Ndejembi amewataka watendaji wa Halmashauri kuwa wabunifu ukiwemo wa kutumia rasilimali ya takataka kuwa fursa ya kuzalisha nishati ya gesi

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,510
4,224
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh Deogratius Ndejembi amewataka watendaji wa Halmashauri kuwa wabunifu ukiwemo wa kutumia rasilimali ya takataka kuwa fursa ya kuzalisha nishati ya gesi na umeme hatua ambayo licha ya kusaidia kudumisha usafi itaongeza ajira na kuwarahisishia wananchi maisha.

Akizungumza baada ya kutembelea dampo la jiji la Arusha Mh Ndejembi amesema kwa sasa wakati umefika wa kutumia takataka ambazo zinapatikana kirahisi kila kona ya nchi kama rasilimali za kusaidia kurahisisha maisha ya kila siku na ni jambo linalowezekana na ambalo limekuwa likifanyika katika nchi mbalimbali.

Hata hivyo Naibu Waziri amewapongeza watendaji wa jiji la Arusha kwa kuanza mchakato wa kutumia takataka kuzalisha umeme na amewataka kuharakisha utekeezaji wake ili iwe mfano na chachu kwa halmashauri zingine.

Kwa upande wao wananchi wa jiji la Arusha wamesema mpango huo ni mzuri na wenye tija kama utatekelezwa kwa vitendo na kusimamiwa vizuri.

Je, huu ni mwanzo wa mageuzi katika sekta ya nishati?
 
Back
Top Bottom