Story ya ndugu yangu
Nimeolewa na huyu mwanaume miaka 5 iliyopita,wakati wote huo sikugundua kama ananisaliti.
Nakumbuka ilikuwa mwezi wa pili 2017, mume wangu aliposafiri kuelekea kijijini kwao, alikaa huko kwa muda wa wiki tatu, baada ya kurejea nilibaini kama huko alipata mchepuko, nilimuuliza kwa wema, akakubali na akaomba msamaha, yakaisha.
Lakini baadae nikagundua tena ana mchepuko mwingine kazini kwake, nikamuuliza alibisha sana, nikasema Mungu yupo na atamuumbua. Baada ya muda tena ndo nikayabaini mawasiliano yake na Huyo mwanamke anayefanya nae kazi, (pia huyo dada ni mke wa mtu) baada ya kumuuliza akakiri kosa.
Kinachoniumiza ni leo tena nimegundua bado anawasiliana na Huyo mwanamke, baada ya kumuuliza kanijia juu eti bora ndoa ivunjike.
Please great thinkers nisaidieni ushauri kwa huyu ndugu yangu. Kumbuka ana watoto 3 na ni mjamzito. Pia huyu mwanamke ni mfanyakazi wa serikali, mume pia ni mfanyakazi.
Wakiachana watoto itakuwaje?
Na wanafanya kazi sehemu moja, kisaikolojia athari zake ni zipi? Kwa watoto na wenyewe wahusika