Ndoa inaelekea kunishinda

Ndoa inaelekea kunishinda

Pole sana miss chuga

Kwanza kabisa acha hizo mambo za kushusha na kupandisha presha yako. Jitunze afya yako kwanza ukifa leo mwenzio hata haweki matanga maana waombolezaji ndio hao ulosoma msg zao.

Kabla ya kuuliza umsamehe au ufanye nini. Kwakuwa mwanaume ndio anayeamuaga amuoe nani, hebu rudi nyuma ujiulize ujiulize katika kweli na haki bila kuuongopea moyo wako KWANINI LIAMUA KUKUCHAGUA WEWE KATI YA HAO AKAKUOA? Je, ilikua ni sababu ya upendo au kuna lingine?
Je, wakati anaamua kukuoa alikua na michepuko mingapi? Au hukiwahi kuligundua hilo?

Pole mwaya tunza afya yako na huyo mtoto uliyembeba, ondoa hasira maana huwezi badili chochote kwa kukasirika.

Jifunze kumwomba Mungu kwa imani yako maana kama yeye uliyeingia nae mkataba anakucheat hakuna anayeweza kumshurtisha aache na akupende na kukuheshimu wewe tuu na asiwe na mwingine. Kama amedhamiria kundeleza kabumbu atashauriwa, watamsema atakubali atakubali kuacha halafu atabadilisha mbwinu... sim ya michepuko atakua anaiacha nje ya nyumba kuwaridhisha

Michepuko mitatu ndoa ya mwaka mmoja bwana huyu katisha
Asante mwaya
 
Either uhuni ni hulka yake au kuna nguvu za giza. Shetani hapendagi kuona watu wana furaha. Wewe cha kwanza kama una wifi yako mnaelewana mwambie. Mimi naamini dada wa mumeo hawez yaanika mapungufu ya mdogo ake. Akiendelea na hiyo tabia basi hakufai.

Sio kila ndoa ni lazima mzeeke pamoja. Kuliko kua na mawazo ya kuua bora urudi kwenu aibu utaipata kwa muda mchache lakini utakua na amani ya moyo kwa muda mrefu
Huyo uhuni wake anaujua

 
Case closed hapa.

Mwana alikuwa anakosa sex kwa muda kutokana na sababu hii. Mshkaji anakupenda sana. Ana huruma na wewe. Alipoona unaumia akaona asikutese bure.

Dada zetu kuna mambo mengi sana hamyaelewi.

Screenshot_20220131-104122_Chrome.jpg
 
Fuatilia vizuri ndugu yangu. Pengine huyo mchepuko aliepigiwa simu anacheza game tu ili amuharibie mwana kwako. Pengine kawapa hao wengine namba ya mwana ili wamtumie hizo msg kichaa wewe uzishike kiwake.

Mwana upo nae 5 years kabla hajaoa na alikuwa na uhuru wa kuchepuka lakini hakuwa hivyo, Leo miezi sita eti umshike na michepuko mitatu ghafla ghafla?? Mwana sio boya kiasi hicho.

Jengine, enyi wanawake, wavumilieni tu wanaume. Hali ni tete sana!

Kubalini ukewenza acheni kushupaza shingo.

Ukewenza ndio asili ya mwanadam.

Tutaelewana tu kidogo kidogo.

IMG_5681.jpg
 
Tujue kwanza sababu za yeye kukuchiti tusijekua tunamlaumu Bure kumbe sababu ni wewe labda huumpi haki yake au unakiburi au jeuri au una dharau au humlidhishi maana sababu ziko nyingi sana.
Ila naona next time usiweke makosa yake tu pia elezea na yako ili tujue sababu Iko wapi ndio tuanze kutoa ushauri .
Huwezi kutibu tatizo bila kujua chanzo
Kwa upande wangu hakuna tatizo Kama ni mapenzi nampa huyu tu ni tabia yake inaonekana Kama siyo Basi shetani labda yupo kazini anamtumia kwa akili tu za kawaida hata Kama ningekuwa Mimi ndo mwenye tatizo angetulia Basi na mchepuko mmoja angeeleweka kwahiyo unataka kunambia mchepuko wa kwanza kaukuta una kasoro Kama zangu ndomana akatafuta wapili huyo naye ana kasoro Kama zetu ndomana akatafuta tena watatu huoni kwa style hii atatoka sasa na dunia nzima yani moja kwa moja hata ukimuelezea mtoto asiye na akili hapa mwenye shida ataonekana tu ni mwanaume
 
Pole sana, jitahidi kuweka pembeni yaliyotokea japo ni ngumu lakini inabidi ufanye hivyo, jua kuwa Mume wako anakupenda ndiyo maana katika kundi la Wanawake wengi alikuchagua wewe, Wanaume kuchepuka kwao ni kitu cha kawaida. Mungu akusaidie.
 
