Ndio kuachwa huku au?

bryleen

Member
Jul 28, 2011
90
24
Natumai wote mko pouwa wapendwa wana jf!nisameheni kwa kutoonekana maeneo haya siku nyingi ila mungu ni mwema nimerudi tena,hapa simuongelei mtu wala kuigiza ila hii na yangu mwenyewe imenitokea na inaendelea mpaka sasa please naombeni ushauri wenu wandugu na naomba matusi na kashfa zipunguzwe katika majibu yenu nawaomba sana.
nipo kwenye mahusiano tangu mwezi wa 6 mwishoni baada ya kukaa muda mrefu bila mtu,mungu ni mwema kweli huyu shemeji yenu mpya alinipenda na kunijali ingawa kazi yake ni kuwa busy karibu wiki nzima kasoro j2 tu ndipo anakuwa free na alijitahidi sana kuwa nami na kuspend siku hiyo nzima ya j2 kwenda sehemu mbalimbali na mm ili hata tupumzike na kubadilishana mawazo mbalimbali,haikuishia hapo pia alijitahidi muda wa kazi kunipigia simu muda mwingi kunijuza anapoenda kwaa muda huo hata na mengineyo hope mnajua penzi la kwanzakwanza linavyokuwaga tamu na motomoto ila nasikitika kuwaambia kuwa mwezi wa nane nilipata taarifa za babayangu kupata ajali ikanipasa niende nyumbani mara moja kumcheki baba then baada ya wiki moja nilirudi kuendelea na kazi lakini kwa bahati mbaya tena baada ya kama wiki mbili nilipata tena taarifa baba yangu mkubwa kaanguka ghaflana kufariki hivyo nilienda tena nyumbani na baada ya wiki 2 nilirudi kazini na hapo ndipo nilipoanza kuona tofauti za huyu shemeji yenu kwani inaweza kupita hata siku nzima asinipigie wala kutuma meseji na kila ninapomuuliza anasema anakuwaga busy muda mwingi au huwa anakuwa na bosi wake kama binadamu kuna kummiss mpenzi wako so nimejaribu kumuomba hata tutoke tuongee nijue nn shida anakuwa na visingizio jamani na kwa bahati nzuri tupo wote katika jengo moja, tatizo simuelewi maana anaweza akanitumia meseji nzuri ya kimapenzi au hata akiniona nimesimama na mkaka yoyote atapiga simu na kuonyesha alivyo na wivu juu yangu.nahitaji ushauri wenu ni kwamba amenichoka ama vipi maana hakuna tena mawasiliano kama yale ya awali wala ukaribu kihivyo na naumia maana ni muda mfupi sana wa mahusianao ila kabadilika ambapo nakuwa njia panda sijui kama nimeachwa ila ana wivu wa kawaida kwangu au bado ananipeda.NIFANYEJE
 

Jestina

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
4,831
1,700
atakuwa mguu mmoja nje,mguu moja ndani labda kasikia habari mbaya kuhusu wewe hivyo anakupima,jifanye hauko interested naye tena endelea na mambo yako kama bado anakutaka atakuja na speed kama hakutaki naye atauchuna tu wewe tena itabidi uanze kutafuta mwingine....life goes on...
 

the grate

JF-Expert Member
Sep 24, 2011
204
36
pole mwaya kwa yaliyokusibu.me nahisi huyo mwenzio hayuko stable katika maamuzi yake hana uhakika na hisia zake. Mwambie kwamba unataka jibu la kueleweka..u hv 2kic many frogs b4 meeting the right one
 

bryleen

Member
Jul 28, 2011
90
24
thanx much na ndicho nachofanya saivi ni kupishana koridoni kama hatujuani ingawa ni kama inamuuma coz kama anatamani hata anisimamishe aongee na mimi afu mungu ni mwema mi ni mtu wa kujichanganya so m always happy nadhani kama mungu kanipangia huyo its okey bt kama sivyo pia nitamshukuru mungu.
 

JICHO LA 3

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
356
62
POLE MWAYA...pengine presha yako kwa vile uhusiano bado mpya,
labda na yeye anakusoma msimamo wako katka mapenzi yenu kama unampenda au la!
mimwenyewe ishawahi kunitokea jamaa alikuwa bize sana na mimi thn mi nikawa kawaida tu, akaanza kupunguza mawasiliano trtb ikabidi mie tena ndo nianze kuwa bize nae..baadae tukawa sawa wote nauliza why mwenzangu mawasiliano siku hizi jibu nilikuwa nakupima kama upo interest na mimi hiyo ni kawaida.au kuna mtu anamzingua ndo mana yuko hivo ukipata nafasi ongea nae muulize kwa undani na umwambie awe muwazi kwako naamini utapata ufumbuzi toka kwake.
kwa sababu uhusiano mpya ni mgumu sana asikuambie mtu wote mpo katika kuchunguzana.
 

