Ndoa hizi zisikieni tu

Ndoa hizi zisikieni tu

Wapo wanaokesha makanisani wanasaka ndoa wengine wapo ndoani wanajuta kwanini waliolewa basi tabu tupo
back to point.

Kuna binamu yangu yeye hali ni tete kwenye ndoa yake ndoa yake inamiaka 2 anamtoto 1. huyo binam yangu hana kazi anabiashara ndogondogo tu mumewe ni doct.

Jamaa anaishi kiubabe sana mwanamke hana sauti jamaa anaweza amwambie kesho nasafiri akiuliza unaenda wapi we jua nasafiri.

Kipato cha mme hakijui wala matumizi anachojua kala kashiba basi mme alishazaa nje kabla hajamuoa anaongea na mzazi mwenzie mpaka saa 7 usiku hatakiwi kuuliza anaambiwa hayakuhusu kwan huli ukashiba?

Inshort hana amani kabisaa, jamaa ana jeuri vibaya mno anaweza akarudi saa 6 usiku akimuuliza anamjibu mi sio mtoto.

Ndoa hizi zisikieni tu.
Pole sana ila naamini ni wewe mwenyewe na si binamu
 
umeona eeh!wadada tunapenda titles sana mume dk.ukute yule aliyezaa nae ndo anaempenda ila kamuoa huyu ili asipate laana ya wazazi tujifunze jamani!

Hata Mimi napenda mume mwenye title! Goigoi akae mbali na Mimi!
Issue hapa si title ni tabia binafsi ya mtu! kuna uzi mkulima mmoja huko kilombero alimpiga na kumtoboa mke wake jicho kisa amedai talaka baada ya mume kutaka kuoa mke mwingine!
Sasa huyo naye ana title gani?
Na kuna wanaume wana titles zao matajiri wa akili na mali na wanawapenda wake zao na kuwaheshimu!
Mfano my uncle ni well off tena ni advocate mkubwa tu lakini anampenda sana mke wake ambaye ni mama wa nyumbani tena kaishia form 2!
Mume/mke mwema atoka kwa Mungu
 
kwan pesa ndio zinambakiza mtu kwa mwanaume? licha ya mabaya anayotendewa?

Manka we hujui kuna wanaovumilia ili wajisitiri kiuchumi? Anawaza nyumbani kwao hoi labda, elimu huna, ajira huezi pata, biashara hujui, mtaji nao kizungumkuti! Mtoto au watoto ushazaa uende wapi?
Wengine wanaolewa ili kupunguza ukali wa maisha yaani wataponea kwenye ndoa!
Ni sheeeder!
Ndiyo sababu unaona mwanamke anayejiweza kiuchumi ni ngumu sana kudumu kwenye ndoa yenye manyanyaso!
 
Hapo ujue mwanamke anavumilia tu kwa sababu akitema sumu atakuwa hana pa kushikilia,

Mwambie awe anaenda pembeni pale anapoona mumewe anongea na mke mwenzie, simple!

ajifanye tu haoni kama bado anaitaka hiyo ndoa....

Hahaaaaa ndoa ndoano! Ili kubaki mjengoni (kwenye ndoa) ni kuishi kwa matumaini siku zote! Looool inipitie mbali!
 
huo ni upande mmoja wa
shilingi.umeshajiuliza huyo binamu yake anamhudumia vipi mumewe??!!
maana baadhi ya wakinadada wa siku hizi ni hedeki tupu wala hawafai
kuitwa wake. yeye anachojua ni kuvaa ngozi ya kondoo kabla ya ndoa ila
akishaolewa utayaona makucha yake ndugu. jiulize kwa nini huyo dr
hakumuoa mama motto wake wa mwanzo na akaolewa binamu yako halafu sasa
hivi dr anakuwa karibu sana na mama motto wa zamani??!! something is
wrong somewhere na huenda dr anajutia uamuzi wake wa kumuacha mama mtoto
wa zamani na kumuoa binamu yako. usipende kulaumu upande 1 bila kujua
ukweli halisi

umeongea point kwel, huwez kujudge upande moja wakat hujackliza upande mwngne
 
hilo nalo neno maana wadada wa sasa wanvopenda kuolewa,hata ukimuambia ukweli kuhusu jamaa yaani hawaelewagi as long as jamaa katangaza ndoa baaaasi.....akifika huko ndio sasa utumwa wa hiyari unapoanzia cc The Boss.

