figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,720
- 55,859

Wajukuu wa aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini Philimoni Ndesamburo,wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wake wakati wakilitoa nyumbani kwake Kiboroloni Kuelekea kanisani kwaajili ya Ibada ya Kumuaga.Picha na Diana Saria.
Kwa ufupi
Mwili wa Ndesamburo unaagwa kanisani leo kabla ya mazishi kufanyika nyumbani kwake baadaye mchana
Moshi. Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo unaagwa kwa mara ya pili na wafuasi wa Chadema pamoja na wananchi ambao hawakupata nafasi ya kumuaga siku ya jana katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi, Joseph Selasini amewataka wananchi na watu wote waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Usharika wa Kiborloni kuacha kupiga picha mwili wa marehemu ili kutunza heshima yake.
Viongozi mbalimbali wameendelea kuwasili katika kanisa hilo wakiwemo viongozi wa Chadema na Mbunge wa Singinda Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu.
Awali wafuasi na wanachama wa Chadema walifurika nyumbani kwa Ndesamburo kwa ajili ya kuandamana kupelekwa mwili wake kanisani.
Mwili wa Ndesamburo umesaliwa nyumbani kwake kabla ya kupelekwa kanisani.


Yanayojiri Moshi Kwenye Mazishi ya Mzee Ndesamburo
JUNE 6, 2017.

MOSHI, KILIMANJARO: Viongozi wa CHADEMA pamoja na wananchi wakiwasili katika Usharika wa Kiboriloni kwa ajili ya ibada ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Muda Mrefu wa Moshi Mjini na Muasisi wa chama marehemu Mzee Philemon Ndesamburo.

Maandalizi kanisani hapo.

Viongozi wa Chadema wakiwa wamejiandaa kuupokea mwili wa marehemu.

Kaburi ambamo atazikwa mzee Ndesamburo.










Mbunge wa zamani na mfanyabiashara maarufu kutoka Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo amezikwa leo June 6, 2017 nyumbani kwake KDC Moshi huku mazishi yake yakihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi mbalimbali.