Elections 2010 Ndg. Jamal Abdallah TAMIMU wa Muhambwe: Elimu Darasa la Saba. Ni Rushwa?

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Huyu sijui TAKUKURU wamemkosaje? Alikuwa anatoa rushwa waziwazi.

Shughuli zake hazieleweki vizuri na kuna malalamiko mengi dhidi yake toka kwa wananchi juu ya Ujambazi.

Hivi Millenium hii ya pili bado viongozi wasio na Elimu wala maadili wana nafasi???

CCM safisheni aibu kama hizi!! Wapiga kura tunaona na tutaamua
 
Kwa kigezo cha Elimu nimeona wapo wengi wenye Elimu ya msingi akiwemo LAMECK wa ROrya tena kuna wadau wanasema jamaa aliishia la 4 tu akiingia kwenye mishe mishe zake!! ccm imechafuka haswa hakuna msafi ndani ndo mana wameamua kufunika kombe.....
 
Huyu sijui TAKUKURU wamemkosaje? Alikuwa anatoa rushwa waziwazi.

Shughuli zake hazieleweki vizuri na kuna malalamiko mengi dhidi yake toka kwa wananchi juu ya Ujambazi.

Hivi Millenium hii ya pili bado viongozi wasio na Elimu wala maadili wana nafasi???

CCM safisheni aibu kama hizi!! Wapiga kura tunaona na tutaamua
Kwenye elimu yupo pia Jah People kule Njombe na yeye siku zote amekuwa akijisifu ni darasa la saba tena lile la juu. Lakini kwenye Ujambazi nadhani unahitajika uthibitisho ni tuhuma nzito saana hizo!
 
KWA WALIOPO CHADEMA..........MUULIZENI WAZIRI WA ZAMANI ALIYESHINDWA NA HUYU BWANA ATAWAAMBIA YOTE(kuhusu ujambazi na utekaji akishirikiana na wakimbizi).........! ILA HAITAKUWA GIA YA KUMSHINDA KWANI CCM HUKU HAINA MPINZANI......!
 
nadhani kwa elimu ya msingi RUKWA wameongooza ...sina tatizo nao anyway ingawa kwa karne hii?????anyway anyway
nadhani kwenye hii list kuna wauza madawa ya kulevya (madai sina uthibitisho), mafisadii, walaghai, wazinzi (wanaoambukiza watu VVU kwa makusudi -madai tu sina uthibitisho) na waporaji...yote haya ni sawa tu au ujambazi ni extreme case???
mix with yours
 
hongereni kwa kumtoa selelii.... pia hoja yenu ya uraia imewasaidia sana, well done
 
Nchi imeangamizwa na wasomi, nikianzia na Dr Balali, Dr Andrew,Chenge, Dr Kikwete, Prof Kapuya, Dr Kamala, Dr Nchimbi wale wanasheria wa IMMA nadhani wananchi wanajaribu turufu na wale wasio na elimu! Tanzania bila elimu inawezekana. Nimewapenda hawa kuwa kweli kuliko yule Chitalilo, Dr Mzindakaya, Dr Nagu, Dr Mathayo David
 
Kuna mmoja yule wa Mbeya Vijijini elimu yake wameandika" ANAJIENDELEZA" sijui ndio kisomo chenye manufaa? Chadema wakijipanga vizuri lakini wasiwe OVERCONFIDENT wanaweza kulitwaa hili jimbo.
 
Nchi imeangamizwa na wasomi, nikianzia na Dr Balali, Dr Andrew,Chenge, Dr Kikwete, Prof Kapuya, Dr Kamala, Dr Nchimbi wale wanasheria wa IMMA nadhani wananchi wanajaribu turufu na wale wasio na elimu! Tanzania bila elimu inawezekana. Nimewapenda hawa kuwa kweli kuliko yule Chitalilo, Dr Mzindakaya, Dr Nagu, Dr Mathayo David

Kwa hiyo itakombolewa na wa darasa la saba?
 
KWA WALIOPO CHADEMA..........MUULIZENI WAZIRI WA ZAMANI ALIYESHINDWA NA HUYU BWANA ATAWAAMBIA YOTE(kuhusu ujambazi na utekaji akishirikiana na wakimbizi).........! ILA HAITAKUWA GIA YA KUMSHINDA KWANI CCM HUKU HAINA MPINZANI......!

