Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015!

Mali za Lowassa hazisemwi kama alivyokuwa Mubarak madarakani penginehuelewi nafasi ya Lowassa ndani ya chama kulingana na mjadala huu, nimeyasema mengi sana. Kama EL ataondolewa madarakani kabisa, na hakubaliki na wananchi kama Mubarak mali zake zitakuja julikana wala sii zake tu na wenigine wote waliokuwa chini yake ama pamoja naye - Lowassa hajaondoka bado.

Pili, kinachonifanya kutompenda Lowassa sii utajiri wake narudia tena sii utajiri wake bali UFISADI wake sijui anapokea kiasi gani ktk madeal ya Citywater, Richmond, Buzwagi, Bulyanhulu, Mara, TRC, ATC, Bank kuu na kadhalika list ni ndefu sana, maamuzi mabaya yalifanyika chini ya uongozi wake na kutugharimu hadi leo acha mbali hesabu za siku zake akiwa madarakani.

Tatu, maadam mimi na explore reality nakuomba nambie hivi kweli Lowassa akiwa rais, Chadema wataweza kuzungumzia Ufisadi tena? kuna mtu anaweza kusimama na kulaani Ufisadi chini ya jicho lake..JF kweli itapona au itakuwa hii ya leo.... na mtu anayesema JK achukue maamuzi magumu.. Unamkumbuka T. Mhando alipo sukuma issues za Chadema ilikuwaje? Mwandishi wa rais Rweyemamu akimwandikia yeye barua ya kuomba ajira na sio ofisi ya rais. Mawaziri wakijipendekeza kwake wachaguliwe uwaziri na hadi ubunge bado huoni ubaya wa huyu mtu hadi ujue mali zake?. wabunge ili wapate kutumikiwa majimbo yao lazima wajipange naye ktk kumlamba miguu..

Ebu nambie wewe siku Ile Dr.Slaa alipomtaja Lowassa kama fisadi ulielewa vipi kama unajua haikuhusiana na kukwapua mali za Umma..Na Je, wewe unasubiri pato la Taifa liibiwe lenyewe na sio mikakati inayolikosesha Taifa mapato sio wizi sio?..Basi watu tunatazama vitu tofauti sana maana wewe unatazama kimachinga wakati mimi natazama sera na mikakati..

Siwapingi na Chaguo lenu, lakini tafadhali msitake kuupoteza Umma kama nyie mnamchagua Lowassa mchagueni kwa matakwa yenu lakini kumpigia chapuo hapa JF kama vile sisi mijinga iliyolala hapo wakuu zangu mnatupeleka kusiko... tumjadili kwa sifa zake na mziweke wazi lakini sio tu Lowassa hana madhambi wanamsingizia.. Huyu mtu ni hatari na sioni tofauti yake na Dikteta wa Syria au Ghadaffi ana agenda chafu sana.
 
 
Mfano wa Sigara hauhusiani kabisa na Ufisadi hata kidogo. Ufisadi unaweza fanywa na baba watoto wasiwe mafisadi, unaweza fanywa na ndugu mmoja wengine wakawa wazuri hii ni hulka ya mtu - period.

Na unamhukumu mtu kwa hulka yake na sio kusingizia sigara maana mvuta sigara anaweza kuacha kuvuta lakini sio fisadi . Tatizo lenu mnafikiri kwamba hata fisadi anaweza kuacha Ufisadi akilishwa zaidi..Hapo ndipo mnapokosea toka lini ikawa hivyo na hamna hata mfano mmoja wa fisadi aliyewahi kuwa fisadi akaacha Ufisadi kwa sababu kapewa nafasi ya kuongoza..Magereza zisinge jengwa!.

Oooh Pasco! maneno yako kweli uliposema - Kama kula nguruwe tumchague aliyenona! basi Lowassa amenona haswa.....ina maana tunamchinja na kumla sijui tumchome kwa moto ndio atapendeza zaidi na kumwekea pilipili.. maana ndio hatakuwepo tena..Wewe ndio kwanza unataka kumfuga anone zaidi huku wewe una njaa ya kufa.
 

Well said, Mkandara. Sina cha kuongeza hapo.

Labda tu niulize recycling Tz itakwisha kweli kama mambo yenyewe ndo hivi?
 
Well said, Mkandara. Sina cha kuongeza hapo.

Labda tu niulize recycling Tz itakwisha kweli kama mambo yenyewe ndo hivi?
Haiwezi kwisha mkuu wangu kwa sababu matatizo ni sisi wananchi kama alivyosema Mag3. Na matatizo haya tunayaona kwa mifano hapa hapa JF, watu wanazungumzia biashara za kimachinga kwa maana tunashindwa kufikiria nje ya hapo.. ndio maana hadi leo hatuwezi hata kutengeneza sindano ya kushonea wakati nasikia Ethiopia leo wanatengeneza magari na umeme wa kumwaga.
 
