawishi mkeo mjaribu kuishi kama zamani. Ukifanikiwa kuishi na mkeo (hata kama amekukera kiasi gani) kuna faida nyingi kwako/kwenu kuliko hasara utakazopata ukiamua mtengane. Achana na epuka kabisa masuala ya kumpeleka mkweo au mkeo mahakamani - EPUKA KWA NGUVU ZOTE.

Kuna mengi lakini muda hautoshi - kama unahitahiji ushauri zaidi njoo pembeni
 
Asante saaana ndugu yangu nimekuelewa saaana,,mm sina nia ya kupelekana mahakaman kwani najua matokeo yake,,baba mkwe ndie ananitishia kunipeleka mahakaman,sijaona kosa la kupelekwa mahakaman lakin lengo n kwamba kama sitak kupelekwa mahakaman nikubali kufata kila atakacho yey na wazaz wake
Kuhusu suala la kwenda kazin kwangu cjui nieleze nin! Hata kazin kwangu walipomtaka aende kwanza ustaw wa jamii hakufanya hivo! Kama kungekuwa na jambo la msingi la kumpelekea kufanya hivo kwa nn hakufanya hivo!? Natimiza majukumu yangu vilivo lakin hapend kuona nasaidia ndugu hata mzaz wangu ! Cjui nikueleze unielewe!
 
Hao watoto ni wako kweli usikute umepigwa changa la macho ndo maana wanakuletea ujinga, kapime DNA usiwe mtumwa unafanya makosa sana kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe, wakati mwingine unapaswa kuwa aggressive kuwa dominant siyo muda wote hekima sijui busara sijui huruma
 
Mama zetu pia sio wakamilifu ila nahisi ukipata mke utanielewa
Kwel kaka.tusipende kuingiza ishu za wazaz kwenye ndoa zetu.Tu deal na wake zetu sisi kama sisi.wazaz sio wakamilifu wakat mwingine.

Huwa nakumbuka kauli ya mzee wangu alinambia siku naoa.
"Mwanangu ndoa ni yenu.Nyie ndio wachezaji sie wengine (hata wao wazazi) ni mashabki tu,msipende kusikiliza kila tunachoongea.Mkikutana na mambo magum mnayoshindwa kusuluhishana karibun milango iko wazi tutawashauri kama mtataka tufanye hivyo.Ila sio lazima."

Ushauri wangu kwa kiongoz hapo ni kwamba kama mmeshindwana ww mpigr chini tu.Watoto warud kwenu uwalee huyo mtu mzima mwezako pambana nae kisheria mmalizane salama kila mtu aendelee na maisha.

NI NGUMU SANA KUURUDISHA UPENDO MIONGON MWENU PINDI UKIPOTEA.shika yako mwache apambane na yake
 
Hao watoto ni wako kweli usikute umepigwa changa la macho ndo maana wanakuletea ujinga, kapime DNA usiwe mtumwa unafanya makosa sana kutokuwa na maamuzi yako mwenyewe, wakati mwingine unapaswa kuwa aggressive kuwa dominant siyo muda wote hekima sijui busara sijui huruma
Kabisaa mkuu.Kama kiongoz wa familia you must claim your recognition right .kuna muda mwingine usipokua hivyo lazima hawa viumbe watakusumbua tu
 
Haingii akilini mwanamke uliyeoana naye kwa mapenzi na hadi mkapata watoto leo aende kazini kwako kudai mshahara!
Haingii akilini wazazi wanaompenda binti yao ghafla wamshawishi aachane na wewe hadi kufikia kukupeleka mahakamani!
Haingii akilini tena from nowhere mkeo atamke kwamba 'Mama Mkwe wangu ni kama mke mwenza kwangu'

(UMENENA KWELI KABISA NAONGEZEA HAPO CHINI)

Kwa mara ya kwanza kabisa kusoma comment zote:

Wengine wamekuuliza umeoa kabila gani Chagga (mama) Muha(baba)= Binti ni wa Kiha au Muha- havina uhusiano wowote na ndoa yako.

