Ndio maana Wanagongwa!!

anacho anacho kitafuta,ameshindwa kuandika namba!!!
 
hapo unarudi nyuma kwa ghafla ...afu akianguka chini unaanza kumfuata spidi...kudadadeki...!!!
 
Hawa ndio polisi wetu na harakati za kusaka noti kwa ajiri ya sikukuu ya pasaka

[MENTION]paloma[/MENTION] angalia vijana wako
 
Hawa jamaa huwa wanajituma kumbe nyuma ya pazia mkwanja wao
Wana mpaka vitabu feki vya faini!
 
Huyu naona alipigwa mkono akagoma kusimama. Jamaa akaamua liwalo na liwe akadandi hako ka rava foo.

Inanikumbusha yule traffic aliyempiga mkono jamaa pale ubungo. Jamaa akapiga gia kutambaa. Traffic naye kwa ubishi akadandia nyuma ya ile gari (pickup). Duh! Jamaa kapiga simu home waache geti wazi. Kapiga gia hadi Makongo juu, kazama naye traffic hadi kunyumba. Bahati yake traffic alikuwa na redio akawapigia wazee wa kazi wakatia timu, bila hivyo ingekuwa balaa.

Wazee wa kazi kuja, mtuhumiwa karuka ukuta kalala mbele. Jamaa wakasomba kila waliyemkuta mule wakatambaa nao. Sijui iliishaje ile maneno.
 
Mkuu mkeshaji hiyo nayo kali kupindukia.
 
Hawa jamaa ni watu wa ajabu sana. Kuna siku nilishuhudia trafiki akikimbilia barabarani pale Tabata Shule, Dar es Salaam, kulazimisha gari lisimame. Kama dereva asingepiga breki za dharura trafiki huyo angekuwa marehemu sasa.
 
Samahani nilitoka kidogo nilikuwa napata lunch na supu ya pweza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…