Hapana mnakosea kusema tunapenda sana kuolewa! Kwani kuolewa si ni jambo zuri tu?? Kupata life partner ni kubaya?
Issue ni unaolewa na nani????? na unatarajia nini kwenye ndoa!
Kuolewa ni jambo zuri na jema la kulipigania kwa hakika! Namuomba Mungu niolewe kabla ya 32! Amen!
 
Hata Mimi napenda mume mwenye title! Goigoi akae mbali na Mimi!
Na kuna wanaume wana titles zao matajiri wa akili na mali na wanawapenda wake zao na kuwaheshimu!

Uko wapi mpenzi wangu nakuhitaji????!!!!
Popote we ulipo ujue bado nakupenda!!!
 
Hapana mnakosea kusema tunapenda sana kuolewa! Kwani kuolewa si ni jambo zuri tu?? Kupata life partner ni kubaya?
Issue ni unaolewa na nani????? na unatarajia nini kwenye ndoa!
Kuolewa ni jambo zuri na jema la kulipigania kwa hakika! Namuomba Mungu niolewe kabla ya 32! Amen!

Sawa!!!!
 
Waswahili wanasema; bora kukosea kujenga nyumba, unaweza ukaibomoa ukajenga ukaijenga vizuri kuliko kukosea kumchagua mwenza.

Back to point;

Ndoa ni nzuri ikiwa utakuwa makini na utajaaliwa kumchagua mwenza anae endana nawe and its vice versal is always true.

Watu huoa au kuolewa kutokana na sababu moja katika nne zifuatazo;
  1. Kuvutiwa na Uzuri
  2. Kuvutiwa na Mali
  3. Kuvutiwa na Mfumo wa maisha / mwenendo
  4. Kuvutiwa na ukoo fulani (Kabila)

Kuoa/ Kukubali kuolewa na mtu kwa kigezo cha mwenendo mzuri ni bora kuliko zilizo baki,

If u fail to plan, u plan to fail

Mungu atunusuru!
 
...Doct...wa kutibu wagonjwa ama Doct wa kusomea?...hizi kada zinanichanganyii....HATA BUNGE LA KATIBA utasikia Doct,....hujui ni wa fani ipi
 
Hapana mnakosea kusema tunapenda sana kuolewa! Kwani kuolewa si ni jambo zuri tu?? Kupata life partner ni kubaya?
Issue ni unaolewa na nani????? na unatarajia nini kwenye ndoa!
Kuolewa ni jambo zuri na jema la kulipigania kwa hakika! Namuomba Mungu niolewe kabla ya 32! Amen!

!NUKTA...kama nakuona vile.
 
Mmmmhh kuoa/kuolewa na MTU Mwenye mtoto yapaswa kuwa mvumilivu
 
Wapo wanaokesha makanisani wanasaka ndoa wengine wapo ndoani wanajuta kwanini waliolewa basi tabu tupo
back to point.

Kuna binamu yangu yeye hali ni tete kwenye ndoa yake ndoa yake inamiaka 2 anamtoto 1. huyo binam yangu hana kazi anabiashara ndogondogo tu mumewe ni doct.

Jamaa anaishi kiubabe sana mwanamke hana sauti jamaa anaweza amwambie kesho nasafiri akiuliza unaenda wapi we jua nasafiri.

Kipato cha mme hakijui wala matumizi anachojua kala kashiba basi mme alishazaa nje kabla hajamuoa anaongea na mzazi mwenzie mpaka saa 7 usiku hatakiwi kuuliza anaambiwa hayakuhusu kwan huli ukashiba?

Inshort hana amani kabisaa, jamaa ana jeuri vibaya mno anaweza akarudi saa 6 usiku akimuuliza anamjibu mi sio mtoto.

Ndoa hizi zisikieni tu.

Isije ikawa huyo binamu yako alikubali kuolewa na jamaa kisa ana profession ya udocta na kumuacha mapenzi wake aliyemwona kuwa hana future!!.kama ndio hivyo basi mwabie ajue laana inamtafuna sasa.
 
Back
Top Bottom