Ndoa inaelekea kunishinda

Wanawake hapo ndo mnapofeli, et unataman umshirikshe mchungaji wenu??? Huna wazaz, ndugu na jamaa?? Kuwa makin na hao wachungaj watakuomba buree!! Nao binadamu
Weee unawajua ndugu wewe si bora hata mchungaji, kuna ndugu niwanaa hajipata kutokea mie mwenyewe siwezi mshirikisha ndugu mambo mengine bora nife nayo
 
acha kufikiria mambo ya kumchomoa mtoto, hilo neno lifute haraka maana shetani naye yuko kazini,,kwani mtoto ana shida gani jaman

omba sana usiwaze mawazo negative juu ya kiumbe asie na hatia

Mungu akushindie
 
Wanaume wote Baba yao mmoja
 
Halafu yeye akisikia kuna mtu kajisevia huko anavyokuja kama mbogo, ndiyo maana wanakufa mapema kwa stess
 
Unaona mwenzio mke kajua michepuko 3 ndoa haina hata mwaka , nayeye akipata kamchepuko kamoja atamlilia nani huyo baradhuri!
 
Pole sana, vumilia ujifungue kwanza ukipona ndiyo utajua mbivu na mbichi, inamaana hapo mkiwa uchumba alikuwa anakuzunhusha tu kwenye magori ili usijue chochote, subili ujifungue kama si tabia yake labda atabadilika lakini kama ndiyo zake mmm hapo kisu utakuwa nacho mkononi
 
Bado una hasira za kitoto Sana, mi siwezi kumpigia mchepuko wa mume nikigundua kuna uchepukaji we komaa na mwanaume

Kwa jinsi maisha yalivyo achepuke kwa kunipumbaza nisijue nikihitaji mkuno naupata fresh arrrghhh jinsi uwanja wa mapenzi ulivyo chafuka huko kitaa dah naweza kumfuma na nikamsamehe vizuri tu, Kwanza naona km mumeo anakupenda au nae Bado ana akili za kitoto kukubali kupigia simu mchepuko na kuweka loudspeaker,
 
Kwanza Pole hayo ni mapito katika ndoa yako pia binafsi nisingependa mambo ya ndoa kuyqweka public maqna huwa sioni faida yake direct lqbda ushauri wangu ...umesema ni mume wako hope unajua mapungufu yake sikushauri sana uchunguze simu zake lakini pia jaribu kumfanyia jambo ambalo analipenda sana then mfanyie mara kwa mara lengo ni kumteka kihisia then baada ya mda labda miezi miwili


Naamini hapo atonal umuhimu wako then unanza kumweleza nijinsi gani hupendezwi na tabia yake
Na using penda kuona hiyo tabia inajirudia tena na kama ndo tqbia yake mwambie abadilike jaribu kumweleza athari zake ..... pia mkumbushe hali ya ujauzito uliyo nao ...... kiubinadam lazma atajirudi Pole sana
 
Huyo shetani mshinde kabisa, maana shetani mwingine unaye ndani, hana tu akili na inawezekana hakupata malezi mazuri kwa wazazi wake, halafu ndugu wa Mme sio wakuwambia hizo habari wengi wao hawanaga maana kabisa, pambana na mwenyewe ukimtanguliza Mungu basi.
 
Eeeh usimfatilie unataka kufa uache watoto wako ety .......akimwaga mboga we mwaga ugali...kama uwezi kumwaga ugali jipe likizo hata ya week 2 ukirudi nyumbani maisha yanaendelea

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Vumilia usikate tamaa hivyo jamani! Mungu akusaidie kulishinda hilo, labda bado mdogo sana yaani upo kwenye uchumba ndoa miezi 6 michepuko 3? Hakuwa siriasi na ndoa huyo, kwanza michakato ya ndoa ikianza michepuko huwa inatoswa ila huyo alikuwa nao , mpe nafasi tena huyo ng'ombe labda atajirudi, kama ni kwa mchungaji angalia maana wote wanaume ujue huwa wanasaidiana hao uchungaji wanaweka kando
 
ndoa sio ngumu best, unavyoichukulia ndo utapata shida

ndoa ni nzr sana maana mko wawili mnashirikishana maisha na kusaidiana

omba na zungumza na mwenzako mambo yatakaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…