Msaada wa kisheria tafadhali

mimimnyenyekevu

JF-Expert Member
Apr 19, 2023
697
940
Wasalaam ndugu zangu.
Niende Moja kwa mojakwenye mada

Ikiwa wazazi wameachana na watoto wakawa wanaishi na mama kwa kuwa baba ameoa mke mwingine,je ni sahihi mama wa watoto kukatazwa kujua watoto wake wanapokwenda wakati wa likizo? ( Kwa baba Yao anayeishi na mama wa kambo)

Na je endapo watoto watapata tatizo huko kwa baba Yao je,mama huyu atapataje taarifa hata za kwenda wakati hapajui?

Wanasheria naomba mnisaidie hili

Asante .
 
Kama watoto wanakaa na Baba yao hakuna shida, sijajua waliachana kwa namna gani huenda mwanamke ndo mwenye matatizo ndio maana Baba mtoto hataki kabsa watoto wake waige tabia za ajabu.

Muache adange huyo mwanamke 😂😂 hakuna kuona mtoto hapa. Nyie wanawake mkikaa na watoto huwa mnajikuta keki leo yamewakuta mzee kafunga tinted😁 ngoma droo.
 
Ni hivi,watoto Huwa wanaishi na mama,maana wapo chini ya miaka 8,na baba Huwa anafahamu watoto wake wanapoishi na mama Yao.

Swali ni je,huyu mama haruhusiwi kufahamu kufahamu watoto wake wanapokaa wakati wa likizo?(kwa baba Yao)
 
Kama watoto wanakaa na Baba yao hakuna shida, sijajua waliachana kwa namna gani huenda mwanamke ndo mwenye matatizo ndio maana Baba mtoto hataki kabsa watoto wake waige tabia za ajabu.

Muache adange huyo mwanamke hakuna kuona mtoto hapa. Nyie wanawake mkikaa na watoto huwa mnajikuta keki leo yamewakuta mzee kafunga tinted ngoma droo.
,Asante mkuu kwa mchango wako
 
Ni hivi,watoto Huwa wanaishi na mama,maana wapo chini ya miaka 8,na baba Huwa anafahamu watoto wake wanapoishi na mama Yao.

Swali ni je,huyu mama haruhusiwi kufahamu kufahamu watoto wake wanapokaa wakati wa likizo?(kwa baba Yao)
Oyaaa unatuchanganya naomba utuache. Mara wanakaa wa mama mara wanakaa kwa Baba. Shiit🙄🏃 which is which
 
Oyaaa unatuchanganya naomba utuache. Mara wanakaa wa mama mara wanakaa kwa Baba. Shiit which is which
Hujaeelewa wapi mkuu,watoto wanaishi na mama,ila ikifika likizo yaani wakifunga shule wanaena kwa baba Yao,Sasa swali ni je huyu mama hatakiwi kufahamu watoto wanapoishi wakati wa likizo?
 
Ni hivi,watoto Huwa wanaishi na mama,maana wapo chini ya miaka 8,na baba Huwa anafahamu watoto wake wanapoishi na mama Yao.

Swali ni je,huyu mama haruhusiwi kufahamu kufahamu watoto wake wanapokaa wakati wa likizo?(kwa baba Yao)
Kama hapafahamu je watoto walifikaje? Kama ana uhakika wapo huko basi wapo kwenye mikono salama kwa wakati huo ,haina ulazima wa kupajua kikubwa ana uhakika wapo kwa baba yao na watarudi.
 
Ni hivi,watoto Huwa wanaishi na mama,maana wapo chini ya miaka 8,na baba Huwa anafahamu watoto wake wanapoishi na mama Yao.

Swali ni je,huyu mama haruhusiwi kufahamu kufahamu watoto wake wanapokaa wakati wa likizo?(kwa baba Yao)
Mama ana haki kisheria kuwaona watoto na kujua mazingira wanayoishi bila kujali waliachama kwa namna ipi.
 
Unachotakiwa kujua ni kuwa watoto wako na baba yao, na wako kwenye mikono salama.

Kwa vitimbi na kashfa ulivyomfanyia huyo aliyekuwa mume wako, hata mimi nisingependa upajue, watoto walipo.
 
Wasalaam ndugu zangu.
Niende Moja kwa mojakwenye mada

Ikiwa wazazi wameachana na watoto wakawa wanaishi na mama kwa kuwa baba ameoa mke mwingine,je ni sahihi mama wa watoto kukatazwa kujua watoto wake wanapokwenda wakati wa likizo? ( Kwa baba Yao anayeishi na mama wa kambo)

Na je endapo watoto watapata tatizo huko kwa baba Yao je,mama huyu atapataje taarifa hata za kwenda wakati hapajui?

Wanasheria naomba mnisaidie hili

Asante .
Kuna Viumbe mnapenda Kesi/sheria! Yaani hizi siku 15 za Likizo ya mwisho wa mwaka baba kuchukua watoto wake kwenda Vacation au Likizo binafsi nazo unamtafuta Mwanasheria kisa hujaambiwa wanaelekea wapi? Kwani angekwambia anaenda Kilolo Iringa lkn akaenda Vunjo Kilimanjaro ungefaidi nini sasa.
Wanawake wa aina hii ndio wanafanya Vijana waje na kaulimbiu ya KATAA NDOA.
 
Story yako ipo nusu.

Yeye baba anasemaje kuhusu wewe kufahamu wanapoishi watoto?

Kama anakataa, sababu gani anatoa?

Je, watoto wanataka kumuona baba au baba ndiye anawahitaji watoto?

Makubaliano yenu yalikuwaje wakati wa kuachana kuhusu watoto?

Chanzo cha kuachana ni kipi haswa?

Ni nani anawahudumia watoto?

Majibu ya maswali hayo yataeleza msingi wa changamoto yako.
 
Ni hivi,watoto Huwa wanaishi na mama,maana wapo chini ya miaka 8,na baba Huwa anafahamu watoto wake wanapoishi na mama Yao.

Swali ni je,huyu mama haruhusiwi kufahamu kufahamu watoto wake wanapokaa wakati wa likizo?(kwa baba Yao)

Anaruhusiwa.
Sema Wamama wengii huwa wanaleta shida kwenye ndoa za watu kwa kisingizio cha Mtoto
 
Asante mkuu kwa maoni yako,Sasa huyu mama anawawekeaje watoto madawa wakati ndo anaishi nao? Mbona mama yeye hajaona tabu kumuonyesha mwenzie sehemu wanapoishi na watoto,mbona baba anapafahamu tu vizuri,Sasa kwa nn yy amkatalie mwenzake? Hujaona Iko shida hapo
Mama amemkubalia jamaa kwa sababu jamaa ni muungwana anafanya kile kilichompeleka eneo husika (kuchukua watoto) yan hana ajenda nyingine za kuharibu au kuvuruga.

Mwanaume anamkatalia mtalaka wake kwa sababu ya tabia zake huenda ni mgomvi , mtu anachukua watoto kwa ajili likizo mara siku mbili tu dada huyu hapa anakuja na varangati anataka kuchukua watoto anajaza mtaa kwa fujo na kumtukana mke mwenzie.

Yule ni baba wa watoto mradi hamna shida yeyote kwa watoto fuatilia mwenyewe kujua anapoishi.
Huenda wewe ni mshari au una michezo ya kiswahili Dear Ex anaogopa usijue details zake mpya au muulize kwanini hataki !!
 
Back
Top Bottom