Ndoa inanimaliza!

Pole mkuu!
Nimecheka tu uliposema 'anajikwaza' ananuna tena,hivi mtu anajikwazaje?
 
Kama ye bubu we kuwa kiziwi.......
Mkuu ujue tatizo hilo ni serious acha utani, hii kitu ikitokeaga kwangu aisee huwa napata mtihani mzito sana, tena ukute nyumbani kuna mgeni wa muhimu kama vile mama hivi kawatembelea, aisee... nyumbani hapakaliki, ofisini utendaji wako unazorota... unaweza ukazianza bia asubuhi usipokuwa makini!
 
mwanamke yeyote akichelewa kupata mtoto huwa ananuna hivyohivyo, na anavyozidi kuwa na stress ndivyo anavyovuruga mwili wake na anatakavyozidi kuchelewa kupata mtoto. unatakiwa umfariji, kuna siku akipata mtoto atakuja kuwa mtu wa furaha sana. subiri tu.

sidhani kama umeelewa nilichoandika nimesema matatizo ya kununa hayatokei sababu hana mtoto. Tuwe na imani na maneno ya watu ndiyo maana tunashindwa kutoa ushauri mzuri katika jamii kwa kujifanya tunamacho ya chuma, kama mtu anayehitaji ushauri kakwambia hilo siyo tatizo nawewe umekomaa na kusema hilo nitatizo utamshauri nini?
 
Huyo mkeo dawa yake sio kumuacha bali ushauri

Kwanza jitahidi kuwa rafiki yake na kama suala hilo la kutokupata mtoto unaliongelea sana punguza na ikiwezekana acha kabisa kuliongelea na jitahidi kuwa karibu yake kisha nendeni kwenye kituo cha afya mkapime ili mjue tatizo liko wapi na mkijua mlifanyie kazi

Kama mkikuta hakuna mwenye tatizo jitahidi sana kutokulizungumzia hilo katika hali hasi,mpeleke kwa wataalam wa ushauri na atakuwa bomba tu

Malezi yametuharibu sana kuhusiana na suala zima la kuzaa na kupata mtoto
Mtu akiwa hana uwezo huo huonekana kama amepungua ubinadamu wake kwa 70% hivi
Ujinga huu sijui utaisha lini

Katika mambo ambayo hayaniumizi akili ni hili!

hapo mstari wa mwisho
anaheri huyo mkeo
 
Ushauri umefanyika sana na hata kupima tumepima wote zaidi ya mara 3 daktari alisema hatuna shida. sina muda na wala sijawahi kulizungumzia hili suala katika negative side zaidi ya kumtia moyo tu kuwa ipo siku mungu atattenda. nimejaribu sana kuwa rafiki yake lakini wapi

mwambie kuwa kunununa kwake kwa hovyo hovyo ndiko kunasababusha negative forces mwilini mwake na hivyo reproduction system imeathirika...na akiendelea itakulazimu upate asiyenuna....life is too short to live with jitu lisilo na furaha ndani ya nyumba.
 
Pole sana mtumishi wa mungu
ingawa umesema kinachomnunisha si mtoto kwa ulimwengu wa roho napenda kumuunga mmoja wa hoja hapo juu mtooto ndio tatizo..na kinachoonekana wewe ni src ya kuzungumzia mtoto ..ingawa si dk ali mtoto ni baraka za bwana ....ndoa ni muhimu na mtoto ni majaliwa ushauri basi

najua miaka minne ni mingi na inawezekana anachonuna anhisi unatafuta mtoto nje ..jitahdisana uwe nae karibu ..kuna waliokataa tamaa na watotot na mungu ni shahidi yangu na mi ni mmoja wao ingawa ilichukua mwaka mmoja na nusu ila kama bnadamu mungu mmoja mwamini mungu .....

