Heshima yako MALCOM - Merry Xmas, kitu cha kwanza kumbuka kwamba ingawa ndege aina ya TU-154 zilihundwa miaka ya nyuma sana lakini kitendo cha kupotea kwenye rada bila ya marubani kutoa taarifa yoyote kwa waongoza ndege ina maana lilitegwa bomu kwenye cockpit au mmoja wa cabin crew alingia chumba cha marubani amevaa mkanda wa high explosive na kujilipua, kumbuka Urusi ina makabila ya watu mbali mbali wengine wenye akili fyatu ambao wanaweza kurubuniwa na majasusi wa magharibi kuweka bomu wakati wanasafisha ndege,kuweka vyakula
au wakati wana-refuel.
Hii inaonekana it was a well planned operation ya kuhangamiza cream ya wanajeshi muhimu waliokuwa wanakwenda Syria wengi wao wakiwa ni na pilots wa fighter jets, mafundi na ma-instructors, binafsi nafikiri hujuma kama hizi sina shaka Urusi ilijua zinaweza kutokea kutokana na sympathizers wa waasi wa Syria, NATO specifically America na Uingereza hao ndio wako obsessed na Urusi, mafanikio ya kijeshi ya Taifa hilo nchini Syria limeaabisha Mataifa hayo, juzi juzi niliwasikia Majenerali wa jeshi la Merikani wakilalamika kwamba silaha zilizo tumiwa na Warusi nchini Syria hazikuwa na ulazima wowote eti silaha hizo zilitumiwa na Warusi wakiwa na lengo la kuitisha Amerika na washirika wao - just imagine!!
Hata ndege ya Urusi iliyo lipuliwa kwenye anga la jangwa la Sanai wanasema wahusika walikuwa ni majasusi wa Uingereza ndio waliwapa bomu wafanya kazi wa kuhudumia ndege ikiwa aridhini wakaliweka chini ya kiti cha abiria, kwa hiyo hujuma hiyo zitaendelezwa tu - cha muhimu Warusi wawe makini sana na wafanyakazi kwenye viwanja vya nchini mwao ambavyo ni critical kwa operations za nchini Syria.
Binafsi siamini kama ndege hiyo was brought down na MANPAD ambazo Obama alipania kuwapatia waasi kabla hajaondoka Ikulu. Mkuu that's my plausable explanation, I might be wrong.