FOX21
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 425
- 781
Ndugu zangu mnaoishi Musoma kwanza niwape pongezi kwa jinsi mnavyo pambana kupata mkate wenu wa kila siku.
Mkoa huu wa MARA japo una wakazi wengi wenye elimu ya sekondari na kuendelea ila nahuzunika kusema kundi kubwa la vijana wanahangaika mitaani kwa kukoswa ajira za kueleweka na kujikuta wanaishi kwenye mazingira magumu na hii inapelekea wengine kujihusisha na matukio ya kiuhalifu, kama kupora mali za watu na unyang'anyi.
Kwa hali kama hii ninapenda kuiomba serikali kulitizama kwa umakini sana ili kuiokoa jamii na matukio yasiofaa kama ubakaji na unyang'anyi. Maana tutaanza kusikia kuna makundi ya kihalifu kama miaka ya nyuma vijana walipokua na magenge ya uhalifu.
Ifikapo mida ya saa mbili za usiku, bado ni mapema sana ila huu muda usishangae kukutana na uporaji wa kutumia nguvu katika baadhi ya maeneo kama, Nyabange, Bweri, Majengo(songe), Baruti, Nyakato, Nyasho, nk. Inatakiwa jeshi la polisi liweke juhudi kutokomeza tabia za namna hii kwa Nguvu zote ili kuilinda heshima ya mkoa wa Mara. Naamini samaki hukujwa angali mbichi.
Nimefurahia ziara ya mkoani, japo maisha ya walio wengi ni changamoto.