Huyo uhuni wake anaujua

Ohooo nimeona. Yan hatari alishaiona tangu mwanzo hapa ndio unaambiwa 'umeyataka mwenyewe iliyobaki shauri yako'. Alishapewa signs zote ila akang'ang'ana na ndoa. Kumbe ameolewa na muhuni na anamjua hiyo tabia yake. Itabid apambane na huba lake tu
 
Fuatilia vizuri ndugu yangu. Pengine huyo mchepuko aliepigiwa simu anacheza game tu ili amuharibie mwana kwako. Pengine kawapa hao wengine namba ya mwana ili wamtumie hizo msg kichaa wewe uzishike kiwake.

Mwana upo nae 5 years kabla hajaoa na alikuwa na uhuru wa kuchepuka lakini hakuwa hivyo, Leo miezi sita eti umshike na michepuko mitatu ghafla ghafla?? Mwana sio boya kiasi hicho.

Jengine, enyi wanawake, wavumilieni tu wanaume. Hali ni tete sana!

Kubalini ukewenza acheni kushupaza shingo.

Ukewenza ndio asili ya mwanadam.

Tutaelewana tu kidogo kidogo.
Mpaka na Mimi nashanga naona ni kitu Cha ajabu mpaka nawaza isije ikawa Kuna mtu anamchezea akili ili Mimi niteseke tu
 
Yaan michepuko mitatu tuu ww unataka kuvunja Ndoa..... Kweli wewe siyo Mwanamke mvumilivu.

Mke wang mtarajiwa kokote ulipo naomba uwe na Moyo wa Uvumilivu na Kusamehee maana siku ukinikamata jua unakamata Idadi ya Namba hawatokuwa chini ya 7
 
Bidada kwanza unatakiwa ujue kuwa huyo mumeo ajaanza kwenye ndoa yenu huo mchezo, huyo ameuanza tangu mko wapenzi mpaka mnafikia uchumba na kumaliza ndoa. Apo ni Mungu tu ndio kakufungulia uone Ili ujue ni jinsi gani utajilinda ww na mwanao dhidi ya magonjwa.

Mwanaume kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja Ilo ni jambo halizuiliki maana wameumbwa na tamaa, ni wachache Sana ambao atakuwa mwaminifu katika mahusiano yake na wapewe tunzo ya uaminifu kwa kweli. Kati ya hao wote ww ndiye uliyepata bahati ya kuolewa na huyo mumeo, ivyo shukuru umeijua tabia yake.

Ukiona nyani wamezeeka bado wapo pamoja ujue wamekwepa mishale, mikuki na nyundo nyingi uko mstuni. Kwa sasa angalia afya yako ww na mtt wako wa tumboni Ili usije ukampoteza na ata usije ukamchukia huyo mtt kiasi cha kutaka kufanya jambo lolote lile ovyo. Wazazi wetu mpk wanazeeka wapo pamoja, ujue mwanamke ndiye ameibeba ndoa, amevumilia sanaa, asa ktk vipindi vya kujifungua anachezea mikojo muda wote, mwanaume Yuko bize nje ya ndoa. Kama unapewa huduma zote, basi akili kumkichwa, unatakiwa ujiongeze apo,( kula na akiba acha). Kila la kheri.
Asante mwaya
 
Ohooo nimeona. Yan hatari alishaiona tangu mwanzo hapa ndio unaambiwa 'umeyataka mwenyewe iliyobaki shauri yako'. Alishapewa signs zote ila akang'ang'ana na ndoa. Kumbe ameolewa na muhuni na anamjua hiyo tabia yake. Itabid apambane na huba lake tu
Tatizo binadamu huwa tunakuwa wabinafsi. Unaona mwenzako anapenda k kutwa mara tatu! Wewe unambania ati una mimba Qu sijui huwezi sex kwa vile una maumivu D2, yeye abake? Mengine ya kujifanya huoni ili siku isogee
 
Kama ni movie ndio kwanza ipo kwenye ....
”Starring”....“Executive Producers”...”Title”... usijaribu kuvunja ambacho mungu amekiunganisha mkuu!

