Ndege za kuangusha mabomu za Marekani zapaa Korea

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,916
Ndege za kuangusha mabomu za Marekani zapaa Korea
_95862697_238c54de-2521-4222-8576-8adeffe2f1ae.jpg

Haki miliki ya pichaREUTERS

Ndege za kuangusha mabomu aina ya B-1B Lancer zikipaa juu ya Korea Kusini awali
Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.

Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.

Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.

Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.

Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.

Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.

Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya White House alisema baadaye kwamba mazingira kama hayo, yanayoweza kufanikisha mkutano wa Trump na Kim hayapo.

Korea Kaskazini imeongeza kasi katika majaribio yake ya makombora na silaha za nyuklia miaka ya karibuni licha ya marufuku ya Umoja wa Mataifa.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Han Song-ryol aliambia BBC awali kwamba Korea Kaskazini inaamini kwamba silaha zake za nyuklia zinaweza "kuilinda" dhidi ya tishio la shambulio la kijeshi kutoka kwa Marekani.

Korea Kaskazini inahofia kwamba Marekani na Korea Kusini wanaweza kutumia nguvu kumuondoa madarakani Kim Jong-un.

Jumatatu, Japan ilituma meli ya kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya kwanza ya aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata iliyowezesha taifa hilo kuanza kupanua uwezo wa jeshi lake.

Meli hiyo kubwa ya kubeba helikopta ambayo imepewa jina Izumo ilitumwa kuifuata meli ya kubeba mizigo na vifaa vya kijeshi ya Marekani ambayo inapitia katika maeneo ya bahari ya Japan.

Meli hiyo ya Marekani inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za taifa hilo zinalohudumu eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson na meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.

_95852246_c3120fd9-57ba-4706-9d38-3fff544d7eaf.jpg

Haki miliki ya picha

Image captionIzumo ndiyo meli kubwa zaidi ya kivita ya Japan
Korea Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.

Aidha, taifa hilo lilifanya jaribio la kurusha kombora ambalo lilifeli Jumapili, licha ya kuonywa mara kadha na Marekani na nchi jingine dhidi ya kufanya majaribio ya makombora au majaribio ya silaha za nyuklia.

Kutumwa kwa Izumo kumejiri baada ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na Japan na Marekani, pamoja na shughuli nyingine za majeshi ya majini.

Meli ya kutekeleza mashambulio baharini ya Ufaransa iliwasili kusini magharibi mwa Japan Jumamosi kwa mazoezi ambayo yatashirikisha majeshi ya majini ya Japan, Marekani na Uingereza.

_95853287_china_aircraft_carrier_624_swahili_v3.png

Image captionUkubwa wa meli za kivita za mataifa yenye nguvu
_95852248_aae413d6-8d25-4f1d-be39-e26441dc3072.jpg
Haki

miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli kubwa ya kubeba ndege ya Marekani ya Carl Vinson ikiwa kusini mwa Japan Jumamosi

Chanzo: BBC Swahili

My take;
hakika huyu bwana mdogo hawezi kupona. pamoja na trump kumsifia kote kule. kwamba ni mwelevu.
watu wanasema ogopa sana ukiona adui anakusifia.
 
Si azisogeze kwa mapanki.tuone vitu vikiinuka alafu viuiwe.fuate propaganda .za magharibi awapendi kuona nchi nyingine ikijiendesha yenyewe.nk miaka 27.wamewekewa vikwazo ila wanadunda.huyo ndio kidume sio kulialia tu.anaonyesha uhalisia wake kua marekani ata akimpiga ila ifahamike kua marekani ataki nchi iwe ina systems yake.marekani anata kudukua Habari zote azijue yeye
 
Thubutu! Mapanki hajaribiwi wala huwa hazungumzi! Utasikia NK wanazungumza wengine tu! Yeye Mapanki siyo mtu wa vyombo vya habari! Ni mtu wa amri tu! Marekani wanamjua vizuri kwa hiyo hawawezi kufanya kosa LA kuingia kwenye anga ya Korea kaskazini, vinginevyo ni kiyama kwa Korea ya kusini na marekani mwenyewe!
 
USA anamkwara ya mbwa koko ambaye anaishia kubweka tu na kuparua ardhi makucha lakn hawezi kukusigerea kukung'ata..

Kama USA anahisi anauwezo wa kumpiga n.k na yeye akabaki salama basi hizo ndege azirushe kwenye anga ya north Korea au ajitoe ufaham arushe kombora moja tu . hapo ndio ntaamini kuwa kweli USA na trump ni mwanaume
 
Acha unaz
 
Ukiangalia kwa karibu marekani hana mandate ya kuvamia nchi ingine passipo idhini ya UN. Itakua imetumia vibaya nguvu zake kijeshi na hata nchi washirika wanasita kwa sababu hiyo.

