Kanyafu Nkanwa
JF-Expert Member
- Jul 8, 2010
- 850
- 103
Kinachonishangaza hapa ni hii habari kuwa abiria wa ndege bado hawajaokolewa toka ndege ianguke! Huku Africa, ukiwa mzima shukuru Mungu wako sana.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/3587-ndege-yaanguka-morogoro
Geofrey Nyang'oro
NDEGE ndogo ya Kampuni ya Safari Linck iliyokuwa imebeba watalii kuwapeleka Mbuga ya wanyama Selous, imeanguka.
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkuu wa Usama wa kampuni hiyo, Azizi Abdallah ambaye ni rubani, alisema tukio hilo liitokea jana katika eneo la Matombo, mkoani Morogoro.
Abdallah alisema ndege hiyo ilikuwa imebeba watalii wawili ambao walikuwa wanakwenda kuangalia wanyama katika mbuga ya Selous, mkoani humo na kwamba ndege hiyo, ilikuwa ikiendeshwa na rubani kutoka Norway.
"Ndege hii ndogo yenye namba ya usajili 5HMG1 imeanguka leo (juzi) saa 10:00 jioni, mpaka sasa haijaokolewa na tunaendelea na juhudi za uokoaji," alisema Abdallah.
Abdallah alifafanua hadi jana abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo, walikuwa hawajaokolewa.