Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndiyo, Lowassa ni fisadi na hilo halina ubishi lakini ndani ya CCM yupi ni afadhali Urais 2015!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Dec 27, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wanajamvi, bila shaka lolote kila binadamu hupenda madaraka, hupenda sifa na hupenda mali na kama yupo binadamu ambaye hapendi hivyo vitu, huyo hajaumbika nikiwa na maana ana mapungufu fulani. Kinachotutofautisha ni msukumo na kiwango cha tamaa kilicho nyuma ya jitihada zetu katika kuvitafuta. Tamaa ya wastani ni kitu kizuri kwani haitoi nafasi kwa tabia za ulafi, udanganyifu, wizi na hujuma. Lakini tamaa inapovuka mpaka, then hell breaks loose, na vyama kama CCM hugeuka na kuwa kama shamba la kuotesha na kukuza mafisadi kama Lowassa.

  Edward Lowassa ni mfano tosha wa mavuno halisi kutoka shamba hilo la CCM lakini tofauti kati yake na makada wengine ni kwamba anawajibika. Aliwajibika kama Waziri Mkuu kwa kujiuzulu ili kuisetiri serikali ya CCM pamoja na Kiongozi wake mkuu, Raisi Jakaya Mrisho Kikwete. Kwa hekima fisadi msaidizi ilibidi ajiuzulu ili fisadi mkuu abaki madarakani kumlinda yeye na mafisadi wengine ndani ya chama na serikalini. Hata hivyo yanayotokea sasa ni uthibitisho tosha kuwa ushirika katika maovu hauwezi kudumu milele na ni swala la muda tu kukuru kakara huanza.

  Washiriki wote katika kuisetiri serikali pole pole wanaaza kuvuna walichopanda tukianza na Mwakyembe, Sitta, na Kikwete mwenyewe. Nyumba (CCM) inayowasetiri imeanza kuungua moto na taratibu moshi wake umewaathiri wote wanaoishi humo kiasi wanashindwa hata kuonana. Lengo langu hapa si kumtetea Fisadi Lowassa, la hasha, kwangu adui mkubwa wa taifa letu si mtu moja bali ni zimwi CCM. Ndani ya CCM naamini hakuna aliye safi hata moja lakini kama ni kumla nguruwe, hakuna aliyenona kama Edward Ngoyai Lowassa, mbunge wa Monduli.

  Mimi, tofauti na wengi, naamini EL pamoja na madhambi yake yote, katika kujiuzulu Uwaziri Mkuu alitumia busara. Nampongeza kwa tendo lake hilo, likifuatiwa na la juzi la kukataa kujiuzulu CCM na kumhusisha Raisi katika sakata la Richmond, jambo ambalo limezidi kuiumbua CCM na kuiacha uchi. Wakati wa Richmond kuna watu kama Hosea tulitegemea wangejiuzulu lakini hawakufanya hivyo na leo kuna watu kama Luhanjo tulitegemea watajiuzulu mara moja lakini bado wapo tu ! Tusidanganyane, Kikwete hakuwa na ujasiri wa kumfukuza Lowassa.

  Karibuni mtakaodai na mimi Mag3 niko kwenye payroll ya Lowassa, hilo halinipi taabu hata kidogo, siwezi kumzuia yeyote kufikiria hivyo. Ukweli ni kuwa kama Raisi 2015 atatoka CCM (na hilo Mungu atupishilie mbali !), basi ndani ya hiki Chama cha Mafisadi, kwa sasa hakuna kama Lowassa kama taifa linataka kujinasua kwenye dimbwi la utawala legelege uliojaa usanii. Uwajibikaji, uvumilivu na ujasiri aliouonyesha ni dalili nzuri katika Uongozi kama hazitasukumwa na ulafi na tamaa, vitu ambavyo hata hivyo vimemganda kama kupe na kumwandama kama kivuli chake !
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Aliye afadhali hajulikani, anayejulikana hana afadhali.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mhh
  Mi ndhani anayeuliza nani ana afadhali ndai ya CCM kuliko Lwasa labda kwanza atujibu yeye mpaka anamuona Lowasa ana afadhali kamlinganisha na kina nani?

  Yaaani kama huoni hata mmoja au wawili wenye afadhali kuliko Lowasa ndani ya CCM basi wewe utakuwa na tatizo.

  Mimi naweza kukutajia hata Wilison Mukama, Nape. SAS, Membe, Asha Migiro etc .
   
 5. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwani Lowasa kakwambia nataka kuwa raisi? au wabongo wamekuambia kuwa wako kkwenona wewe ye mchakato wa kumtafuta rais mpya? Mbona wewe ni mmbea kiasi hicho kama sio kiherehere. Lowasa kakupa bei gani ili uanze kumpigia debe?
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kundi la Mwanakijiji linaanza kumsafisha EL; Mag3, one..two..I am counting
   
 7. k

  kamangaza25 Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 15
  we acha ujuha wako
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280

  duh!................
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  wewe utakuwa hujasoma kilichoandikwa
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Amesema hivyo ili tusimshtukie ..nakwambia soon utamwona mwanakijiji na makala marefu ku-divert public attention kujitayarisha kwa ajili EL

