Ndesamburo kugombea tena Moshi Mjini

Ndesamburo kugombea tena Moshi Mjini

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,485
Moshi,
MBUNGE wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), amesema ataendelea kutetea nafasi yake ya ubunge katika jimbo hilo endapo chama chake kitampitisha katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.


Ndesamburo alitoa kauli hiyo jana katika ufunguzi wa semina ya Baraza la Wanawake wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro (BAWACHA), ambapo alisema chama kisipompitisha yupo tayari kushirikiana na atakayechaguliwa ili jimbo hilo liendelee kubaki mikononi mwa Chadema.


Alisema kumekuwapo na taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na wapinzani wa Chadema kuwa endapo Ndesamburo hatatetea nafasi yake ya ubunge katika jimbo hilo basi litachukuliwa na CCM.


“Hii si kweli na kama sitagombea basi nitahakikisha linaendelea kuongozwa na Chadema, nitakuwa bega kwa bega na atakayechaguliwa kama chama changu kitanitupa pembeni.


“Uchaguzi ni chama, kama kitaniweka pembeni na kumteua mwingine basi nitamsaidia kwa nguvu zangu zote ikiwemo kutumia kiinua mgongo changu chote cha ubunge” alisema.


Ndesamburo ambaye mashabiki wake humwita Ndesapesa alisema Jimbo la Moshi Mjini ambalo linaongozwa na Chadema limekuwa likifanya vizuri hadi kufikia hatua ya kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kumsifu Meya wa Manispaa hiyo, Japhary Michael (Chadema), hivyo lazima liendelee kuongozwa na upinzani miaka mingine ijayo.


Akizungumza katika semina hiyo, Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhary Michael alimtoa hofu Ndesamburo kwa kumweleza kuwa hata akiamua kupumzika, jimbo haliwezi kupotea kwani wapo vijana wenye nguvu na uwezo wa kulitetea jimbo hilo liendelee kubaki Chadema kutokana na kazi ambazo zimekwishafanywa.


Chanzo: Mtanzania
 
Na kweli amekuwa mtu mzima sasa apumzike na abaki kuwa mshauri wa chama kama walivyofanya viongozi wengine wa chadema kama vile mzee Mtei,Bob Makani nk,na jimbo amwachie binti yake na ampigie debe ili aweze kupitishwa na chama chake kusudi aweze kuwa mgombea na aweze kuendeleza yale ambayo anadhani alikuwa hajayatimiza wakati akiwa mbunge,si vibaya mwana kumrithi baba ili mradi tu anapitia njia halali za kichama,huo ni mtazamo wangu tu.
 
Kingunge hadi sasa ni kamanda wa UVCCM huko kwenye chama chako na juzi Mwenyekiti wako aliendelea kumteua Bunge la Katiba kupitia taasisi ya waganga wa kienyeji

Kwahiyo Mnaiga ya CCM halafu mnajiita chama mbadala.
 
ndesa pesa hana mpinzani,na hana haja ya kupiga kampeni yeye akisimama siku ya kufunga na akaomba kura anapita
 
Na kweli amekuwa mtu mzima sasa apumzike na abaki kuwa mshauri wa chama kama walivyofanya viongozi wengine wa chadema kama vile mzee Mtei,Bob Makani nk,na jimbo amwachie binti yake na ampigie debe ili aweze kupitishwa na chama chake kusudi aweze kuwa mgombea na aweze kuendeleza yale ambayo anadhani alikuwa hajayatimiza wakati akiwa mbunge,si vibaya mwana kumrithi baba ili mradi tu anapitia njia halali za kichama,huo ni mtazamo wangu tu.
Mrema.jpg

2.jpg


Duh!
Kilimanjaro kuna vibabu havitaki kutoka, kuwaachia wana wao kazi!!!
 
Kwa kipimo kipi sasa?

Ben hata ushabiki sio hivyo yaani bado unamuunga mkono Ndesa aendelee kugombea ubunge??? Come on hili jimbo awaachie vijana tunauheshimu mchongo wake lakini sasa basi

jafari Michael he can
 
Back
Top Bottom