Mbona hatuaminiani, kuna muda nimeweka rope hapa wakaikata mods, sitakata niirudie maana ilikuwa inahusu kikao cha dharula sehem fulani,
Wana CCM ndo mnaunda serikali kwa kupewa dhamana na Taifa na wananchi wake,
Kuna waziri mmoja anavujisha siri za baraza ilo na kina Ngurumo wamemfaidi sana kule walipo, jamani tuaminiane, tumkosoe hapo hapo kama anakosea, tumdhibiti kama anataka kuvuka mpaka lakin so vema kuvujisha siri hizo, hivo kichwa cha waziri mwingine ambaye alileta mvuto naye anaondoka soon Tuwe wakweli
Baraza linamkosa Nchemba ,Nape sasa na huyu kijana dahh
Britannica
Usichonganishe watu .
Siasa sio uhasama.
Tulitegemea awamu ya tano muhula huu wa kwanza kuelekea 2020 serikali iende mbele zaidi katika kupambana na wizi wa Mali za Umma, usalama wa watu na Mali zao ,kupiga vita rushwa kubwa na ndogo, kuhoji viongozi na watumishi wenye mali zisizolingana na vipato vyao, kupinga uonevu wa vyombo vya mabavu kwa wananchi, kutoa sana elimu ya kuheshimu sheria , kusimamia haki kwa wote bila kujali itikadi zao, Kuanzisha makazi na miji mipya iliyopimwa kisasa, ujenzi wa barabara za mwendo kasi (kuelekea Mbagala ,Airport na Mandela road), Kuvutia wawekezaji wa ndani kwa masharti ya kushirikiana na wale wa ndani, kuvutia wawekezaji wa viwanda vya Sementi ( ili ishuke bei kufikia 5000/-), kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya Chuma ili kufufua mgodi wa Chuma Liganga, Kupunguza kodi na ushuru wa bandarini kwa mizigo isiyozalishwa nchini (kama magari n.k ), kutoa mishahara ya watumishi wa umma inaolingana na uhalisia wa maisha ya mahitaji ya msingi ya binadamu, kuanzisha makambi ya JK kwa ajili ya vijana kujifunza ufundi,ujasiriamali na kilimo,kuimarisha miundo mbinu ya vijijini, kujenga mabwa ya maji kwa ajili ya mifugo na kilimo, kujenga masoko makubwa kabisa ya kimataifa ya mazao ya kilimo mipakani, kupunguza kodi kwa wafanyabiashara wadogo na kusimamia masuala ya kodi za frem ili zisiwe zinakua tofauti na zile za serikali. Kuanzisha umeme wa Makaa ya mawe,gasi, mwanga wa jua na upepo, Kutunza mazingira kwa kutumia teknolojia mbadala kama gesi , Kuzuia kabisa suala LA watumishi hewa, Kujenga dhana ya Cheo ni dhamana ili watawala na viongozi wawaheshimu wananchi wao na kuwasikiliza sio kisiasa bali kwa misingi ya sheria bila kuonea watu kwa itikadi za kisiasa, tukuze zaidi diplomasia na mataifa ya mengine duniani kwa lengo la kujitangaza kwa sifa njema ili kuvutia watalii kwa wingi zaidi hasa watalii kutoka nchi za magaharibi, kutoa mikopo ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu, kupunguza ada za sekondari na shule za msingi lakini sio kuzifuta kabisa huku mzigo ukibakia wanapofika elimu ya juu serikali inakosa uwezo wa kutoa hata mikopo 100%, kujenga while za Msingi na sekondari za ufundi, Uhuru wa wananchi kupata habari kwani hauzuii watwala kutimiza majukumu yao, Kuimarisha muhimili wa mahakama na kuuacha uwe huru ili kila mtu atendewe haki bila upendeleo wala vitisho, kujenga demokrasia zaidi ili wananchi wapate fursa ya kuchagua viongozi wenye uwezo na nia ya kuwatumikia na kuweka maslahi binafsi pembeni bila kujali vyama, kutumia vyanzo vya maji vikubwa kama ziwa Victoria ,Tanganyika,Nyasa,Rukwa , Jipe ,na mengine kusambaza na kuwapatia maji wananchi bila kujali itikadi za vyama. Kuwatafutia maeneo rasmi wafanyabiashara wadogowadogo ili kuondoa kero ya kufanya biashara barabarani, Kulinda mipaka yetu zaidi, kudumisha kwa vitendo umoja, mshikamano na amani miongoni mwa watanzania, kudhibiti kwa vitendo aina zote za upendeleo na urafiki kwenye kazi umma na kuzuia na kudhibiti vitendo vya wizi wa mitihani, kuweka fursa za vyombo vya mawasiliano kushindana kwa haki sawa ili bila mwananchi kuumizwa n.k
Haya ndiyo watanzania na binadamu yeyote aliyeko huru tulikua tunayataka na kuyategemea sana kuwa tutayapata awamu hii ya Tano kutokana na Kamapeni za mwaka 215 na shamrashamra zilizokuwepo ikiwemo pushapu ,sio umaarufu wa mtu au Chama au kikundi cha watu.