Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa, mihogo...

Ndege ya Rais yadaiwa kubebea mkaa, mihogo...

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,476
Reaction score
21,046
zenjiplane.jpg

Ndege maalumu ya Rais Tanzania pia hutumika kubeba viongozi wa Serikali

Wabunge wa CCM Zanzibar wameibua zengwe jipya dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba anatumia ndege ya Rais kubebea mkaa, mihogo na ndizi kutoka Pemba kwenda Unguja.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaeleza kuwa, tuhuma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita.

Kitendo hicho kinachodaiwa kufanyika mwezi uliopita kimeonekena kuwakera baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo wabunge wa CCM Zanzibar, ambao wakati wa kikao hicho na Rais Dk Shein mwezi uliopita mjini Zanzibar, walilizungumza kwa uchungu na kuomba Rais amuonye Maalim Seif kwa kuigeuza ndege ya Rais kuwa ya mizigo.

Anayedaiwa kuibua hoja hiyo ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis, ambaye alisema kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege hiyo kubebea mkaa, mihogo na mikungu ya ndizi kinadhalilisha Ofisi ya Rais.

Katibu wa Wabunge wa CCM Zanzibar, Mbunge wa Magomeni, Mohammed Chombo alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo alikiri wabunge hao kulifikisha suala hilo kwa Rais Shein.

"Tulimweleza Rais matatizo mengi likiwamo na hilo la Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege ya Serikali kubebea mihogo na mkaa," alisema.

Alisema kuwa Rais aliwaambia kuwa ameyapokea malalamiko hayo na kwamba atayafanyia kazi.

Chombo alisema kuwa kwa sasa wanamsubiri Rais Shein awaite kuwapa majibu ya matatizo yao.

Baadhi ya wabunge wa CCM Zanzibar ambao walizungumza na gazeti hili, walisema kuwa kitendo hicho ni matumizi mabaya ya mali za umma kwa sababu kuna vyombo vingi vya usafiri vinavyoweza kutumika kusafirishia mizigo hiyo.

Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake kutoka Mamlaka ya Ndege za Serikali, akizungumzia utaratibu wa viongozi wa Serikali kutumia ndege hizo, alisema viongozi wa juu wa Serikali ya Muungano na Zanzibar hukodi ndege zao.

Alisema hajawahi kuona ndege kubebea mkaa, hata ndege ya jeshi hajawahi kuona ikibeba mkaa.

Hata hivyo, Katibu wa Wabunge wa CUF, Mohammed Habibu Mnyaa, alisema madai hayo ya wabunge wa CCM ni siasa chafu dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kwamba wao wanaamini hawezi kufanya jambo hilo.


Source: Mwananchi
 
hivi marehemu juma akukweti si inasemekana ndege aliyopanda ilianguka kutokana na kujaza magunia ya viazi Mbeya? just rumours, recall then learn a lesson
 
hivi marehemu juma akukweti si inasemekana ndege aliyopanda ilianguka kutokana na kujaza magunia ya viazi Mbeya? just rumours, recall then learn a lesson


Haa chazea wake wawili wewe? Jamaa alifungasha mpaka mikungu ya ndizi kwenye ndege sasa kwa nini isichemshe ku gain momentum?
 
hivi marehemu juma akukweti si inasemekana ndege aliyopanda ilianguka kutokana na kujaza magunia ya viazi Mbeya? just rumours, recall then learn a lesson

alijaza magunia ya viaz na mchele wa kyela!

ila jaman mlitaka makamu wa rais abebewe mkaa wake kwa kutumia punda? Hahaha
 
binafsi sijaona shida katika hilo maana naamini hiyo ndege ina sehemu ya kuweka mizigo ya aina hiyo,mbona tunatoka mwanza tunabeba samaki kwenye ndege vp Maalim akibeba zawadi kwa familia yake au ndio siasa tena?
 
Hao watu wanaafanya umbeya wa kisiasa na ni wa kitoto vilevile. Kuna tatizo gani kubeba mizigo kwenye ndege uliyokodisha? Sidhani kama Makamu wa Raisi anasimamia hata mizigo inayopakiwa kwenye ndege? Ikiwa kuna kanuni za aina ya mizigo inayotaakiwa kuchukuliwa wanaopaswa kusimamia ni Wakala wa Ndege za Serikali na wao ndio wangeulizwa.
 
binafsi sijaona shida katika hilo maana naamini hiyo ndege ina sehemu ya kuweka mizigo ya aina hiyo,mbona tunatoka mwanza tunabeba samaki kwenye ndege vp Maalim akibeba zawadi kwa familia yake au ndio siasa tena?
============================

Unafiki mwingine balaa kweli!

Hivi ndege hizi hizi mbona zinabeba mahawala, nyumba ndogo, madawa ya kulevya, samaki, bia, gongo ya Karume, bangi ya Mzee wa Gombe, tindikali, pembe za ndovu, masanduku ya wizi wa kura, nk?

Kubeba mkaa wa Mzee Madevu ndo imekuwa nongwa?!

Siku moja pale Dodoma, Waziri mmoja wa SMZ nusura aachwe na ndege hiyo baada ya walinzi kumkatalia kimada wake apande ndege hiyo. Ilibidi ashuke kuja kuwabembeleza wakati injini zimeishawashwa.


Hiki ni kisingizio cha kuvunja SUK
 
Huku ni kujidhalilisha. Kwani huo mkaa aliingia nao ndani akachafua watu waliokuwamo? Hakika mtu akitaka kukutukana hakuchagulii tusi. Wenye lugha zao husema: Give a dog a bad name and then kill it. CUF tafuteni talaka. Ndoa imekuwa ndoano. Au kama ni koti limebana.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ukiona hvyo jua Mume ambaye ni ccm kamchoka mke ambaye ni CUF. Mbatia zamu yako inakuja kujifanya mke mdogo.

Mume mwenzako unamwona mzuri anapokuwa na mkewe. Subiri waachane halafu wewe uingie ndani ya nyumba ndo utaujua uzuri au ubaya wake. Nampa tahadhari huyu dogo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mbona ndege zinabeba twiga ndizi na vitu kabao tu..hao wamekosa la kusema,huo wivu roho mbaya na wivu wa kijinga..kama kuna nafasi ya mizigo kwa nini asibebe zawadi?
 
Walitaka abebee nini? Waache kumwandama... Seif nae unajidhalilisha bana.. Si ungepakia kwenye boti? Mpaka uchafue ndege na mkaa, utovu wa ndizi na mihogo! Hii aibu sasa..
 
mbona hawazungumzii STK, STJ, SU na STL zetu ambazo zimekuwa ni gari za mizigo badala ya kubeba viongozi. waache unafiki na umbea.
 
AMA hawa CCM Zanzibar wana U-PINDA wanakaa kitako kuzungumzia ndege ya Serikali. Kwani ndege hii ya Serikali au ya CCM?. Mbona hawakuzungumza vikao vya CCM vilivyofanyika Ndani ya IKULU ya Magogoni?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom