NDOA: Huu ujumbe Unaumiza Sana

NDOA: Huu ujumbe Unaumiza Sana

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,488
Reaction score
100,883
Nimeukuta mahali, Mwandishi simfahamu maana hakujitambulisha.

My Rose, Rositha wangu @rosemdenye jana tumekupumzisha salama nyumbani Ludewa. Umelala hautaamka wala kurudi tena hata siku ya mwisho kwa imani yetu ya Kikristo. Kwenye ibada yako ya mazishi baba ako mkubwa alokupenda mnooo Father Ngailo alizungumza mambo nitaya-share na ambao hawakuwepo Ludewa mama Gidi. Father alisema haya;
.
WANAWAKE na WASICHANA: ndoa ni jambo la heri ikiwa na heri na sio shari. Father ametukumbusha wanawake na wasichana kuwa tusivumilie matendo ya ukatili tunayofanyiwa na wanaume kwa sababu ya ndoa. Ametuasa sana kuvijua VIASHIRIA vya ukatili kwa sababu huwa hauji ghafla. Amesisitiza wanawake tuondoke haraka sana ndoani tutakapoona hivyo viashiria maana hatukuzaliwa na hawa wanaume....tusisubirie kukutana na ulemavu wa kudumu au kifo. Hata wao kama walezi wa imani wako tayari kusikiliza mashauri haya na kuvunja ndoa za aina hii.
.
WANAUME na WAVULANA: Father amesema tuwajulishe kuwa mkituchoka na mkiwachoka wake zenu waacheni kwa amani na sio kuanza kuwafanyia ukatili. Mruhusu mwanamke aondoke kwako au ondoka wewe na ukaanze maisha hayo mengine kuliko kusababisha ulemavu au kifo. Ulipokabidhiwa mwanamke au binti huyo, wazazi wake walikuamini kuwa utalinda uhai wa mtoto wao. Mrudishe akiwa mzima na sio akiwa maiti au mwenye ulemavu mkubwa.
.
WAZAZI na WALEZI: ifike mahali mtoto wa kike anaporudi nyumbani kuwaeleza kuwa maisha yake yapo hatarini basi aeleweke hivyo. Mzazi uwe tayari kupigania uhai wa mtoto wako wa kike wakati wowote. Imekuwa desturi mzazi kumrudisha mtoto na kumwambia kavumilie ndoani maana ndoa ndivyo zilivyo. Akirudi kwa kupigwa kofi moja tu hiyo ni sababu tosha ya kukujulisha kuwa maisha ya mtoto wako yako hatarini...sababu tosha kuwa anaeishi na mtoto wako ni katili. MTOTO KWA MZAZI HAKUI
.
VIONGOZI WA DINI: umefika wakati ambao viongozi wa dini wanapaswa kubadili mtazamo wao juu ya ndoa. Ndoa yenye ukatili na manyanyaso sio ndoa tena inayopaswa kuendelea kukingiwa kifua. Ifike mahali binti anapokuja kwa viongozi wa dini kuwa yupo tayari kuondoka kwa mumewe kwa sababu ananyanyasika na anafanyiwa ukatili basi asikilizwe. Mwanaume KATILI habadilishwi kwa vikao ambavyo havichukulii umaanani.endelea na MAOMBI huku ukiendelea na maisha mbali naye.
.
Pumzika ROSE [emoji257][emoji257][emoji257][emoji257] @ Ludewa, Njombe
 
Ukweli katika ndoa tunahitaji KUELEWANA na sio KUVUMILIANA.

Kuvumiliana ndio mwanzo wa ukatili.

Mtu anapigwa kila siku anaenda kwa wazee au wazazi au viongozi wa dini anaambiwa VUMILIA hayo ndio maisha ya ndoa , haya mawazo ya kusema "VUMILIA HAYO NDIO MAISHA YA NDOA" hayakubaliki kwasasa.

Mtu ameleta malalamiko asikilizwe.
 
Huyo father anakiuka miiko.... NDOA NI MKAO WA KATIKA SHIDA NA RAHA.....
Kuuwana katika NDOA ni moja ya SHIDA maana yule mchungaji kenge ataishia SHIDANI...
amen...
 
Huyo father anakiuka miiko.... NDOA NI MKAO WA KATIKA SHIDA NA RAHA.....
Kuuwana katika NDOA ni moja ya SHIDA maana yule mchungaji kenge ataishia SHIDANI...
amen...

Ndio uliapa kwa shida na raha lakini shida sio hizi za kupigana na kumnyanyasa mwenzio kila siku.

Shida iliyokusudiwa hapo ni Ugonjwa au hali mbaya ya kiuchumi.
 
Huyo father anakiuka miiko.... NDOA NI MKAO WA KATIKA SHIDA NA RAHA.....
Kuuwana katika NDOA ni moja ya SHIDA maana yule mchungaji kenge ataishia SHIDANI...
amen...
Khaaa ndio shida za kutoana roho, kama mtu unaona mmeshindwana ni heri mkaachana kwa amani tu.
 
Huyo father anakiuka miiko.... NDOA NI MKAO WA KATIKA SHIDA NA RAHA.....
Kuuwana katika NDOA ni moja ya SHIDA maana yule mchungaji kenge ataishia SHIDANI...
amen...
Hakuna raha ya kusababishiana ulemavu au kifo.

Father yuko sahihi anakwenda na nyakati haswa.
 
Back
Top Bottom