Pili kuna suala la malipo ya uharibifu wa kivita, anayekuwa wa kwanza kutupa risasi ama kombora ndio aliyeanzisha vita hivyo gharama zote za vita hiyo atazilipa hata kama kashindwa vita hiyo.
Hili la pili ndio marekani analikwepa anafanya mazoezi, pitisha ndege, meli ili jamaa apige iwe sababu.

North Korea akipiga kombora wa kwanza hata waashirika wa marekani wanapata sababu ya kushuriki kwa kigezo mshirika wao kashambuliwa.

Hivyo hii vita itaanza tu pale NK utatupa kombora lake. Kuanzisha vita kwa ridhaa ya security council haiwekani maana Urusi na China wanaveto.

Tusibiri kitakachojiri
 
Si azisogeze kwa mapanki.tuone vitu vikiinuka alafu viuiwe.fuate propaganda .za magharibi awapendi kuona nchi nyingine ikijiendesha yenyewe.nk miaka 27.wamewekewa vikwazo ila wanadunda.huyo ndio kidume sio kulialia tu.anaonyesha uhalisia wake kua marekani ata akimpiga ila ifahamike kua marekani ataki nchi iwe ina systems yake.marekani anata kudukua Habari zote azijue yeye
Popote pale lazima kuwe na kiongozi ,ndipo mambo huenda sawa. Uongozi huanzia katika level ya familia, hapo tunamkuta baba kama kichwa cha familia husika.Katika nchi tunakuta kuna Raisi kama Mkuu wake. Katika imani tuna Maaskofu, mashehe , mapadri nk kama viongozi. Katika level ya Dunia lazima awepo kiongozi (US) ambaye anawajibika Ku regulate power kwa baadhi ya nchi zinazokengeuka kwa ajili ya amani na usalama wa dunia, vinginevyo dunia itageuka kuwa uwanja wa fujo.
 
Kwa uongozi huu wa USA ....hapana bana.
 
Muda wa kulala kakojoe ulale
 
Kama USA ana ubavu si arushe kombora moja ili ajue kuwa MAHARAGE siyo mboga. USA anaanzisha chokochoko halafu anaanza kufyata mkia mwenyewe.
NK ni muziki mnene, siyo kama wanavyodhani wengine.
 
Si azisogeze kwa mapanki.tuone vitu vikiinuka alafu viuiwe.fuate propaganda .za magharibi awapendi kuona nchi nyingine ikijiendesha yenyewe.nk miaka 27.wamewekewa vikwazo ila wanadunda.huyo ndio kidume sio kulialia tu.anaonyesha uhalisia wake kua marekani ata akimpiga ila ifahamike kua marekani ataki nchi iwe ina systems yake.marekani anata kudukua Habari zote azijue yeye

Mkuu huu mwaka wa 16 bado wanapelekwa puta na Wateliban huko Afghanistani,leo hii ndiyo watake kuitambia Korea Kasikazini? Labda watumie mabom ya nuclear lakini na wao wakae wakijua watapata madhara makubwa sana sana ambayo hawajawahi kukumbana nayo katika historia yao ya kuvamia vamia mataifa mengine masikini, wakumbuke KK si kama Libya, Afghanistan, Iraq, Yugoslavia ya zamani na Syria - Wakifanya makosa ya kuivamia/piga mabom KK basi Korea Kusini na Japan watachakazwa kweli kweli.

Kitu kingine ambacho ni muhimu, Amerika inapaswa kukumbuka kwamba vita ikipamba moto Uchina na Urusi zitamsaidia Kim kwa hali na mali hawataruhusu Amerika/NATO kusogeza wanajeshi au kuikalia KK kwa nguvu - wataingia vitani liwalo liwe, sasa kama Amerika itahamua kufungua a pandora BOX sisi yetu macho - I hope Trump atakuwa wiser zaidi ata-stick kumaliza mgogoro huu kwa njia ya kidiplomasia.
 
Popote pale lazima kuwe na kiongozi ,ndipo mambo huenda sawa. Uongozi huanzia katika level ya familia, hapo tunamkuta baba kama kichwa cha familia husika.Katika nchi tunakuta kuna Raisi kama Mkuu wake. Katika imani tuna Maaskofu, mashehe , mapadri nk kama viongozi. Katika level ya Dunia lazima awepo kiongozi (US) ambaye anawajibika Ku regulate power kwa baadhi ya nchi zinazokengeuka kwa ajili ya amani na usalama wa dunia, vinginevyo dunia itageuka kuwa uwanja wa fujo.
Una akili sana
 
Back
Top Bottom