Laigwanan76

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
547
146
pole mwaya kwa yaliyokusibu.me nahisi huyo mwenzio hayuko stable katika maamuzi yake hana uhakika na hisia zake. Mwambie kwamba unataka jibu la kueleweka..u hv 2kic many frogs b4 meeting the right one

Pole sana ndio hivyo ingawa wanasema wanaume ni kama watoto lakini kuna wengine watoto kweli......haingii akilini mtu akubadilikie ghafla tu,kama ana tatizo si anasema........kwa mimi hiyo ni kengele ya hatari,mtu wa aina hiyo ni kazi sana kuwa nae kwenye mahusiano utakuwa na presha bure......kama vp mpe ukweli wake.....vinginevyo mpotezee atakukondesha
 

bryleen

Member
Jul 28, 2011
90
24
asante mamii na mi kuna muda nakkaa nafikiria hayo na ndio maana sijawahi mwambia tuachana wal nn bado nina nafasi ya kujua ukweli tutakapokaa na kuongea.asante sana mpendwa
 

shalis

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
270
64
ndugu the same story kama mimi..ila wakwangu(x) alikuwa na mwingine so akashidwa kubalance hesabu 1+1=11 so watch carerfull kumpima mtu ndo kuuchuna na kama yeye ni mwanaume kweli akiwa kama mesikia jambo baya kwanin msikae chini mkayazungumze ... baby watch caref imenitokea mim last week nami nilikuwa na miezi michache tu kama yako in tht relation,
nimeachana ...kazi kwako biashara asubuhi mahesabu ndio jion usichanganye mboga ....
 

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
uvumilivu pays much
jichunguze kama kuna sehemu umeenda tofauti na yeye
jaribu kumtumia sms za kimahusiano nyingi kadri unavyoweza
jitahidi kutoa pole ya kazi kila wakati hasa majira ya jioni
ingia gharama ya kumpigia simu mara kwa mara
usikubali kupishana naye pasipo kumjulia hali
usiwe na tabia ya kumkimbia kama unavyofanya sasa
lakiniyote haya yafanye kwa kipindi cha muda maalum
then fanya tathmini na kisha uamue kama hakuna badiliko
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,444
2,479
tatizo wanawake mna kawaida ya kukariri hasa kupigiwa simu emails nk, kwani usipopigiwa simu siku nziam hupendwi? je kama simu kungekuwa hakuna?
nakumbuka hata girlfriend wangu alikuwa hivo visa vingi hujapiga simu asb mara sijampa ua nk.cha muhimu mnapokaa wekend kama anaongelea future yenu pamoja na mikakati alishaionyesha ya wote kuishi pamoja huna haja ya kuanza kuyumba yumba kimawazo
mshirikishe ma mungu pia kwani sisi tunaona tu kwa macho lkn yeye huona yaliyofichika, penzi usinganganie mpe muda kama ni wake utakuwa wake tu..simu sio hoja hata kama akikaa wiki so long anakupenda.
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,904
Pole sana mkuu,hizi relation zina matatizo sana ila kwa vile huna uhakika na hisia zako jitahidi kuwa positive zaidi kuhusu yeye na wewe pia,jipe mda wa kujua ukweli kuhusu yeye na msimamo wake ili usiishi kwa hisia na kuutesa moyo wako, hapo ndio utaweza kujua uchukue uamuzi gani,all in all tunatakiwa tujifunze kupokea matukio kwani sio kila tukio ni baya, coz huwezi jua japo unahis utaumia sana au utaathirika sana akikuacha kumbe inaweza kuwa faida kubwa kwako na kwa maisha yako pia,amini kama sio yeye basi atakuja mwingine kama alivyokuja yeye na siku moja utakutana na aliyeumbwa kwa ajili yako!
 

Rose1980

JF-Expert Member
May 10, 2010
5,685
1,284
cantalisia umeongea vyema
vp faza ajambo?isabela?


MDADA APO KIMBIA...dzain jamaa yupo kwenye dilema ...ana demu mwngne vp ajui abase wap....mwambie akupe TAMKO MOJA...neno moja tu na roho yako itatulia...
 

Cantalisia

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
5,222
2,904
cantalisia umeongea vyema
vp faza ajambo?isabela?


MDADA APO KIMBIA...dzain jamaa yupo kwenye dilema ...ana demu mwngne vp ajui abase wap....mwambie akupe TAMKO MOJA...neno moja tu na roho yako itatulia...
Asante Rose,father filipe hajambo,nasikia isabela ana mpango wa kunichukulia salvado wangu!
 

bulldoza

Senior Member
Sep 28, 2011
133
42
Talk 2 him ask him what he wants you 2do…shud I stay..or shud I go…don't decide on your own..
 

Mocrana

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
536
122
my dia nimeguswa mana namm nilishapita kwenye hiyo hali, usiumize kichwa hana msimamo huyo, najua itakuwa ngumu kumtoa akilini lakini jitahidi, kuwa busy na mambo yako tena hata usihangaike hata kumpigia cm wala kumtafuta, then jaribu kupractise kitu kinaitwa circular dating kama kuna mwanaume anakupenda au unamarafiki wa kiume wa go out on date and have fun but dont sleep with any of them just dating, for more ushauri jaribu kusearch rori raye kwa google kama itasumbua my no 0714666221
 

Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,386
7,229
my dia po;e sana jaribu kukaa na mwenzia umweleze mabadiliko unayoyaona na umuulize tatizo nini maana haya mambo yanahitaji mazungumzo yenu ninyi wawili,pole sana nad try that
 

Nsabhi

JF-Expert Member
Feb 23, 2011
1,093
162
Tatizo lako unaonyesha kumpenda kuliko yeye. .." there is a danger in loving some too much" jaribu kuuchuna ili naye ukatafute wewe.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom