Ndege za Jeshi Dar

Ndege za Jeshi Dar

Si suala la ugeni bali kujua nini kinafanyika. Kama wana mazoezi wangetangaza kabla ili tujuwe, haya ya kushituana wakati mnajuwa tulishawahi lipukiwa kule mbagala na gongolamboto hayafai..
Utaratibu huo haupo Tanzania, nchi ya kibabe hii. Wanajeshi walijua masaa saba kabla kwamba mabomu ya gongo la mboto yangelipuka lakini wakahamisha familia zao bila kuwatangazia wananchi kuondoka maeneo ya karibu. Wakawaacha hadi wafe. Hili li nchi yaani linaongozwa kihuni wee acha tu. Raia hawana say kwenye nchi yao. Sasa wanaungurumisha tu Madege na huku wanajua kwamba tupo kwenye mgogoro na Malawi. Wanataka sisi tuhisi tu kwamba ni salama, kama tumevamiwa je?
 
hayo mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya ckukuu ya muungano april 26, wala hamna kitu kingine chochote

asanteni kwa kutukuza ila ni kweli taarifa ni muhimu sana. na hapa suala si ugeni jamani. kwani hata kama umezaliwa dar sio lazima uwe unajua kila kitu kinachoendelea jijini. tuwe na subira basi tunapotoa majibu.
 
Ni ndege za jeshi jeshi letu za zamani sana! Zinafanya mazoezi kwa ajili ya sherehe za kitafa zinazokuja. Ndege kama hizo wenzetu walitumia miaka ileee ya hamsini kweusii...ni moja ya silaha chache tulizonazo na ambazo tunadanganywa kuwa jeshi letu ni la kisasa...
 
fanyeni mazoezi ya kurusha ndege mjini alafu yatokee yakutokea tuanze kumtafuta mchawi nani.
 
Kama wana mazoezi wangetangaza kabla ili tujuwe, haya ya kushituana wakati mnajuwa tulishawahi lipukiwa kule mbagala na gongolamboto hayafai..

Uko sahihi. Kufanya mazoezi bila kutangaza si jambo sahihi hasahasa katika majiji makubwa. Kunaweza kuwa na watu wameshaathirika na hiyo mishtuko.
 
Kila inapofika 26.04 katika parade basi huwa na ndege nazo zinacheza parade lake na kutoa heshima kwa mgeni rasmi na kuondoka. Hiyo huongeza mbwembwe ya maadhimisho ya sherehe hizo.

Kwa hiyo ndege hizo zipi katika mazoezi.
 
Utaratibu huo haupo Tanzania, nchi ya kibabe hii. Wanajeshi walijua masaa saba kabla kwamba mabomu ya gongo la mboto yangelipuka lakini wakahamisha familia zao bila kuwatangazia wananchi kuondoka maeneo ya karibu. Wakawaacha hadi wafe. Hili li nchi yaani linaongozwa kihuni wee acha tu. Raia hawana say kwenye nchi yao. Sasa wanaungurumisha tu Madege na huku wanajua kwamba tupo kwenye mgogoro na Malawi. Wanataka sisi tuhisi tu kwamba ni salama, kama tumevamiwa je?

aiseee! Walikuwa na taarifa saa 7 kabla ya mlipuko kumbe? Sasa wale wanajeshi waliokufa kwenye milipuko hawakuwa informed au walijitolea kufa? Na mbna mali nyingne ziliharibika jeshin mkuu? Au walizitoa sadaka?
 
acha ushamba usidharau ulichonacho mfukoni eti kwavile umesha tumia umeridhika kithani kama kile unachofikiria kukipata sasa unavyosema scraper ikitokea vita haitakusaidia hiyo unayosema scraper.
 
aiseee! Walikuwa na taarifa saa 7 kabla ya mlipuko kumbe? Sasa wale wanajeshi waliokufa kwenye milipuko hawakuwa informed au walijitolea kufa? Na mbna mali nyingne ziliharibika jeshin mkuu? Au walizitoa sadaka?
Wewe unaongelea milipuko ya wapi? Mimi nasema ya gongo la mboto! Kama una ushahidi wa mwanajeshi aliyekufa au familia ya mwanajeshi iliyopata hata kovu tu kutokana na milipuko ya gongo la mboto ulete hapa jamvini.
Kuhusu mali za jeshi, ni kichaa tu ataanza kuhama na mali wakati wa vita. Nafikiri uhai ndiyo huwa ni first priority kuliko kingine chochote.
 
Kwahiyo mkuu unathibitishia jamvi hapa hakuna askari yoyote aliepata madhara kwenye ile kadhia ya gongo la mboto? Kama taarifa walikuwa nazo 7hrs before si kulikuwa na uwezekano wa kufanya evacuation within that time frame? Pia wangeweza wakahamishia hyo milipuko mbali ili kupunguza ukubwa wake sasa hapa unataka kutuambia jeshi letu haliko makini au?
 
Wamehamisha familia zo tangu saa saba, na mabomu yameanza kulipuka saa mbili usiku. Hivi wangeamua kupita na kipaza sauti kule kuwatangazia wananchi waondoke maeneo ya karibu na gongo la mboto si wangeokoa maisha ya watu wengi tu? Au wangeleta magari ya jeshi na kuwabeba watu watu kuondoka eneo la hatari kama walivyofanya kuwabeba kuwarudisha kwenye maeneo yao, si wangekuwa wamesaidia sana?
 
Leo nimeona zimepita tano zimechoka hizo! Spidi hata mia haifiki ikabidi nijifiche visije niangukia bure mie
 
Achana nao hawa ni wasiopenda maendeleo. Mi nakuhakikishia watu wa aina hii hata wasikie chadema wanefanya ovu gani basi watalitetea na kufanya liwe jema, lkn CCM wafanye jema lolote basi wataliponda tu. hawana kheri hawa..

btw mi mwenyewe tangu majuzi (kama wiki) naona izi ndege, lakini nazikuta ni rangi ya njano mpaka najiulize za wapi zile??? Nikafikiri mazoezi ya kujiandaa na malawi...

Mkuu hebu waache wamalawi wapumue!
 
Mchukue tahadhali nyie mnaokwenda huko kiwanjani kusherekea muungano kwani hizi ndege ni za zamani na huko nyuma ziliwahi kuanguka na kuua marubani kwenye maonesho ya sikukuu kama hiyo!!
 
Back
Top Bottom