Nchi ya Tanzania ilinunua ndege mpya aina ya dreamliner natumaini ni mwaka 2021 lakin ndege hii haina zaidi ya miaka mitatu tayari iko gereji. Ndege mpya aingii akilini mwangu. Wakati ndege hiyo inapelekwa kwenye matengenezo wananchi hatukutaarifiwa na baadaye raia mwema ndo katoa taarifa hii.
Hasara inayopatikana kwa ndege hiyo kutofanya kazi kwa muda huo ni hasara kubwa na hii inaonyesha jinsi hatuko maakini na mali za umma. Ndege ina muda mrefu kwenye matengenezo na wananchi wanakosa huduma na huku tukielezwa na MD wa Air Tanzania kuwa iko kwenye foleni na muda wake wa matengenezo bado kwa sababu kuna ndege zingine mbele yake.
Huu mradi wa kununua ndege binafsi naona kama tunapoteza fedha za umma bure na ni afadhali fedha za kununua ndege mpya zingeelekezwa kwenye miradi mingine kama afya, barabara, maji n.k. Mwaka ujao utaona ripoti ya CAG kuhusu hasara ya ATCL.
Nimesoma leo kuwa Ethiopian Airlines imetengeza faida ya $6.1 billion kwa mwaka mmoja na Kampuni inasimamiwa na Serikali ya Ethiopia. Sisi tunakwama wapi. Tuwe maakini na fedha za umma. Wananchi wanakamuliwa kwa jili ya kodi.