Kamanda acha uongo Basi, yaani unadanganya hata aibu huoniNdesa umetuacha Njia Panda, kwenye usiku wa giza nene.
Lala salama.
Jamani chadema leo mlitakiwa muiachie familia na wasemaji wa familia.bado tu mnapora ya kwenu ya kisiasa na mabendera si mlifanya jana? Leo ilitakiwa kisiweko chochote cha kichama ili watu wasiopenda chadema na viongozi wa vyama mbali mbali na serikali wawe free kuhudhuria.
Sijapenda hili la SELASINI kuendelea kuwa msemaji.wapishe wazee wa ukoo au ndugu wa ndesamburo leo ndio washike usukani wa shughuli yao.
Jana mlisema chama kinaaga sasa na leo mumo tu mnakera.Familia ya ndesamburo mumeipora madaraka yote
ndugu unapoona hali kama hiyo ujue kila kitu kimepangiliwa na sio matakwa ya chama. jaribu kuelewa pia sio kila kitu kitakwenda kama utakavyo wewe. ndio maana umeambiwa ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi!Jamani chadema leo mlitakiwa muiachie familia na wasemaji wa familia.bado tu mnapora ya kwenu ya kisiasa na mabendera si mlifanya jana? Leo ilitakiwa kisiweko chochote cha kichama ili watu wasiopenda chadema na viongozi wa vyama mbali mbali na serikali wawe free kuhudhuria.
Sijapenda hili la SELASINI kuendelea kuwa msemaji.wapishe wazee wa ukoo au ndugu wa ndesamburo leo ndio washike usukani wa shughuli yao.
Jana mlisema chama kinaaga sasa na leo mumo tu mnakera.Familia ya ndesamburo mumeipora madaraka yote
Usijali mkuu Lowassa yupoNdesa umetuacha Njia Panda, kwenye usiku wa giza nene.
Lala salama.
Hapa ndo mahala ninapoukubali msimamo wa imani ya kiislam. Kuagaaga Mara mbilimbili ni kumsumbua marehem.![]()
Wajukuu wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini Philimoni Ndesamburo,wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wake wakati wakilitoa nyumbani kwake Kiboroloni Kuelekea kanisani kwaajili ya Ibada ya Kumuaga.Picha na Diana Saria.
Kwa ufupi
Mwili wa Ndesamburo unaagwa kanisani leo kabla ya mazishi kufanyika nyumbani kwake baadaye mchana
Moshi. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo unaagwa kwa mara ya pili na wafuasi wa Chadema pamoja na wananchi ambao hawakupata nafasi ya kumuaga siku ya jana katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi, Joseph Selasini amewataka wananchi na watu wote waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Usharika wa Kiborloni kuacha kupiga picha mwili wa marehemu ili kutunza heshima yake.
Viongozi mbalimbali wameendelea kuwasili katika kanisa hilo wakiwemo viongozi wa Chadema na Mbunge wa Singinda Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu.
Awali wafuasi na wanachama wa Chadema walifurika nyumbani kwa Ndesamburo kwa ajili ya kuandamana kupelekwa mwili wake kanisani.
Mwili wa Ndesamburo umesaliwa nyumbani kwake kabla ya kupelekwa kanisani.
![]()
![]()
Chanzo: Mwananchi