1..kama mmedhamiria mweleze ukweli halisi mkeo kwamba wakati wa kujaribu kwenda kwa ma dk..ni frha yangu kuona dk3s wa jf wakitoa sehemu mbli mbali za kwenda mnachofanya mnapima wote wawili wala usiogope...mi ninajua sehemu moja pale mbuyuni ukielekea posta ...kulia kuna hosp ya wazazi..ni baba mzuri ssana ni garama kidogo lakini mungu anakwenda kuwafungua..na moja ya mahitaji yake ni wote wawili kwenda so mnaitajika ukubali wenu wawili....

2.kununa kwenye ndoa chaa kawaida ..wala usiiogope ukuzaliwa nae kusema mmetunza pamoja ..kama uamini angalia ndugu zako wa damu mnaowashiaana moto mpaka sasa sembuse huyo

3..shekeli
hili ni kitengo kingine muhimu kinachosumbua ndoa ..mnaitajika uwazi wa shekeli zenu ..aisewezkani
mmoja ananunua gari kwa mkopo siku ya kulipa unashangaa majembe wanakuja wakikuta na la mwenzio wanachukua unaishia kulipa deni la mwenzio usilolijua..hii si vyema
kuwa kama mimi baba na mama tunaweka mezani
tunapanga maihitaji ya mwezi mzima ,,inabaki kadhaa tunatoa kiasi hiki ni kwa ajili ya benki zetu za madafu...mungu akikupa watoto ni muhimu pia mnawaweke benki hata laki moja ama mbili kwa mwezi kadri utakavyoongozwa

4..kununa kuna mambo mengi
unajua unapomwibia mungu si lazima akufukuzishe kazi no anaweza kutibua nyumbani mpaka ukawa na akili timamu..sasa basi pengine zaka hutoi kabisa sadaka ni majawaliwa sasa kuna sehemu za kukurudisha kwenye mistari kama hizi so kuwa makini na kutomwibia mungu

ngoja nikale kwanza nitakuja na muendelezo wa kwa nini kuna kunununa kwenye ndoa

asante
hapo no 4 ndo inaitwa kulipa gharama
bahati mbaya san wengi hawajui hili
 
Akinuna na vingine vinanuna au unapewa?

wewe umenichekesha sana, ivi sura ya vile vitu tnaifahamu, sasa sivipatii picha vikiwa vimenuna.

by the way jaribu kumshirikisha mchungaji labda atakuwa na zuli la kuwajengea ndoa yenu
 
sidhani kama umeelewa nilichoandika nimesema matatizo ya kununa hayatokei sababu hana mtoto. Tuwe na imani na maneno ya watu ndiyo maana tunashindwa kutoa ushauri mzuri katika jamii kwa kujifanya tunamacho ya chuma, kama mtu anayehitaji ushauri kakwambia hilo siyo tatizo nawewe umekomaa na kusema hilo nitatizo utamshauri nini?
ukikua utakuja kuelewa. kununa lazima kuna sababu. mtu ukiwa na kidonda moyoni (mfano cha kutopata mtoto) ukitoneshwa hata na kijiko tu unaweza kununa utafikiri umepigwa ngumi. hata hivyo nafuta kauli kwamba ananuna kwasababu hana mtoto. ninachosema sasa, yeye atafute chanzo mkewe kwanini ananuna. ila kwa uzoefu, akija kupata mtoto yeye atakwambia ni nini kilikuwa kinamsumbua. thanks.
 
Huyo mkeo dawa yake sio kumuacha bali ushauri

Kwanza jitahidi kuwa rafiki yake na kama suala hilo la kutokupata mtoto unaliongelea sana punguza na ikiwezekana acha kabisa kuliongelea na jitahidi kuwa karibu yake kisha nendeni kwenye kituo cha afya mkapime ili mjue tatizo liko wapi na mkijua mlifanyie kazi

Kama mkikuta hakuna mwenye tatizo jitahidi sana kutokulizungumzia hilo katika hali hasi,mpeleke kwa wataalam wa ushauri na atakuwa bomba tu

Malezi yametuharibu sana kuhusiana na suala zima la kuzaa na kupata mtoto
Mtu akiwa hana uwezo huo huonekana kama amepungua ubinadamu wake kwa 70% hivi
Ujinga huu sijui utaisha lin
i

Katika mambo ambayo hayaniumizi akili ni hili!

