Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa, mihogo...

Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa, mihogo...

Ivo mzigo wa waheshimiwa wengine wanaposafiri na ndege si huingizwa kwenye ndege hiyohiyo ? CCM jengeni hoja wacheni kuongea pumba . ZNZ tunamengi ya kushuhulikia mfano Rasimu ya Katiba .
 
Ndege ni chombo cha usafiri kama gari, meli nk. Kuna ubaya gani kubeba mkaa na vitu vingine kama anayeitumia kaenda kwao au wananchi wamempa. Kwanza ndege inasehemu ya mizigo. Sasa imewekwa ya yanini? Mbona ndege zinabeba samaki na vitu vingi tu. Kwanza ndege yenyewe inakuwa na watu wachache sana sioni ubaya kwa anayeitumia kubeba vitu vyake vichache anaporudi nyumbani. Mbona magari ya serikali yanabeba mikaa, ndizi nk? Ukifuatilia utakuta hata rais mwenyewe huwa anafungashiwa vitu mbali mbali anapokuwa katika ziara zake ikiwa ni pamoja na mifugo kama mbuzi na kuku. Itakuwa ni matumizi mabaya ya pesa za umma kuanza kulipia gharama za meli au gari wakati ndege ina nafasi na haina mizigo na watu wengi. Hivi Kikwete na Shein wakisafiri huwa hawabebi mizigo? Hizo ni siasa za maji taka!
 
haoo jamaa wa uvccm ni fitna tu sio chengine

Hawana hoja. Ndege ni chombo cha usafiri na ina sehemu ya kuweka mizigo sasa kuna ubaya gani kubeba mizigo hata ikiwa ni mkaa? Itakuwa ni ujinga kusafirisha mizigo mizigo kwa usafiri mwingine na kwa gharama nyingine za wananchi wakati ndege inanafasi na haina abiria wengi kama zilivyo ndege za viongozi. Mimi ninavyojua ndege inaweza kubeba mzigo wowote ili mradi ni salama na umechunguzwa na ukaonekana hauna madhara kwa abiria na ndege yenyewe. Ndege zinabeba mabomu, unga, magari, samaki, bunduki, risasi, wanyama, maiti, magogo, nk sembuse mkaa? Hebu sasa tuchunguze Jk na shein huwa wanabeba nini katika ziara zao. Na ukweli huwa sio wao wanaopakia bali ni watu wa itifaki katika misafara yao ndio huamua mizigo ya rais ibebwe vipi. Unaweza kukuta rais anaikuta nyumbani bila kujua imebebwa vipi kwakuwa kuna watu wanaoshughulika na mizigo ya rais. Hawa waibua hoja hii ni pinda tu!
 
Kwa maana ya heshima ya mamlaka inakuwa siyo nzuri vinginevyo poa tu
 
zenjiplane.jpg

Ndege maalumu ya Rais Tanzania pia hutumika kubeba viongozi wa Serikali

Wabunge wa CCM Zanzibar wameibua zengwe jipya dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba anatumia ndege ya Rais kubebea mkaa, mihogo na ndizi kutoka Pemba kwenda Unguja.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaeleza kuwa, tuhuma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita.

Kitendo hicho kinachodaiwa kufanyika mwezi uliopita kimeonekena kuwakera baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo wabunge wa CCM Zanzibar, ambao wakati wa kikao hicho na Rais Dk Shein mwezi uliopita mjini Zanzibar, walilizungumza kwa uchungu na kuomba Rais amuonye Maalim Seif kwa kuigeuza ndege ya Rais kuwa ya mizigo.

Anayedaiwa kuibua hoja hiyo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis, ambaye alisema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege hiyo kubebea mkaa, mihogo na mikungu ya ndizi kinadhalilisha Ofisi ya Rais.

Katibu wa Wabunge wa CCM Zanzibar, Mbunge wa Magomeni, Mohammed Chombo alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo alikiri wabunge hao kulifikisha suala hilo kwa Rais Shein.

“Tulimweleza Rais matatizo mengi likiwamo na hilo la Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege ya Serikali kubebea mihogo na mkaa,” alisema.

Alisema kuwa Rais aliwaambia kuwa ameyapokea malalamiko hayo na kwamba atayafanyia kazi.

Chombo alisema kuwa kwa sasa wanamsubiri Rais Shein awaite kuwapa majibu ya matatizo yao.

Baadhi ya wabunge wa CCM Zanzibar ambao walizungumza na gazeti hili, walisema kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya mali za umma kwa sababu kuna vyombo vingi vya usafiri vinavyoweza kutumika kusafirishia mizigo hiyo.

Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutoka Mamlaka ya Ndege za Serikali, akizungumzia utaratibu wa viongozi wa Serikali kutumia ndege hizo, alisema viongozi wa juu wa Serikali ya Muungano na Zanzibar hukodi ndege zao.

Alisema hajawahi kuona ndege kubebea mkaa, hata ndege ya jeshi hajawahi kuona ikibeba mkaa.

Hata hivyo, Katibu wa Wabunge wa CUF, Mohammed Habibu Mnyaa, alisema madai hayo ya wabunge wa CCM ni siasa chafu dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kwamba wao wanaamini hawezi kufanya jambo hilo.


Source: Mwananchi

Afadhali yeye kabeba ndizi na mkaa, wengine wanapakia pembe za ndovu, na madini ya wizi.
 
Kwani kuna tatizo gani akibeba mihogo au ndizi?! Mlitaka abebe pizza na burger wakati hazipo Pemba?!
 
Back
Top Bottom