Ndoa inaelekea kunishinda

Asante mwaya
 
Huyo uhuni wake anaujua

 

 
Kwa upande wangu hakuna tatizo Kama ni mapenzi nampa huyu tu ni tabia yake inaonekana Kama siyo Basi shetani labda yupo kazini anamtumia kwa akili tu za kawaida hata Kama ningekuwa Mimi ndo mwenye tatizo angetulia Basi na mchepuko mmoja angeeleweka kwahiyo unataka kunambia mchepuko wa kwanza kaukuta una kasoro Kama zangu ndomana akatafuta wapili huyo naye ana kasoro Kama zetu ndomana akatafuta tena watatu huoni kwa style hii atatoka sasa na dunia nzima yani moja kwa moja hata ukimuelezea mtoto asiye na akili hapa mwenye shida ataonekana tu ni mwanaume
 
Pole sana, jitahidi kuweka pembeni yaliyotokea japo ni ngumu lakini inabidi ufanye hivyo, jua kuwa Mume wako anakupenda ndiyo maana katika kundi la Wanawake wengi alikuchagua wewe, Wanaume kuchepuka kwao ni kitu cha kawaida. Mungu akusaidie.
 
Ohooo nimeona. Yan hatari alishaiona tangu mwanzo hapa ndio unaambiwa 'umeyataka mwenyewe iliyobaki shauri yako'. Alishapewa signs zote ila akang'ang'ana na ndoa. Kumbe ameolewa na muhuni na anamjua hiyo tabia yake. Itabid apambane na huba lake tu
 
Mpaka na Mimi nashanga naona ni kitu Cha ajabu mpaka nawaza isije ikawa Kuna mtu anamchezea akili ili Mimi niteseke tu
 
Yaan michepuko mitatu tuu ww unataka kuvunja Ndoa..... Kweli wewe siyo Mwanamke mvumilivu.

Mke wang mtarajiwa kokote ulipo naomba uwe na Moyo wa Uvumilivu na Kusamehee maana siku ukinikamata jua unakamata Idadi ya Namba hawatokuwa chini ya 7
 
Asante mwaya
 
Ohooo nimeona. Yan hatari alishaiona tangu mwanzo hapa ndio unaambiwa 'umeyataka mwenyewe iliyobaki shauri yako'. Alishapewa signs zote ila akang'ang'ana na ndoa. Kumbe ameolewa na muhuni na anamjua hiyo tabia yake. Itabid apambane na huba lake tu
Tatizo binadamu huwa tunakuwa wabinafsi. Unaona mwenzako anapenda k kutwa mara tatu! Wewe unambania ati una mimba Qu sijui huwezi sex kwa vile una maumivu D2, yeye abake? Mengine ya kujifanya huoni ili siku isogee
 
Hivi unafiki mtaacha lini baadhi ya Wanaume wa Jf laiti kama hii mada ingeletwa na Mme ungetoa ushauri hivi😬
 
Na wewe wakati fulani upunguze kumfuatilia huyo mume wako! Kitendo cha kumfuatilia sana, kinachangia kumpunguzia uwezo wake wa kujiamini (ingawa wanaume wengine hatuwezi kuishi bila ya kucheza mechi za ugenini) na hivyo kujikuta anapuyanga tu huko nje.

Jitahidi kuifanya nyumba yako kuwa kituo cha furaha, amani na upendo. Na pasiwe mahali panapo waka moto muda wote. Achana kabisa na gubu kama unalo, wivu uliopitiliza, kununa nuna hovyo, kumhukumu mtu kama huna ushahidi ulio jitosheleza, acha mara moja tabia mbaya ya kushika shika simu yake na kusoma sms ambazo hazikuhusu, nk. Maana wanaume tulio wengi huwa hatupendi hivi vitu.

Pia kwa sasa huna sababu ya kuishi maisha ya mateso. Labda kama hatimizi majukumu yake kama mume! mfano kununua chakula, nk. Unatakiwa ujali maisha yako na ya huyo kiumbe aliyeko tumboni! Baada ya kujifungua salama, utakuwa na maamuzi sahihi ya kufanya.

NB: Halafu wanawake muwe mnatuelewa wakati mwingine. Tumeumbiwa tamaa na kutotosheka! 😋 Ukiona mwanaume ana mke mmoja tu, basi ujue huyo anavumilia! Na ameamua tu kumheshimu mke wake. Ila kutotosheka na tamaa ya mwili, viko pale pale. Na hao ndiyo wanaume.
Na hii ni siri ya kambi, ila nimeona niwang'ate tu sikio kwa lengo la kuwapunguzia maumivu yanayoweza kuzuilika.
 
Hivi unafiki mtaacha lini baadhi ya Wanaume wa Jf laiti kama hii mada ingeletwa na Mme ungetoa ushauri hivi😬
Hahahhahah kwahio mie mnafiki jamani😅 natoa ushauri kulingana na situation! Mwanaume ndio kazingua. Mke angezingua ningemshauri mwanaume afukuze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…