Kwa maana hiyo maadili na elimu si hoja, hongo ndio kigezo cha kiongozi mzuri!

Jamani hapa CCM imeporomoka kabisa, yaani walau wangeweka minimum level Elimu ya Sekondari.

Tutapiga kampeni kali za kuhakikisha huyu Jamal wa Std. 7 hatuwakilishi bungeni.
 
Kwa hiyo itakombolewa na wa darasa la saba?

Mkuu hujanisoma wasomi wetu wanasiasa hawana tofauti na darasa la saba waliowengi! Richmond haikusainiwa na Ngumbalu, Deep green hawakuwa darasa la nne! Mikataba ya kilevi ya madini ni wasomi wetu! wala rushwa na drugs dealers ni wasomi
common hebu waacheni hao wakweli wa elimu ndogo wafanye mambo afterall ubunge hausomewi
 
Mkuu hujanisoma wasomi wetu wanasiasa hawana tofauti na darasa la saba waliowengi! Richmond haikusainiwa na Ngumbalu, Deep green hawakuwa darasa la nne! Mikataba ya kilezi ya madini ni wasomi wetu! wala rushwa na drugs dealers ni wasomi
common hebu waacheni hao wakweli wa elimu ndogo wafanye mambo afterall ubunge hausomewi

Mkuu nimekupata

Nadhani hata hivyo ni muhimu hata kujali maadili yao kama wana sifa mbaya au utajiri usiojulikana umepatikanaje. Au ndo tunauza nchi hivyo? Well labda mie sioni mbali.
 
kati ya waliogombea jimboni MUHAMBWE ni yupi ambaye angekuwa right candidate ukiacha suala la rushwa( TOA USHABIKI)
 
Huyu sijui TAKUKURU wamemkosaje? Alikuwa anatoa rushwa waziwazi.

Shughuli zake hazieleweki vizuri na kuna malalamiko mengi dhidi yake toka kwa wananchi juu ya Ujambazi.

Hivi Millenium hii ya pili bado viongozi wasio na Elimu wala maadili wana nafasi???

CCM safisheni aibu kama hizi!! Wapiga kura tunaona na tutaamua

Kigezo cha elimu inaweza isiwe kikwazo kwa huyu bwana lakini biashara zake zinatia mashaka. Ni mfadhili wa siku nying wa CCM pale Kibondo nakumbuka wakati wa kampeni za mwaka 2000, CCM waliandaa chakula cha mchana nyumbani kwa huyu jamaa na Mkapa akashauriwa kutokula mahali hapo kutokana na huyu jamaa kuhusishwa na kashfa ya DC kumbaka mzungu nyumbania kwake mwaka mmoja kabla.
 
Naona hii story ya RaiaMwema la wiki hii inamhusu huyu bwana:

CCM yapitisha aliyetajwa kuuza viungo vya Albino

Mwandishi Wetu​
Agosti 18, 2010

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM) iliyokutana Dodoma kuchuja na kupitisha majina ya wagombea wake wa ubunge, imepitisha jina la mgombea ubunge aliyewahi kupigiwa kura na wanakijiji akitajwa ni muuaji na mnunuzi wa viungo vya maalbino, Raia Mwema imebaini.

Mgombea huyo (jina linahifadhiwa) ambaye sasa atakuwa ameweka rekodi ya kushinda kura ya maoni CCM pamoja na kura ya maoni ya mauaji ya maalbino iliyowahi kuendeshwa na Serikali, ni kutoka katika jimbo moja (jina linahifadhiwa) mkoani Kigoma.
Gazeti hili limefanya uchunguzi na kuwasiliana na vyombo vya usalama, na kuthibitishiwa na baadhi ya wakazi jimboni humo ambako mgombea husika ameteuliwa kugombea ubunge. Taarifa tulizo nazo zinaelekea kumshutumu mteule huyo wa CCM kwa makosa kadhaa ya jinai, na mshangao ni wa jumla kuhusu uteuzi wa mtu anayeonekana hafai kwa kigezo chochote isipokuwa matumizi ya fedha na ufadhili wake kwa wakuu wa chama.

SOURCE: RaiaMwema Toleo 147
 
Back
Top Bottom