Ndesamburo: Nitalirudisha Soko la Kiborloni

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,445
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chedema), amewahakikishia wakazi wa Kata ya Kiborloni kuwa atalirejesha soko lao la nguo na viatu vya mitumba lililohamishwa mwaka 2007.

Soko hilo maarufu kwa wakazi wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha lilihamishwa Kata ya Kiborloni na kupelekwa eneo la Memorial Kata ya Karanga na kusababisha usumbufu kwa wafanyabiashara.

Akihutubia mkutano wa hadhara sokoni hapo jana wakati wa kumnadi mgombea udiwani wa kata hiyo, Frank Kagoma, mbunge huyo alisisitiza kuwa litarudi.
Ndesamburo maarufu kama ‘Ndesa pesa' ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, alisema alikuwa na ugomvi na Mkurugenzi aliyestaafu wa Manispaa ya Moshi, Bernadeta Kinabo, kuhusu suala hilo.

"Naapa kwamba Soko la Kiborloni lazima lirudi hapa. Piga ua, mvua inyeshe ama jua liwake lazima soko litarudi na mtaendelea kufanya biashara zenu kama kawaida."

Aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua mgombea wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Februari 9, akisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa balaa.

"Ndugu zangu CCM imekuwa balaa, achaneni nayo, inataka kuwarudisha kwenye vumbi wakati sisi tumekuwa tukiwapigania ili mpate barabara za lami.
"Najua mmekwishaamua diwani wenu awe huyu Kagoma, sasa hakikisheni Jumapili mnajitokeza kwa wingi kupiga kura na mzilinde, kisha baadaye tutasherehekea pamoja," alisema Ndesamburo.

Kwa upande wake Kagoma aliwaomba wananchi kupuuza propaganda chafu za CCM kwamba si Mtanzania, akisema hata wakimfunga sasa atashinda akiwa gerezani.

Uchaguzi katika kata hiyo unafanyika baada ya aliyekuwa Diwani wake, Vincent Rimoi (CHADEMA) kufariki dunia mwaka jana.
 
Asante mleta mada,kwa pale Kiborloni hakuna ubishi,ushindi ni misa ya kwanza..Viva Chadema!!!
 
Ndesaburo anaota.
 
Toka 2007 diwani na mbunge wake wamekua wakiapa kuleta maji,kurudisha soko na kukarabati soko la vyakula ambalo kila siku linazidi kushuka kiwango.huu ni utapeli wa Ndesa kwa watu wa kiboriloni.hakuna cha maana amewafanyia zaidi ya kuwafanya punda vijana wa kiboriloni.
 
Kati ya watu waliochoka ndani ya CDM ni huyu mzee, anapaswa apumzike.
 
Mkuu Ndesa kwa moshi kweli anapendwa coz ni mzawa na pia amewekeza moshi ila hakuna chochote alichofanya kwa moshi zaidi ya kujiwekea Lami hadi kwake majirani wanateseka shida ya maji kabla ya 2009 alikua ameweka bomba la maji kuwasaidia wananchi wa mtaani kwake.Wanawakiboriloni wanaumia sana.
 
misa ya kwanza? na kwa waislamu tusemeje?

Ndio maana nasema akili zenu kama za nepi,kura huwa zinapigwa siku gani wewe gamba?Akili zenu ni majanga hatuwashangai kwa udini wenu mnamsupport mwenyekiti wenu.
 
MBONA ILO SOKO LIKO ENEO ZURI SANA SASA HIVI(MEMORIAL). SEHEMU YENYE UWAZI, SASA HIVI ENEO LA Kiborloni NI DOGO SANA HALIWEZI KUACCOMODATE WAFANYABIASHARA
 
Kipindi nasoma Moshi Technical School - hili soko lilikuwa linatusaidia sana kupata mahitaji yetu madogo madogo siku za jmosi hasa sisi wanafunzi tuliokuwa tumetoka familia za hali ya chini. Naunga mkono lirudishwe
 
mkuu fuso Unamaliza lini hapa m . tech ulimuacha mapande?
 
anaitwa Mwalimu Mpande!! Mwalimu wa VIJANA yule namkumbuka kwa zile fimbo Super SIX, hasa akikukamata hujakimbia mchaka-mchaka.

Kuna siku nilipigwa Super SIX kisa eti niligoma kuchukua kadi za umoja wa vijana wa CCM, sijui alizitoa wapi kuja kutugawia kwa nguvu.

Mimi ni mkongwe - ni zile enzi za Malale (RIP) na Munuo teacher wa nidhamu.
 
MBONA ILO SOKO LIKO ENEO ZURI SANA SASA HIVI(MEMORIAL). SEHEMU YENYE UWAZI, SASA HIVI ENEO LA Kiborloni NI DOGO SANA HALIWEZI KUACCOMODATE WAFANYABIASHARA
Mkuu watu wakiboriloni tunasema hatulitaki kwani kwa sasa kiboriloni imekua poa sana sehemu nzuri ya makazi,pili kiboriloni hakukua na soko bali wauza mitumba walikua wanajibanza kwenye baraza za nyumba za watu na kwenye vichochoro.Tunalo soko la vyakula kama alikua na nia nzuri waliboreshe soko la vyakula na kuleta maji ambayo ni tatizo kubwa ameshidwa kulitatua toka amekua mbunge.
 
kila mwaka hiyo ndio gear ya ndesamburo ya kupatia kura moshi hususan kiborloni. hana jipya huyo. soko hilo lipo eneo zuri sana la memorial sasa yeye kama amekosa agenda, alale
 
miaka 15 ya ubunge wa ndesamburo moshi mjini ameishia kujenga uzio wa makaburi, hakuna la maana alilofanya
 
Miaka yote ya ubunge wake kashindwa kulirudisha leo tena analeta ulaghai.
mkuu, mimi nimekaa moshi miaka 8, ndesamburo amejulia sana watu wa moshi, amekaa katika ubunge miaka 15 hajafanya kitu cha maana, amebaki kutafuata viajenda vya kilaghai laghai kama hiki cha kuhamisha soko.
 
Ndesa uje pia huku Usangi diwani mteule akisha apishwa,wana wa Usangi tunakuhitaji sana.
 
Back
Top Bottom