Ndesamburo atoboa siri ya utajiri wake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

MBUNGE wa Jimbo la Moshi mjini (Chadema), Philemon Ndesambro, amewataka wakazi wa Moshi kutoogopa kukopa fedha kwenye taasisi za fedha nchini kwa sababu, hata yeye amekuwa akikopa kuendesha biashara zake.

Siri hiyo ya Ndesamburo ambaye anamiliki vitega uchumi mbalimbali nchini, ikiwamo Hoteli za kitalii na Kampuni ya Utalii ya Keys miji ya Moshi na Dar es Salaam, alisema kinachotakiwa ni nidhamu katika urejeshaji mikopo hiyo.

Ndesamburo alitoa kauli hiyo juzi mjini Moshi, wakati akifungua mkutano wa tano wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos) cha Usharika wa Karanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini.
“Msiogope kukopa na baada ya kukopa lazima mkumbuke kurejesha mkopo kwa uaminifu…hii ndio siri ya utajiri na hata mimi ninatumia mikopo kufanya biashara zangu kwa mafanikio,” alisisitiza.

Mbunge huyo alitaka uongozi wa Saccos hiyo kuangalia uwezekano wa kuanzisha idara maalumu ya wataalamu wa masuala ya ujasiriamali, ambao watakuwa na wajibu wa kutoa mafunzo na ushauri kwa kila mkopaji.

Katika taarifa yake kwa mbunge huyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Humphrey Urassa, alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto ya kusaidia makundi maalumu, wakiwamo wajane, yatima na walemavu.

Urassa alisema kama wangepata ufadhili wa Sh10 milioni kutoka kwa mbunge huyo na wengine, wangeweza kukopesha makundi hayo maalumu kwa sababu hayana uwezo wa kununua hisa wala kuweka akiba.

Akijibu maombi hayo, Ndesamburo aliahidi kukisaidia chama hicho fedha, lakini akakataa kutaja kiwango zaidi aliwataka viongozi wa chama hicho kukutana naye ofisini kwake ili kukubaliana jinsi atakavyosaidia.
 
Back
Top Bottom