1. Wakati yeye anataka kujifungua alitaka kwenda kujifungulia kwao (hilo ulilikataa) mara nyingi mtoto wa kwanza huwa mama hajui cha kufanya na huwa anajisikia huru kuwa karibu na mama yake mzazi na hapo anaweza kudeka na kufanya ambayo wewe wakati haupo mama yake mzazi kwa mapenzi ya mwana atafanya. . Huenda alipoenda kujifunguliwa kwa wazazi wako hakuweza kufanya yote na huenda wakati anafanya yote hayo mama yako bila kujua yule kiumri na pia na ugeni wa kuzaa akawa anampa maneno ya karaha ( mama wa kinyakyusa hapo anajionea shida kwanini anadeka) Hapo ndipo jina la kusingana kama mtu na mke mweza likazaliwa sio kwamba mke mwenza kwa maana ya kulala pamoja no ya kwamba wanavyosingana na kurushiana maneno hayo yote ni ukiwaweka wanawake pamoja (Thou mkeo alikosea alitakiwa kuuvumilia shida iishe arudi kwao)

2. Wewe mwenyewe umeshajiwekea una kipato kuzidi familia ulioa. so unaona wanakutegemea sana mpk kufikia kusema kwamba hela ya matumizi wataitumia ndio sivyo si kweli.... Kutokana na maneno waliyolishwa na binti yao wakati wa mara ya kwanza kujifungua tayarani hata hawawezi kukuheshimu tena na wanaona kabisa huna mapenzi mema na mwanae so inabidi nguvu ya ziada kutumika.

3. Mimi binafsi hainingii akilini ata umehamishiwa kikazi mkoani kwako huna nyumba kwa kigezo unaamua mkeo akakae kwa wazazi wako wewe ukae kwa ndugu zoko (seriuos kweli) kwani nyumba huko Mbeya chumba na sebule kwa mwezi hata laki huenda isifike kinachokufanya usikae na familia yako nini? Eti toka August unadhani haongei na familia ya kwao na kumwambia mama yake kwamba toka mmehamia huko Mbeya wewe unaishi kwa wazazi wake na manyanyaso ya mama yako huku wewe mwenyewe ukishindwa kuishi nyumbani kwenu sababu mama yako ni mkorofi? Kwa kuwa nimesikiliza upande wako imebidi niviae viatu vya mwnamke mwenzangu ana watoto wawili baba hayupo wala useme jioni akija atacheza na wanawe hapana yuko mkoa huo huo anasubiri Week end kuwaona hapana haikubaliki huku ukijinasibu unawapenda wanao sio kweli ungewapenda ungefanya niwalo ukae nao.

4. Takaka mazingira sio mazuri like seriuos mahali amekuzwa mtoto mpk leo hii ukamwona anavutia na kumwoa sio mahali salama kwa wanao sure, wanao ni Lulu ya mgodi gani?

Kaa chini tafuta nyumba kaa na familia yako acha kutafuta huruma kwa migogoro unaianzisha mwenyewe.

HAKUNA UKWELI WOWOTE KUHUSU WAZAZI WA KICHAGGA KUINGILIA FAMILIA YA MWANAE TENA WA KIKE HAKUNA AIBU KM HIYO
 
Pole sana kaka umeoa mwanamke anayekucontrol, sioni mwisho mzuri wa hili jambo.

Nje ya mada, huyu mwanamke ni mchaga?
BILA SHAKA JIBU NI NDIO!!! Ukifuatilia harusi nyingi mjini zinazofungwa hawa wanahusika, ndio sbb ndoa nyingi zinafunjika nyakati hizi. Pole ndugu
 
Aisee ndoa ndoa ndoa. Mnatupa tabuu ambao atujaoa. Anyway kwa nilivyoona mkeo anamatatizo haiwezekani akufananishie mama yakoo mzazi Kama mkee mwenzie.
 
Kitendo cha Baba Mkwe kutaka kumchukua binti yao na kama una mpatia matunzo ina maana moja tu. hujapewa huyo mke au kwa lugha nyingine hujapeleka mahali.

Au huyo Mwanamke kapata bwana anaemsubmua anatafuta kukuza mambo ili umuache aende zake. Wewe timiza majukumu yako. na timiza majukumu yako hayo maneno ya mdomoni yasikupe shida. siku baba mkwe akimchukua mpeleke katika vyombo husika.

hawa wanawake sometime wakipata interest mpya nje wanasumbua sana wana wablackmmail wazazi wao. wazazi wanakuja kimyume chako.

