Ng'wamapalala
JF-Expert Member
- Jun 9, 2011
- 6,811
- 6,507
mkuu shughulisha ubongo wako kidogo kujaribu kuelewa mantiki nzima ya maoni ya Mh Ndesamburo alipokuwa anajumuisha hoja yake hiyo ili uwafahamishe na wenzako. Changamoto zilizopo kwenye jamii yetu ni nyingi sana ( kiuchumi, kijamii na kisiasa) je zina impact gani ndani ya Bunge?, Je zina impact kwenye usalama wa taifa? nini kufanyike ili kuzikabiri?. Je athari zake ni zipi kama hizi changamoto hazitakuwa addressed kwa wakati muafaka? nani wa kufanya jukumu hilo?
Sasa mtu anayeogopa challenges zinazomkabili atafikiria kuzuia bunge lisirushe matangazo live ili wananchi wasijue kinachoendlea akisahau kwamba habari sasa hivi zinawafikia watu wa njia nyingi mno, atazuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani ili wasitoe mrejesho wa udhaifu wa serikali yetu bungeni; atafikiria kutumia vyombo vya dola kudhoofisha vyama vya upinzani; atafikiria hata kupindisha kanuni za bunge ili hoja inayoikaba serikali toka kwa upinzani isipite na mambo kama hayo!
Sasa mtu huyu ni hatari zaidi ya zile ngumi alizosema mzee Ndesa!!
Hiki ulichoandika hapa ni maneno mengi yasiyobeba uzito wowote wa hoja iliyo mezani.
Hiki alichokisema Mzee Ndasamburo ni kuharalisha uvunjifu wa sheria kwa watunga sheria achilia mbali utamaduni tuliojijengea katika jamii. Hii dhana ya kwamba kwa sababu bunge kwa sasa lina vijana basi ni ruhusa kurushiana ngumi ni kutojali utawala wa sheria ambazo wao ndiyo watungaji.
Kama kurusha ngumi kwa CHADEMA inakubalika ili kupata haki ndani ya bunge haina tofauti na mwananchi nje ya bunge kujichukulia sheria mkononi ili apate haki.
Kama kwa CHADEMA kukabiliana na changamoto kwa haraka na wepesi ndani na nje ya bunge ni kutumia mabavu mpaka kupigana wasije wakaanza kushangaa pale watu wanapoanza kukabiliana na changamoto mbali mbali kwa njia ya uvunjifu wa sheria ili haki ipatikane kwa haraka.
Kwa kauri yake hii, inaonyesha huyu Mzee ni bogus kabisa.