Zing said:
Utadhani bongo zetu zimekuwa cloned kwamba Bila medula oblangata ya Eddo magogni basi UFASADI hautaisha
Mkuu "medula oblangata" zaidi ya EL ziko nyingi tu, sema haziko kwenye hizo cycles za kisiasa...

Cha kwanza kwenye cycles hizo ni majina yenye influence kwenye siasa, pamoja na watu wao wa karibu ndugu jamaa na marafiki etc, then pesa...

Simply as that, hata ukielezea kwa namna gani, this is the bottom line...Kwamba tutawapata viongozi kutokana na cycles za kisiasa...

Na hivyo si kweli kwamba EL ndo ameonekana kuwa anafaa kati ya wenye "medula oblangata"

Bali tunamzungumzia yeye kwa kuwa yuko kwenye hizo cycles zinazo determine ama kutoa viongozi wakuu wa nchi...

Kwa kifupi yuko kwenye tabaka la watawala...
 

nikuongezee mzee kama unakumbuka barabara ya shekilango ilisuasua kuanza ujenzi, siku hiyo kaenda na waandishi wa habari na kupayuka pale nataka barabara hii ianze mara moja kesho na kesho yake tunaonesha kwenye matv kazi imeanza nikabahatika kuongea na engineer mmoja pale site akasema mwongo walikuwa wemeshaweka vifaa kuanza kazi kesho yake na alilijua alipotuma vijana wake na yeye kuwahi one day before! mjinga sana huyu jamaa

hatutaki viongozi wa namna hii kwa kweli
 
Mkuu I hope na naomba sana isiwe kwamba mnamfagilia huyu jamaa kwa malengo fulani maana katika cycles za viongozi hakuwepo aliingia kwa nguvu na Ufisadi mkubwa dhidi ya wale aliowakuta. Kajipandisha cheo kama Hitler au Idd Amin na mtu kama huyu lazima tumwogope sana halafu wala msifikirie kwamba JK leo anaongoza nchi bila Lowassa..

Lowassa yupo na amejaa tele kama pishi la mchele...hivyo, matokeo yote mnayoyaona leo yanatokana na kuwepo kwake kwa sababu wapo viongozi wengi wanashindwa kuifanya kazi yao kwa sababu yake. Mwinri, Mama Ana Tibaijuka, Magufuli ni miongozi mwa wachache wanajaribu kutoa ushawishi wa maana lakini wamefikia mahala wanakwenda na upepo tu.

Huko Ikulu na Usalama ndio usiseme aidha uko na Lowassa au kinyume ndio utanafsirika umesimama wapi na hakuna upande wa JK..Ni siasa ambazo zipo bungeni hadi NEC CCM wenyewe makundi ndani ya chama ni ya Lowassa na wapinzani wake..JK haonekani ni hakimu aliyepigwa Kipapai.
 
True, on the other hand, kama ukiwa upande wa EL ninaamini ni sawa na kuwa upande wa JK na ukiwa upande wa JK ni sawa na kuwa upande wa EL, hilo wengi hawalioni.
 

ongezea na
1. scandal zake za ustawishaji makao makuu
2. scandal zake za Kituo cha uwekezaji cha Taifa

Sitta hafai kabisaaa.......
 
Lowassa ni mpiga kelele, arrogant, dharau sana kwa wananchi, yes hufanya maamuzi.......lakini maamuzi yake ni yale ya kupiga hatua moja mbele na kurudi hatua kumi nyuma..........damn Lowassa!
 
ongezea na
1. scandal zake za ustawishaji makao makuu
2. scandal zake za Kituo cha uwekezaji cha Taifa

Sitta hafai kabisaaa.......
Lakini mbona mnamsema Sitta kwa ushahidi ambao hamuukubali kwa Lowassa?.. Siita hafai lakini kwa uchache wake ni bora kuliko Lowassa yaani Lowassa hana mfano CCM hata mdogo na tunaendelea kuishi ktk zama zake. Hivi jamani mmewahi kujiuliza kwa nini wazungu wanatengeneza vicatoon vya kina Batman, The Incredible Hulk, The Magnificent seven na kadhalika kama sii kusisitiza kizazi chao kiwe na Ujasiri wa kupambana na Ufisadi wakati hawa ni mabepari..Sasa leo sisi badala ya kujifunza na catoon ama sinema hizi kumbe tunaenda kutazama kama intertainment na kurudi nyumbani tukisimuliana jinsi Jambazi lilivyowasumbua..

Jamani ni wakati wenu nyie vijana, vijana ambao niliweka sana matumaini yangu toka mwaka 2003 na sitaki kuamini hata nyie mmefikia mahala mnasema basi hatuwezi tena bora tuishi ktk maisha ya Ufisadi kuliko kuendelea ku support watu ambao hawaaminiki wakati nyie wenyewe mnaonyesha wazi kutoaminika maana niliweka matumaini yangu makubwa sana kwenu.

