Ndege Yaanguka, Yaua Wanne Mlima Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndege Yaanguka, Yaua Wanne Mlima Kilimanjaro

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ab-Titchaz, Nov 9, 2008.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #1
  Nov 9, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ndege Yaanguka, Yaua Wanne Mlima Kilimanjaro ​


  Ally Sonda na Rehema Matowo, Moshi

  WATU wanne ambao ni raia wa kigeni wanaodhaniwa kuwa ni watalii wamefariki dunia papo hapo, baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kuanguka kwenye Mlima Kilimanjaro.

  Habari zilizopatikana jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko zilisema kuwa ajali hiyo ilitokea jana kati ya saa 5:00 na 6:00 mchana.

  Kamanda ameitaja ndege iliyopata ajali ni aina ya Cesna 206 inayomilikiwa na kampuni ya kukodisha ndege ya East Africa Air Charter ya jijini Nairobi nchini Kenya na kwamba ilikuwa na abiria wanne na rubani wake.


  Alisema ndege hiyo iliyokuwa imebeba raia hao wa kigeni wakiwa na rubani mwenye asili ya kiafrika inadaiwa ilikuwa ikitokea Kenya kuja Tanzania.

  Kamanda alisema watu waliofariki ni wanaume wawili na wanawake wawili wote raia wa kigeni na kwamba, hadi jana jioni majina yao na uraia wa nchi wanakotoka ilikuwa haijafahamika.


  Majeruhi wa ajali hiyo ambaye ni rubani (naye jina halijafahamika) amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu na hali yake ni mbaya sana na miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.


  Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo imeanguka jirani ya kilele cha Mawenzi ambacho ni sehemu ya Mlima Kilimanjaro mita 4,000 kutoka usawa wa Bahari.


  Haijafahamika mara moja kama ndege hiyo ilivutwa na mvuto wa asili wa mlima huo au iligonga miamba kutokana na mawingu mazito yaliyopo mlimani ambayo ni hatari kwa usafiri wa anga.


  Hata hivyo, Kamanda Ng'hoboko alisema uchunguzi wa ajali hiyo umeanza kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya pamoja na kufahamu uimara wa ndege hiyo.


  Hii ni mara ya pili kwa ndege aina ya Cesna kuanguka mkoani hapa, mwaka huu mwanzoni ndege aina hiyo ilianguka kwenye Mtaa wa Viwanda mjini Moshi na kuua watu wawili akiwemo rubani na kujeruhi watatu.

  Mwananchi Read News
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  RIP watalii, na rubani apone haraka. Hizi Cesna zimechinja sana..
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jamani kuna haja ya kufanya utafiti na kuunda tume kwa nini ajali nyingi zinatokea Kilimanjaro za ndege?
  RIP watalii namtakia rubani apone haraka.
   
 4. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  UUUh! Jama hizi ndege nazo ni za zamani mno. Mwaka jana tu ndege ya sky dive pale moshi ilianguaka karibu kabisa na depot ya BP. Iliua rubani na kujeruhi. Mwaka huu ndo hivi tena. Umefika wakati tuweke yote pembeni na sheria ifuate mkondo wake.
  Ndege ya Sky dive ilinunuliwa toka kwa mfanyabiashara mjanjamjanja hapa moshi. Ananunua ndege mbovumbovu zilizokwisha kuwa grounded. Anarepair then anaanza biashara. Saa ingine ukiwa pale moshi unaweza kufikiri hii ndege sasa inaanguka, maana kanatoa Moshi hako, mara ingine kanazima kakiwa angani, lol. Mimi niliwahi kubook ndege pale Moshi Sky dive kwa ajili ya kuzunguka Mlima Kilimanjaro. Nilipoiona hiyo ndege tu nikastuka, maana hata mafuta yanapimwa kwa kijiti (sijui ndio utaratibu huo), hata mdogo wangu alinishauri nisiruke. Nikaghairi nikaacha wenzangu waende. Walirudi salama, lakini miezi michache baadae ikamuua yuleyule rubani Mzanzibari nilikuwa niruke naye.
  Hizi ndege ni mbovu sana! Mbona kwenye magari ya utalii wamewekewa sheria ya magari yanayotakiwa kufanya biashara hiyo yawe na umri gani? Mbona kwenye ndege wasiwekewe viwango vya ndege ziwe na umri gani na masaa mangapi angani?
  Serikali isipokuwa makini tutauzorotesha utalii wetu ambao naaamini kuwa unatuingizia mapato makubwa sana kwa wakati huu.
  Let us pray for Pilot to recover soon
  and RIP for those tourists on board.
   
 5. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hazina hata black box wakafanya tathmini? RIP tourists and get well soon the pilot
   
Loading...