  Ukishajua bei ya mwanaharakati inakuwa tamu sana
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nadhani ulitaka kusema dr.salim may be umekosea bahati mbaya kutokana na lowassa kumwaga watu wengi humu ndani kuhakikisha jina lake halitoki masikioni mwa watu ili kuwachanganya,naona mtego wake umekunasa bahati mbaya kama nilivyosema lakini lengo lilikua ni salim,kwa kuwa yeye ni ccm damu na sio fisadi na hata zile tuhuma kina kikwete na lowassa walizombambikia imekuja kuonekana ilikua ni uzushi kutokana na uoga waliokua nao dhidi yake.Salim anafaa kuwa rais na ataiweza ccm na tanzania pia atamuweza mgombea wa chadema,halafu ni mzanzibari hili tusilisahau mana juzi tulimsikia maalim seif akikumbusha kwamba safari ni busara rais akatoka upande wa pili wa muungano ili kuuenzi muungano wetu.
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  Salm ana msimamo gani juu ya muungano?
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, hajulikani mwenye uafadhali na mpaka sasa wote wanaojulikana hakuna mwenye uafadhali !
  Ni kweli Dr. Salim Ahmed Salim hana makuu yake yanayojulikana lakini kwa ambao tumemfahamu kwa muda mrefu ni vigumu kutaja hata kimoja cha kukukumbukwa alichokifanyia taifa hili kama kiongozi kwenye serikali. Na huko UN na OAU mmh ! Halafu umri nao unakwenda, anahitaji kupumzika !
  Bahati zuri hao ulowataja wote nimewalinganisha na Lowassa lakini sikubahatika kuona uafadhali wao.
  Hakuna popote niliposema Lowassa anataka kuwa Raisi. Hiyo pointi ya pili nineshindwa kuielewa na hiyo ya tatu ya Lowassa kunipa bei gani ili nimpigie debe nakuachia uamue mwenyewe.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Raisi ajaye wa Jamhuri ya Tanzania atachaguliwa kwa kura awe anatoka bara au visiwani, hayo ya Maalim Seif ni yake ! Dr. Salim Ahmed Salim, mwaka 2015 umri wake utakuwa umefikia miaka 74 anahitaji kupumzika !
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,601
  Trophy Points: 280
  Mag3, asante kwa thread hii, umefunga kila kona mpaka wale wenye chuki na Lowassa hawana pa kutokea!.

  Yote iliyoyasema ni kweli isipokuwa sio kweli kuwa CCM woote ni mijizi au CCM woote ni mafisadi, wako wana CCM safi wa Nyerere type ambao wametapakaa vijijini wakiishi kwa taabu ndani ya lindi la umasikini uliotopea ambao sio wezi wala sio mafisadi, ila kwa vile sifa kuu ya kuwa kiongozi wa CCM ni ufisadi, hao CCM wasafi hawawezi hata kufikirika kwenye uongozi hata wa shina tuu let alone wa taifa!.

  Hata mimi katika utetezi wangu kwa Lowassa, nakiri Lowassa ni fisadi tena ni fisadi mkubwa tuu, ila Lowassa ni fisadi mwenye uwezo to do something worthwhile kwa Watanzania kuliko hao mafisadi wengine ambao ni wapuliza vuvuzela kwa kelele nyingi za vita dhidi ya ufisadi huku ni mijitu milafi tuu yenye uroho wa madaraka huku in actual fact haiwezi kufanya chochote kwa taifa hili!.

  Ukichagua nguruwe Nguruwe, chagua aliyenona, CCM ni chana cha mafisadi, kati ya mafisadi hao, fisadi mwenye afadhali ndio Lowassa peke yake!.

  Lowassa for CCM 2015!.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mag3,
  Hebu tuangalie nje ya sanduku. Si lazima rais mpya atoke CCM 2015. Natamani sana kukizika hiki chama cha CCM ambacho kimesaliti misingi aliyotuwekea Mwalimu Nyerere.
   
 17. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  Kama umenisoma vizuri Raisi kutoka CCM is the last thing I'd ever wish for and God Forbid it ! Najaribu sana kuangalia nje ya sanduku na kama ningekuwa na uwezo, hata hiyo 2015 ni mbali sana CCM kubaki madarakani kwa sababu madhara yake ni makubwa na yanaongezeka kila leo. Lakini kulingana na mentality ya Watanzania wengi ambao bado wanaamini hii CCM bado ni ile ile ya Mwalimu, sitaona ajabu akichaguliwa Raisi kutoka CCM labda tuwe na katiba mpya. Ndiyo maana nasema kuwa kama itabidi Raisi atoke CCM, Lowassa ni afadhali mara mia kuliko yeyote ndani ya CCM kwa sasa. Hebu fikiria kuna mtu hapo juu anawataja kina Nnauye, Membe na Mukama, duh !...what's wrong with us people ?
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Dec 27, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hivi Lowassa kafanya nini la maana?.. ebu nipeni list ya mazuri aloyafanya akiwa sijui waziri mkuu ama kabla ya hapo?.. Shule za kata au huo muafaka wa MoU maana sioni zuri..
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hahahha Mag3 kwa kweli unachekesha . Umewalinganisha na Lowasa kwa vigezo gani. Siwezi kukataa maana inawezekana wewe una priority zako amabaz hata hazingaalii miiko na maadili ya uongozi. Ebu nipe vigezo hivyo vya kumfany Lowasa katika mamlioni ya wanachama wa CCM awe na nafuu au awe ana compteteive advantage kwa CCM na Kwa taifa

  Naanza
  • Mchapakazi teh teh teh
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ohhh kwani Nnnauye membe mukama wa ana tatizo gani ukimligaisha na Lowasa as far leadrship is concerned. kumbe watu wengine tunaamni tunataka mabadiliko lakin tup tayari kurudi nyuma. Sijui una umri gani mpaka ushindwe kuona reformed , real CCM ya wananchi without the likes of Lowasa is possble .Kuna watu wenye nafuu na wana uwezo.
   
Loading...