La ajabu sana mnapomsema Sitta hali nanyi mnachukua maamuzi kama ya Sitta kusalimu amri kwa Lowassa, sasa huu kama sii unafiki kitu gani jamani. Siitta Fisadi na anaogopea uhai wake he has a point na hamuwezi kumlinda kwa sababu sisi wanafiki tu...Mtanisamehe lakini kusema kweli nimesikitika sana na kujiona mjinga sana kupoteza muda wangu wote kuweka matumaini kwa vijana wa leo wanamageuzi kumbe nao yale yale wananunulika?.... naosha mikono!
Tutapambana ktk uwanja wa wazi na hapo ndipo kitaeleweka!
 

Asante sana Bob.........
 
Mkandara kaka yangu. Mbona ya Richmond umeshaambiwa kwenye NEC ya CCM? Yaani ukweli unaujua lakini umeamua kuupindisha?
Richmond Lowassa alikua bangusilo!

a Big NO.....Lowassa hakuwa bangusilo Richmond (hiyo ni picha anayojitahidi kui-paint).............JK hakumuambia Lowassa apindishe ushauri wa Tanesco FYI.....huo ulikuwa ni ushauri wa EL kwa JK..........
 

NO...tofauti na Karume (RIP)...haikuwa idea yake......isitoshe......mradi ule wa shule za kata haukuwa na hauko endelevu....Edo aliuvaa mradi ule kwa nguvu ili ku-cover movements zake.........
 
a Big NO.....Lowassa hakuwa bangusilo Richmond (hiyo ni picha anayojitahidi kui-paint).............JK hakumuambia Lowassa apindishe ushauri wa Tanesco FYI.....huo ulikuwa ni ushauri wa EL kwa JK..........
Unajua watu wasauhaulifu sana na nadhani hili ni tatizo la Wadanganyika.. Inabidi tukapimwe vichwa vyetu maana ni huyu huyu Lowassa akiwa madarakani tuliona Karamagi akichukua bandari TICKS, Mzee Kigunge akichukua vituo vya Mabus na Parking, mashirika ya simu na TV yalokuwa na bei nafuu kwa wananchi yakipigwa vita hadi yakafilisiwa na kuzaliwa kwa Voda ambayo contract zake zote ni za serikali ya Lowassa, EPA, Buzwagi, Banki kuu Mama Meghji akitoa mabillioni na kutetea bungeni mwisho wake mabangusilo Balali, Msabah, Diallo na Karamagi aliyeweka mkataba akiwa London wakajiuzulu.. hivi kweli hawa wote ni heroes kwa kujizulu mbona hawasemwi ila Lowassa!... Likaundwa baraza jipya la mawaziri yote kutokana na kushindwa kwa waziri mkuu kuongoza njia inayotakiwa, leo bado watu wanamfikiria Lowassa...Ama kweli kama hutastaajabu ya Mussa ya Firaun kiboko..
 

hata mimi nimepita shule, kama sitakuelewa katika hili, basi walimu wangu walifanya kazi bure.

(japo siku nyengine nitataka ushahidi wa madai yako kuwa Lowasa 'alimpangisha' JK ikulu)
 
Kama historia ni kitu cha kuamini na kukitegemea Lowasa hawezi kuwa Rais wetu. Hakuna kiongozi nchi hii amewahi kuwa WAZIRI MKUU kisha akawa RAIS mbali na Mwalimu ambaye hata hivyo alisaidiwa na Tanganyika kuwa Jamhuri na badiliko hilo likatupatia muundo mpya wa uongozi wa nchi yetu.
Nafasi ya Uwaziri Mkuu imemnajisi sana Lowasa kuliko mwingine yeyote kati ya waliowahi kushika wadhifa huo. Hauwezi kuwa Waziri Mkuu mchafu wa kiwango hicho halafu watu wazima na akili zao wanakaa kukujadili upewe nafasi ya juu zaidi. Tunahimizana kabisa humu kama mazuzu kumkubali Lowasa kama vile nchi imeishiwa kabisa viongozi.
Naamini hata JMK alipomteua Lowasa kuwa Waziri Mkuu mbali na makubaliano waliokuwa nayo alidhani mara hii Lowasa angebadilika. Kwa mshangao wake hakuamini alichokishuhudia kwa huyu swahiba wake. Hakuna namna ya kumbadili mtu anayependa na kuabudu mali na hasa aliyepata mali hizo kwa njia za madaraka aloopewa na UMMA.
Lowasa ni "spent force" tayari. Tuangalie mbele tunakoelekea.
 
nakubaliana na mkuu waberoya, CCM wote ni wezi, hakuna msafi CCM, huyu EL nakumbuka aliwahi kusema bungeni, ameonewa sana, amedhalilishwa sana, na tatizo ni uwaziri mkuu......sasahivi anautafuta urais kwa nguvu zote ili wale waliomuonea na kumdhalilisha arudishe kisasi kwao, kwa CCM hata wakimteua malaika kutoka mbinguni asimame 2015 bado atageuka kuwa shetani kama lucifa maana waliomteua ni wezi na lazima afuate matakwa ya wezi hao, HAKUNA ANAYEFAA CCM, PERIOD.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…