Ndege ya Emirates yaweka record kukaa hewani masaa 17

Ndege ya Emirates yaweka record kukaa hewani masaa 17

Mkuu waambie huku Afrika mashariki wezi wa kura tunapongezana
 
Mkuu hiyo ndege sidhani kuwa ni Airbus 380,nijuavyo mimi ilikua ni Boeing 777-200 LR flight number EK 449 na ilifanya hiyo safari tarehe 2-3-2016 imesafiri kilometer 14,203 non stop.


Boeing sasa hivi wameachwa nyuma sana Kitekonolojia na AirBus, wana kazi kubwa sana ya kuwafikia AirBus leo hii, kwa maana AirBus wanauza kama hawana akili nzuri wanavunja rekodi kila siku kila mahali bado kuna ya mizigo Airbus beluga ni noma!

Airbus Beluga - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Hili dege Ni la ukweli sana, limetengenezwa kwa teknolojia ya juu sana, ukiangalia Kule kwenye cockpit unachoka! Kuna moja Kama hio iliungua engine km chache tu baada ya kuruka Ila hakufa mtu! Ila binafsi sipendi sana ndege za kubeba watu wengi, likitokea la kutokea wanakufa wengi.
 
Mtu unachoka sana safari ikiwa ndefu hivyo....... Unakunywa wee mpaka pombe zinakuisha kichwani, unalala unaamka bado tu hamjafika[emoji134]
 
Daaah!! Wananikumbusha safari yangu ya Amsterdam to ottawa
 
Mimi navunja rikodi kwa kutumia mkokoteni wa Punda kilomita 50 masaa 12.
 
3cd1d6e81b72be37835ca97ded019a4b.jpg


Iringa Mjini to Mwatasi
 
Ni airbus 380 emirate ilitoka dubai hadi new zealand kilometa 14,000 masaa 17 bila kusimama..kiboko yao
 
View attachment 327861 View attachment 327862 View attachment 327863

Ndege ya shirika la Emirates imekamilsha safari ya moja kwa moja ndefu zaidi duniani kutoka Dubai hadi New Zealand.

Ndege hiyo aina ya Airbus 380, ambayo ndiyo kubwa zaidi ya abiria duniani imesafiri angani kwa kilomita 14,200 bila kusimama, safari iliyochukua masaa 17 na dakika 15.

Kwa taarifa yako na wengine wasiojua. Hii sio safari ndefu ya ndege ya abiria kama unavyodai. Ilikuwepo safari ya masaa 18:30 kutoka Newark Liberty Intenational Airport -USA hadi Singapore Changi Airport ikifanywa na Singapore airlines. Ndege ilikuwa airbus A340-500 na safari ina umbali wa km 15,343. Ilikuwa ina julikana kama Singapore Airlines flight 21. Hiyo safari kwa sasa imesitishwa.
 
Back
Top Bottom