Nachokiona wewe umeolewa ila ni mgeni kwenye michezo ya mapenzi. Nikutoe hofu tu kuwa wanaume 80% huwa wana cheat ila kwa adabu sana! 20% ndio ambao hawana adabu kwenye cheating wao hawana aibu kuonesha kuwa wana cheat na hawa ndio wabaya sana.

Ukivunja ndoa sababu mume ameku cheat jua uendako pia utachitiwa tu na utakuwa dissapoonted mara mbili! Jifunze kuishi na hio hali kuwa mumeo sio muaminifu na maumivu yakizidi na wewe tafta mtu akugongege kwa siri ili akufariji. Hio ndio namna ya kupunguza machungu ila usiache kumuheshimu mumeo hata ukishaanza kuliwa maana ukiteleza hapo tu utapewa talaka kwa aibu na fedhea. Liwa nje ila usianze dharau na kejeli utakamatwa.
Hivi unafiki mtaacha lini baadhi ya Wanaume wa Jf laiti kama hii mada ingeletwa na Mme ungetoa ushauri hivi😬
 
Ushauri wenu jamani mimi nimeolewa nipo kwenye ndoa hatujamaliza hata mwaka Ila kinachoniumiza mme Wangu ananisaliti, nimemkuta anamiliki simu ya Siri pamoja na line alikuwa kaficha kabatini baada ya kugombana naye akakubali kuwa ana mchepuko akampigia akaweka loud nikawa nawasikia akamuomba samahani kwa kumchezea akamwambia Mimi nimeoa, nina mke nmeona siyo vizuri kumsaliti mke wangu dada akalalamika we badae akakubali kumblock kidogo nikapata amani.

Baada ya hapo hiyo simu ya Siri akaweka mezani akatoka zake Ila kilichoniumiza zaidi baada ya lisaa zilikuwa zinaingia text kutoka no. tofauti tofauti 2 baada ya kuchart nao kumbe nao ni michepuko yake tena jumla nimemfuma na wanawake 3 kwa wakati mmoja.

Msamaha kaniomba Ila nashindwa kumsamehe, naumia sana Bora ningemkamata hata na mmoja nisingeumia sana Ila wa 3 ukitegemea ndoa haina hata mwaka nawaza sijui kalogwa, natamani nimshirikishe hata mchungaji wetu Ila napata wakati mgumu naona ni vitu vya aibu hata kushirikisha watu wetu wa karibu. Natamani niondoke Ila kinachonipa wakati mgumu tayari Mimi ni mjamzito yaani nawaza ingekuwa siyo hii mimba ningeachana nae ananifanya Hadi nakata tamaa na mimba niliyonayo kitu ambacho ni dhambi, Naombeni mnishauri nifanyaje nahisi kuchanganyikiwa nakosa maamuzi presha imeshuka naona Kama dunia imeniangukia kweli ndoa ni ngumu sana duh! Mungu anitie tu nguvu.
Na wewe wakati fulani upunguze kumfuatilia huyo mume wako! Kitendo cha kumfuatilia sana, kinachangia kumpunguzia uwezo wake wa kujiamini (ingawa wanaume wengine hatuwezi kuishi bila ya kucheza mechi za ugenini) na hivyo kujikuta anapuyanga tu huko nje.

Jitahidi kuifanya nyumba yako kuwa kituo cha furaha, amani na upendo. Na pasiwe mahali panapo waka moto muda wote. Achana kabisa na gubu kama unalo, wivu uliopitiliza, kununa nuna hovyo, kumhukumu mtu kama huna ushahidi ulio jitosheleza, acha mara moja tabia mbaya ya kushika shika simu yake na kusoma sms ambazo hazikuhusu, nk. Maana wanaume tulio wengi huwa hatupendi hivi vitu.

Pia kwa sasa huna sababu ya kuishi maisha ya mateso. Labda kama hatimizi majukumu yake kama mume! mfano kununua chakula, nk. Unatakiwa ujali maisha yako na ya huyo kiumbe aliyeko tumboni! Baada ya kujifungua salama, utakuwa na maamuzi sahihi ya kufanya.

NB: Halafu wanawake muwe mnatuelewa wakati mwingine. Tumeumbiwa tamaa na kutotosheka! 😋 Ukiona mwanaume ana mke mmoja tu, basi ujue huyo anavumilia! Na ameamua tu kumheshimu mke wake. Ila kutotosheka na tamaa ya mwili, viko pale pale. Na hao ndiyo wanaume.
Na hii ni siri ya kambi, ila nimeona niwang'ate tu sikio kwa lengo la kuwapunguzia maumivu yanayoweza kuzuilika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom