tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,039
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya (KCAA) imethibitisha kuwa ndege ndogo iliyokuwa ikisafiri kutoka Diani kwenda Kichwa Tembo imeanguka katika Kaunti ya Kwale.
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa KCAA, Emile N. Arao, ya leo Oktoba 28, 2025, imesema ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-CCA, iliyokuwa imebeba watalii, imeanguka majira ya asubuhi ikiwa na watu 12 ambao wote wamethibitishwa kupoteza maisha.
Soma pia: Kenya Airways yaongeza Idadi ya Safari za ndege kuelekea Kisumu
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mashirika ya serikali yanayohusika na uokoaji na uchunguzi tayari yamefika kwenye eneo la tukio kuchunguza chanzo cha ajali na kutathmini athari zake.
Imeelezwa, uchunguzi wa kina unaendelea kwa ushirikiano na mashirika husika, na matokeo yataamua kama ajali hiyo ilitokana na hitilafu ya mitambo, hali ya hewa au sababu nyingine.