Kuna jamaa mwanamke alimganda waoane ili hali wapo dini tofauti. mwanamke kamshauri jamaa yake wafunge ndoa ya serikali apate uhamisho kwa haraka halafu watafanya mipango ya kufunga ndoa ya kikristo maana mwanamke ni muislam na alikubali kubadili dini. Jamaaa anasema alipohakikishiwa hivyo kakubali ili wafunge ndoa ya serikali aweze kurahisisha uhamisho wa huyo mwanamke. Baada ya kufunga hiyo ndoa ya serikali wakaomba uhamisho lakini uhamisho nao ulihujumiwa maana document zilipotea na yule mwanamke akakataa kutoa copy alizobaki nazo. Jamaa kuona mambo yanavyokwenda kajitoa muhanga amalizane na wazazi wa yule mwanamke aoe tu yaishe maana kanisani walimbana atoe mahari ili ndoa iwe halali kibiblia. At that moment yule mwanmke kawa amepata bwana nje wa dini yake (muislamu) . Huyo mwanaume alipokomaa kupeleka mahari wazazi wa mwanamke wakagoma wakisema binti yao kapata bwana mwingine .Wakaendelea kumuozesha binti yao kwa dini yao na mahari wakapewa.Jamaa akabaki hajui cha kufanya. Kanisani walimwambia kama wazazi wakipokea mahali wao watabariki ndoa. Lakini mwisho wa siku wazazi walimuozesha binti yao kwingine kwa dini yao na taratibu zote za mahari zikafanyika. Maana yake ni kwamba hata kama akiamua kuvunja hiyo ndoa iliyofungwa kwa ridhaa na wazazi, bado wazazi hawatamtambua wangeendelea kumtambua yule alietoa mahari na yeye angeonekana kama jambazi na binti anakufa na misimamo ya wazazi wake kwa mujibu wa dini yao.

Siku zote ukiruka hatua, ndoa itakusumbua sana. ukitaka mwanamke akutii kweli kweli muoe from skratch yaani usilale nae kabla ya kumuoa utafaidi ndoa yako. itakuwa na utii na wewe mwenyewe utakuwa na mamlaka. Toa mahari na pia oa mbele ya mashahidi wengi hakuna mzazi atathubutu kutamka kuja kumchukua binti yake
 
Suala la mchepuko n kweli nnao lakin hakufanya nishindwe kutimiza majukumu yangu,pia mm kuwa na mchepuko kulichangizwa na yy (sijitetei) akawa hanifulii nguo ,hanipikii kabisa unadhan ningefanyaje?

Sasa hapo ndo ulipokosea kaka mkubwa, kuhalalisha kuchepuka . Hiyo ndo sumu kubwa sana ya ndoa yako ukiacha matatizo ya mkeo na wazazi wake.
 
Hapana mm mnyakyusa yy muha mchanganyiko na mchaga!! Tulikutana dsm tu

Tukiwaambia muoe dada zenu mnakataa mnajifanya mnawapenda wajanga . Haya pambana na hali yako sasa . Abhajaanga bhakaja bhakikulu, ukeete lelo, linga gwalieghile ilumbugho haya yote yasingekupata
 
Kaka kutokana na migogoro mke wangu aliwahi fika kazin kwangu na kueleza uongo ili awe anapewa nusu mshahara, baada ya kupangua hilo na ofisi kuthibitisha kuwa sio kweli! Lakin pia nimekuwa nikitishiwa nae kwa atanikomoa hali ambayo imepwlekea nikae nae mbali lakin akiwa nyumban kwetu na huduma zote anapata lakin ammekuwa mtu wa kuendeleza ugomvi huku akilazimisha kukaa pamoja ambapo hapo cjaua anajiandaa kunikomoa kwa njia gan.Baada ya hapo nilifatilia ili nijue kaanzaje kufika kazin ndipo nilithibitisha kuwa ni maagizo ya wazaz wake ambapo wazaz wake niliingia mgogoro nao baada ya kukataa kuwanunulia viti yaani sofa kwan hawakutimiza makubaliano

Mkuu inaonekana umeanzia mwishoni hili tatizo, unaweza kuelezea toka mwanzo maisha yalikuwaje , kwanini ghalfla mkeo aje ofisini kwako? Nini kilisababisha? tulia eleza vizuri mkuu tukupe ushauri wa kisheria.
 
Idiot una justify mchepuko kwa crap za mke hafui hapiki...kwani mke ni housegirl?
Kupika na kufua ni part and parcel ya upendo. Kama humtreat right atapata wapi hamu ya kukuhudumia?!

Hapa ndipo ilipo shida kubwa ya ndoa yake japokua yeye haoni, anafikiri kuchepuka ni dawa ya kumpunguzia maumivu kumbe ndo anaharibu kabisa. Kuchepuka is a grave mistake inayotafuna ndoa yako.
 
Back
Top Bottom