Very well said mkuu Eiyer
 
Last edited by a moderator:
Mkuu alianza kununa baada ya kuingia kwenye ndoa au hata mkiwa katika kipindi cha urafiki na upenzi?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Ushauri umefanyika sana na hata kupima tumepima wote zaidi ya mara 3 daktari alisema hatuna shida. sina muda na wala sijawahi kulizungumzia hili suala katika negative side zaidi ya kumtia moyo tu kuwa ipo siku mungu atattenda. nimejaribu sana kuwa rafiki yake lakini wapi

Anahitaji maombi alafu hata kupata mimba mwili nao unatakiwa usiwe na stress sasa iyo kununanuna inaweeza kuwa sababu ya yeye kutokupata mimba mwaribu kwa kumwabia hiyo ndo sababu ya yeye kutokushika mimba...... ikishindikana aisee me navyochukia hiyo tabia angekuwa ananiona mda wa kulala tu aise
 
ukikua utakuja kuelewa. kununa lazima kuna sababu. mtu ukiwa na kidonda moyoni (mfano cha kutopata mtoto) ukitoneshwa hata na kijiko tu unaweza kununa utafikiri umepigwa ngumi. hata hivyo nafuta kauli kwamba ananuna kwasababu hana mtoto. ninachosema sasa, yeye atafute chanzo mkewe kwanini ananuna. ila kwa uzoefu, akija kupata mtoto yeye atakwambia ni nini kilikuwa kinamsumbua. thanks.

Na wakati tu nimemuoa ana wiki 2 alikuwa ananunia mtoto?
 
Anahitaji maombi alafu hata kupata mimba mwili nao unatakiwa usiwe na stress sasa iyo kununanuna inaweeza kuwa sababu ya yeye kutokupata mimba mwaribu kwa kumwabia hiyo ndo sababu ya yeye kutokushika mimba...... ikishindikana aisee me navyochukia hiyo tabia angekuwa ananiona mda wa kulala tu aise

Kumbe na wananwake wapo wanasema kweli hongera
 
ni kama vita vile hakuna hata hamu ya hayo mengine

Kaka nisamehe kidogo. Mimi sina dawa ya kuchua bali ni ya kunywa, hivyo ushauri wangu waweza ukawa mchungu kidogo. Naanza kwa kunukuu hayo maneno yako mwenyewe. Umekiri kuwa hakuna hata hamu ya hayo mengine!! Sijui weye ni mtoto mdogo au ni mtu mzima.
Mtoto hupatikana kwenye hayo mambo mengine!!! Bila hayo, hakuna mtoto labda wa kimaabara. Weye ndiyo kikwazo kaka. Huenda hata jamaa za kwako ndiyo wanamsimanga mtoto wa watu. Acha kusikiliza vya pembeni. Kama weye ni mzima, mbegu zako saafi za afya, na yeye kadhalika, iweje usimpate huyo mtoto?
Amesha athirika kisaikolojia, sasa unatakiwa weye mwenyewe umwandae vizuuri kwa kumtoa out kidogo, mnunulie kanguo kazuuri sana ka ndani (kufuli) sio kwamba hana, lakini hili unamwambia ni very special kwake. Mpe ruhusa kuufungua moyo wake kwako. Haya hayaji kwa siku moja tu.
Taratibu, umwambie unampenda yeye kuliko chochote. Si mtoto wala mjukuu anaye zidi pendo lako kwake. Mthibitishie kuwa, hata kama hamtapata mtoto, yeye ndiye bora kwako. Akikuamini, utashangaa, ataanza kutaapika na kula udongo na embe changa sasa hivi.
Mwandae mkeo
 
ni kama vita vile hakuna hata hamu ya hayo mengine

Usikute ana spiritual husband ,muombe ili limtoke na usikute ndio linamyima mtoto.kama unaamini anzeni kuomba na kufunga kwani ukicheza litasambaratisha ndoa ,kukutia umaskini na mambo mengine mengi.
 
Back
Top Bottom