Ndoa halali kisheria ya wake wengi inawezaje kuwa na upendo na mapenzi ya dhati???

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Wapenzi wa jamvi hili,
Nimekuwa nikijiuliza sana hivi ndoa za wake wengi mfano wanne hata kama ni halali kisheria huwa zina upendo na mapenzi ya dhati kweli miongoni mwa wanandoa? Mimi naona lazima mume atampenda sana mke mmoja kuliko anavyowapenda wake wengine watatu. Vilevile, lazima mume awe na mapenzi kidogo kwa mke mmoja kuliko wengine watatu. Mnasemaje wadau?
 
mwenzetu..haya mambo ya mitala tuwachie wenyewe. Wanajua wanachokipata humo. Wengine ni hifadhi tu lakini wana wapenzi wao wa pembeni kama kawa.Waulize wazaramo wataku darasa POL 100.
 
mwenzetu..haya mambo ya mitala tuwachie wenyewe. Wanajua wanachokipata humo. Wengine ni hifadhi tu lakini wana wapenzi wao wa pembeni kama kawa.Waulize wazaramo wataku darasa POL 100.

Haswaaaa, nami nakubaliana na wewe. Hakuna cha upendo wala nini. Kwa mwanaume ni tamaa tu ya kuwa na sampuli tofauti za wanawake ili kuwa na appetite muda wote. Kwa wanawake ni hifadhi kijamii na kiuchumi lakini kingono lazima wapate pembeni kwa namna yoyote ile.
 
Wapenzi wa jamvi hili,
Nimekuwa nikijiuliza sana hivi ndoa za wake wengi mfano wanne hata kama ni halali kisheria huwa zina upendo na mapenzi ya dhati kweli miongoni mwa wanandoa? Mimi naona lazima mume atampenda sana mke mmoja kuliko anavyowapenda wake wengine watatu. Vilevile, lazima mume awe na mapenzi kidogo kwa mke mmoja kuliko wengine watatu. Mnasemaje wadau?

Dumelambegu,

Umelenga ndoa za kijadi katika makabila yetu? Au wake wanne tu?

VIDEO REPORT: Polygamist dies in Kenya leaving 100 wives; 160 children

Mkuu, Kwa wenye "nyumba ndogo",vimada, wapenzi 2,3,4, 5,6 ruksa !!?

https://www.jamiiforums.com/habari-...105997-ungetoa-ushauri-gani-nini-wafanye.html

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/110839-ndoa-za-wake-wengi.html

Dunia uwanja wa fujo...kila mmoja na kanuni zake!!!
 
Mi mwenyewe najiulizaga hili swali. Yani ndo mkiwa pamoja mnamwita mume wetu!! Mume wetu........!!
 
mmmh hapa naona ya kaisari tumuachie kaisari....
Personally naona kwa upendo wa dhati haiwezekani, na kwa maisha ya sasa haifai.. lakini kama nilivyosema
Ya Kaisari tumuachie Kaisari
 
Inawezekana yupo mwanaJF ambaye ana mke zaidi ya mmoja.... anaweza kutueleza ukweli....je anapoenda kuoa mke wa pili, ni kweli bado anampenda yule wa kwanza??? Halfu sio fair kabisa......inabidi na wanawake wanaruhusiwe na mume zaidi ya mmoja... usawa kila eneo..:coffee:
 
ni tamaa za mwili tu,, hakuna kitu hapo. Tena utakuta anahangaikia wengine pembeni ya hao wanne wake wa ndoa...
 
Acheni wivu bwana, sasa kama yule jamaa wa Misri mwenye maguvu kama kifaru akiwa na mke mmoja si itakuwa balaa? ni afadhali yeye anayeoa wanne au sita wakajulikana kuliko anayeoa mmoja then anapanga nyumba ndogo kumi!
 
Itakuwa fair kwa jamaa wa misri... Je ni fair kwa hao madada
Pia watoto wakiwa wengi Je wote watapata attention ya Baba yao...
 
Acheni wivu bwana, sasa kama yule jamaa wa Misri mwenye maguvu kama kifaru akiwa na mke mmoja si itakuwa balaa? ni afadhali yeye anayeoa wanne au sita wakajulikana kuliko anayeoa mmoja then anapanga nyumba ndogo kumi!

Hata kama wakiwa halali au wa mafichoni...point ni kwamba siku zote sio rahisi ukawapa upendo sawa wote...ulipoamua kwenda kwa wa pili, yule wa kwanza alishachuja tayari!! hata kama utawapa mahitaji muhimu, nafikiri ndoa si kwa ajili kula, kunywa na kuvaa! Vyote hivyo waweza kuvipata bila kuolewa!!!
 
Back
Top Bottom