Ndo uanaume wenyewe au nina tatizo?

Ndo uanaume wenyewe au nina tatizo?

I mean kwa watu wengine mfano rafiki zangu ndungu na watu wengine wenye uhitaji huwa natoa pale napoguswa
Eeeh!
Kumbe hauguswi na wanawake!
Nahisi wewe utakua na matatizo ya kisaikolojia.
[HASHTAG]#Missnatafuta[/HASHTAG] anatakiwa akuombee.
 
Siyo tatizo kabisa...

Kila mtu ana namna yake anvyopenda kuishi na kuendesha mambo yake... Binadamu hatuwezi kuwa sawa wote...

Smart911 takes care and gives all mahondaw anytime, any place without hesitation or thinking negative... Same from mahondaw to Smart911...

Tunasema love with collaboration...

Cc: mahondaw
 
dalili ya ubinafsi na uchoyo...
vipi mtu baki akikuomba msaada wa pesa,unatoaga au???
 
Habari zenu wakuu..
Jaman mwenzenu nimekua na tabia moja ambayo nashindwa kuelewa kwamba ni tatizo au ndo uanaume. Mwenzenu huwa cwezi kutoa pesa kwa mwanamke, kila nikitaka kutoa pesa nachukulia kama nahonga vile naahirisha, yaani mwanamke akiniomba pesa huwa natokea kumdharau na kumchukulia kama hana mapenzi ya kweli anataka kunichuna na inaweza kuwa sababu ya mm na yy kuachana. Haimaanishi kwamba cna pesa ya kuhonga au kumpa mwanamke, ila tu imekua tabia yangu kutokutoa pesa.
Sasa hili ni tatizo au kitu gan? Mwenye ushauri plz!!!
Zawadi unanunua?

Out kwenye movie na dinner unawapeleka?
 
Siyo tatizo kabisa...

Kila mtu ana namna yake anvyopenda kuishi na kuendesha mambo yake... Binadamu hatuwezi kuwa sawa wote...

Smart911 takes care and gives all mahondaw anytime, any place without hesitation or thinking negative... Same from mahondaw to Smart911...

Tunasema love with collaboration...

Cc: mahondaw
Asante mkuu
 
Habari zenu wakuu..
Jaman mwenzenu nimekua na tabia moja ambayo nashindwa kuelewa kwamba ni tatizo au ndo uanaume. Mwenzenu huwa cwezi kutoa pesa kwa mwanamke, kila nikitaka kutoa pesa nachukulia kama nahonga vile naahirisha, yaani mwanamke akiniomba pesa huwa natokea kumdharau na kumchukulia kama hana mapenzi ya kweli anataka kunichuna na inaweza kuwa sababu ya mm na yy kuachana. Haimaanishi kwamba cna pesa ya kuhonga au kumpa mwanamke, ila tu imekua tabia yangu kutokutoa pesa.
Sasa hili ni tatizo au kitu gan? Mwenye ushauri plz!!!
Mimi kama ni mwanamke akishaniomba huwanamfuta hata kweli simu yangu kabsa, katika vitu nisivopenda mimi nikuombwa hela tena kwenyemtandao na mwanamke usie mjua, inakera aise, tena saana.

Kuomba hela ni tabia mbayaa saana
 
Zawadi ni kawaida kununua, huwezi kuacha kununua zawad
Basi wewe ni O.G tu (Original Gangstar).

Una kanuni za kizamani za kishua kwamba kutoa hela kwa mwanamke ni kama kununua papuchi. Ni kama unafanya kununua malaya unaona.

Wanunulie zawadi tu basi.

Zawadi ni muhimu kuliko hela. Kwa sababu zawadi inakulazimisha ufikirie cha kununua.

Ila tatizo, mara nyingi, kwenye jamii zetu za kimasikini na wanawake wanaoendekeza umasikini huo, hela inaonekana muhimu kuliko zawadi.

Tatizo la zawadi, si kila mara utanunua zawadi nzuri kwa mtu, na mtu anaweza kuwa anahitaji hela kuliko zawadi.

Kuna mwanamke alimkandia mwanamme kwa sababu mwanamme hakuwa tayari kumpa hela ndogo.

Kumbe yule mwanamme alikuwa hataki kutoa hela, hususan hela ndogo, alikuwa anataka kutoa zawadi kubwa na kupanga mambo yenye future.

Ila mara nyingine hela inaweza kurahisisha mambo zaidi kuliko zawadi, hususan kama mmeshibana na huna sababu ya kutompa anachotaka na anachotaka ni hela kufanikisha mambo fulani.

Nina mfano tofauti kidogo, kwa sababu si wa mpenzi, ila ni wa mtu ninayempenda (mpendwa I guess). Kuna dada yangu (binamu) mmoja alininunulia vitabu adimu kutoka Tanzania, nilikuwa navihitaji sana huku niliko, nikamuomba na kumtumia hela akaninunulia akanitumia.

Nikamshukuru, nikasema nitamtumia zawadi.Muda ukawa unapita kila siku nikasema nitanunua zawadi. Ikafika siku nikasema sasa umepita muda mrefu, ngoja nimtumie hela tu anunue anachotaka.

Hapo hela ilikuwa imerahisisha zawadi, kwa sababu ningeweza kumnunulia zawadi ambayo yeye haipendi na Magufuli akamchanja kodi juu.

Kwa hiyo kuna sehemu hela ina nafasi yake, na kuna sehemu zawadi ina nafasi yake.
 
Back
Top Bottom