Mimi huwa napenda vigezo kwenye hoja zangu, sasa nikupe historia ya hizi ndege za Tupolev -154:
Ndege hii iliundwa kwenye miaka ya 60 wakati wa USSR.
Kwa miongo kadhaa hizi ndege pamoja na uchakavu wake zimekuwa ndiyo zinategemewa tangu ya ilokuwa USSR hadi Russia.
Baada ya kuundwa miaka ya 60 ikaanza kufanya kazi mwaka 1972 na ikapigwa msasa zaidi mwaka 1986 kwa kufungwa injini mpya na vifaa vipya.
Ndege hii katika uhai wake imepata ajali zipatazo 39 zote zikisababishwa na matatizo ya kiufundi.
Pia, hii si ndege ya kwanza kupata ajali na kuanguka kwani zipo nyingine nyingi ambazo zimekumbwa na zahama hii na habari zikaishia kimyakimya.
Ndege hizi zimetumika sana na kuanguka katika migogoro ya Lebanon, Georgia na Afghanistan.
Na pia mwaka 2010 ndege kama hii ya Tupolev -154 ilokuwa imembeba raisi wa Poland Lech Kaczynski, ilianguka na kuuwa watu 96.
Mara zote ni kutokana na hitilafu kwenye ndege au kiuo cha kuongozea hizi ndege.
Merry Xmas!
Mkuu tukifatilia kwa karibu ndege zilizo hundwa Mataifa mbali mbali, takwimu zao za ajali hazina tofauti kubwa na ndege za Urusi specifically TU-154, kwani tatizo liko wapi- tutafutie takwimu za ajali za ndege zilizo hundwa na kampuni za Amerika mfano:Boeing 7X7 x=0,2,3,4,6 and 8; McDonnell Douglas na Lockheed.
Haya sasa twende Ulaya kampuni ya kuhunda Airbus imepoteza ndege ngapi kwenye mazingara ya kutatanisha, moja niliona inashindwa kutua kwenye uwanja ikaparamia msitu mnene uliokuwa karibu na uwanja wa ndege matawi ya miti ndiyo yalisaidia abiria wengi wasipoteze maisha, kuna mifano mingi kuhusu matatizo ya control systems za Airbus lakini mara nyingi usingizia marubani eti walipata kichaa wakiwa angani na kubamiza ndege kwenye makorongo au baharini - nothing can go horribly wrong kwa western manufactured aircrafts save Russian junks hizo ndizo habari watu wa magharibi wanataka Dunia iamini for a reason!!!
Narudia kuhoji hivi takwimu za kimataifa zinaonyesha nini kuhusu track record za usalama wa ndege za TU-154 kabla ya USSR haijasambaratika, halafu mtu anakuja hapa na kudai eti TU-154 zinapata ajali sana lakini Warusi uwa hawasemi ukweli - lini Urusi iliwahi kukaa kimya ndege zake za kiraia zinapo pata ajali - lini?
Ndege ya Poland ilipo anguka na kuua mkuu wa jeshi na Rais na baadhi ya mawaziri ulijua nini kilitokea kabla ya ndege kupata ajali? je, hali ya hewa ilikuwaje na rubani alishauriwa afanye nini akapuuzia, mbona usemi lolote kuhusu ndege ya kiaarabu aina ya Airbus iliyo anguka kwenye uwanja wa ndege nchini Urusi na kuua abiria kutokana na hali ya hewa kama iliyo ikumba ndege ya Poland aina ya TU-154.
Labda nikukumbushe kitu, ni hivi: kuanzia miaka ya sitini, sabini mpaka mwanzoni mwa miaka ya tisini, shirika la ndege la USSR i.e Aeroflot ndilo lilikuwa linaongoza Duniani kwa kubeba abiria wengi kwa mwaka na ndege zao kuwa na safety record nzuri au wewe hilo ulijui?
Ndege zilizokuwa zinatumia kwa wingi na shirika/kampuni ya Aeroflot ni TU-154, hizo ndizo zilikuwa ni workhorse za shirika la Aeroflot zikifuatiwa na Illushin, binafsi nakumbuka nikiwa Shule nilikuwa naona ndege aina ya TU-154 zikitua Dar, nadhani mara tatu kwa wiki, niliwahi vile vile kwenda kiwanjani kuziangalia, nilivutiwa sana na mabawa yake yalivyo kaa slanted downward tofauti kabisa na ndege nyingine, hata inavyo paa angani upaaji wake haufanani na ndege nyingine, si hilo tu hata injini zake hazikuwa na kelele kama za DC-9, Boeing 707,727 na 737 kati ya hizo Boeing 747 ndiyo kelele za injini hazikuwa kubwa sana kutokana na injini zake kufanyiwa high bypass na kampuni ya RollsRoyce.
Sasa kama miaka ya hivi karibuni baada ya Serikali ya Urusi kuruhusu makampuni ya watu binafsi kuanzisha usafiri wa ndege na kama kampuni hizo zinakata kona i.e hazitaki kuzifanyia service za mara kwa mara ndege zinazo beba abaria hapo unategemea nini, unaweza kulahumu workmanship ya ndege aina ya TU-154 au Serikali ya Urusi? - wakati mwingine tusiwe tunalahumu vitu bila ya kufanya tafiti za kutosha?
Nimalizie kwa kusema kwamba wataalamu waliohunda ndege ya TU-154 pia na marubani wanasema ndege aina ya TU-154 hiko tricky sana wakati wa kupaa, wanasema rubani anapashwa kuwa mwangarifu/makini wakati ndege inaroll kugain momentum rubani akifanya makosa ya kinyanyua too soon ikifikia nyuzi/degree kumi na nne au kumi na tano haikubali tena kugain altitude wanasena hiyo ndiyo weakeness kubwa au design flaw ya ndege aina ya TU-154 na taarifa zinasema ndege ilishindwa ku-gain altitude ndiyo maana rubani alikata kona (U-turn) kurudi uwanjani kujaribu kutua lakini ndege ikanguka maili moja kabla ya kufika pwani/uwanjani kwenye kina cha maji chenye urefu wa mita 50-100. Binafsi nafikiri kiufundi hilo tatizo lilijitokeza tena kama rubani alijisahau akafikiri anarusha ndege aina ya Illushin au Sukhoi Super Jet akasahau design flaw ya ndege aina ya TU-154.