Ndege mpya ya Q 400 bombardier ya ATCL yaanza kazi rasmi

khumbu_peresa

Member
Feb 11, 2021
28
105
Habarini wanabodi na watanzania kwa ujumla.

Takribani wiki mbili na nusu shirika la ndege la Tanzania limekua na mfululizo wa delays za ruti zake mbalimbali.

Kwa wenye ushuhuda hapa jamvini wataweza kushea nasi hali ya safari zao walivyotumia shirika hili ndani ya wiki mbili zilizopita mpaka sasa.

Ndege zilitakiwa kuondoka Dar kwenda Mwanza saa 1:30 jioni ziliondoka saa 5,6,7 mpaka 8 usiku hii imekua kero kubwa hasa kwa shirika kama hili ambalo limejozolea umaarufu mkubwa kwa kuwa na ndege zaidi ya 8 mpya kabisa.

Kwa mujibu wa afisa habari wa shirika ndugu Josephat mwingira alisema mapema kuwa ndege zetu zilikua zimeenda kufanyiwa matengezo ya kawaida (service).

Lakini wataalamu wa mambo wanasema ndege haziko kwenye matengezo ya kawaida bali ni mbovu...

Hii imelazimu shirika kuanza kutumia ndege mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 ambayo ilipokelewa mapema tarehe 30/07/2021 na mhe Rais Samia pale uwanja wa ndege wa Dar.

Ndege hii yenye usajili wa 5H-TCK imeanza rasmi leo safari yake ya kwanza kama sehemu ya uokozi', ama kuondoa au kupunguza hizi delays.

Shirika pia limelazimika kuunganisha abiria wa ruti tofauti tofauti ili kuwaweka kwenye ndege moja ili wasikae sana airport.

Mpaka sasa kwa taarifa zilizopo shirika lina jumla ya ndege 9 na safari (destinations) 16.

Shirika lina Boeing Dreamliner 787-8 mbili ambazo ni zile kubwa kabisa kila moja inabeba abiria 262.

Pia lina Airbus A220-300 mbili, ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 132. Na hapa kwenye Airbus moja ni hii anayoitumia Namba moja wetu na moja iko kwenye matengezo kwa mwezi sasa.

Pia shirika lina hizi pangaboi au DASHQ-400 ambazo ziko 5,..zilikua nne na hii ya juzi aliyopokea mama Samia ni ya 5 ambazo hizi zinachukua abiria 76.

Katika hizi DASH 8-Q400 tano ni mbili tu zilikua zinafanya kazi ,mbili ziko matengenezo..ukijumlisha hii iliyoanza kazi leo inakua 3 ziko zinapiga mzigo.

Shirika lijitahidi kwenda na kasi ya biashara ya anga..hizi delays na usumbufu zinawakera abiria ,kupotezea muda abiria na hii itafanya watafute shirika lingine ili waweze kusafiri.

Tunasafiri na ndege ili tuwahi...lakini inakera pale unafika na kuanzia asubuhi mpaka jioni na haujafika safari uendayo.

Kama Ikulu inakodi ndege ya shirika kumpeleka Rais ni vyema, walipie huduma ....ila kama yuko zanzibar na harudi siku hiyo hiyo basi ndege irudi Dar isaidie kuokoa jahazi....

Mhe Rais akitaka kuondoka zanzibar kuja dar basi iende kumchukua.

Hatuwezi kuiweka ndege pale Zanzibar isubirie ,kibiashara ndege haitakiwi kukaa chini muda mrefu.

Wasalaaaaam.

20210820_100103.jpg
20210820_085841.jpg
20210820_100052.jpg
 
Hapa mi naona wangeruhusu ushindani wa kibiashara ili Atcl iweze kuchangamka,uwepo wao unazolotesha usafiri kwa abiria
 
Kuna ndege moja ya ATCL ilipita angani juu yangu nikaiangalia chini..ilikua chafu sana..nikajiuliza kwani huko angani Kuna matope au rough roads sikupata majibu..
 
Kuna siku 2016 nilikuwa natoka Reykjavik Icelend kuelekea Stockholm na budget airlines WOW yani ndege ilitakiwa iondoke saa moja asubuhi tukaondoka saa saa nne asubuhi baada ya masaa matatu kisa wanawasubiria abiria kutoka Canada ambao wangefaulisha.

Yani muda wote tuko ndani ya ndege. Tulimaindi kichiz licha ya kulipa nauli ya kama 25 us dollars. Hilo shirika lilifilisika 2019 hata kabla ya Corona kisa hizi delays za kisoro na lilitawala soko la Iceland na across the Atlantic.
 
Mkuu msemaji wa Shirika ni Josephati Mwingira?,yule nabii magumashi?,hebu fuatilia...nadhani ni somebody Kagirwa...wajuzi watatujuza...
 
Habarini wanabodi na watanzania kwa ujumla.

Takribani wiki mbili na nusu shirika la ndege la Tanzania limekua na mfululizo wa delays za ruti zake mbalimbali.

Kwa wenye ushuhuda hapa jamvini wataweza kushea nasi hali ya safari zao walivyotumia shirika hili ndani ya wiki mbili zilizopita mpaka sasa.

Ndege zilitakiwa kuondoka Dar kwenda Mwanza saa 1:30 jioni ziliondoka saa 5,6,7 mpaka 8 usiku hii imekua kero kubwa hasa kwa shirika kama hili ambalo limejozolea umaarufu mkubwa kwa kuwa na ndege zaidi ya 8 mpya kabisa.

Kwa mujibu wa afisa habari wa shirika ndugu Josephat mwingira alisema mapema kuwa ndege zetu zilikua zimeenda kufanyiwa matengezo ya kawaida (service).

Lakini wataalamu wa mambo wanasema ndege haziko kwenye matengezo ya kawaida bali ni mbovu...

Hii imelazimu shirika kuanza kutumia ndege mpya aina ya Bombadier DASH 8-Q400 ambayo ilipokelewa mapema tarehe 30/07/2021 na mhe Rais Samia pale uwanja wa ndege wa Dar.

Ndege hii yenye usajili wa 5H-TCK imeanza rasmi leo safari yake ya kwanza kama sehemu ya uokozi', ama kuondoa au kupunguza hizi delays.

Shirika pia limelazimika kuunganisha abiria wa ruti tofauti tofauti ili kuwaweka kwenye ndege moja ili wasikae sana airport.

Mpaka sasa kwa taarifa zilizopo shirika lina jumla ya ndege 9 na safari (destinations) 16.

Shirika lina Boeing Dreamliner 787-8 mbili ambazo ni zile kubwa kabisa kila moja inabeba abiria 262.

Pia lina Airbus A220-300 mbili, ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 132. Na hapa kwenye Airbus moja ni hii anayoitumia Namba moja wetu na moja iko kwenye matengezo kwa mwezi sasa.

Pia shirika lina hizi pangaboi au DASHQ-400 ambazo ziko 5,..zilikua nne na hii ya juzi aliyopokea mama Samia ni ya 5 ambazo hizi zinachukua abiria 76.

Katika hizi DASH 8-Q400 tano ni mbili tu zilikua zinafanya kazi ,mbili ziko matengenezo..ukijumlisha hii iliyoanza kazi leo inakua 3 ziko zinapiga mzigo.

Shirika lijitahidi kwenda na kasi ya biashara ya anga..hizi delays na usumbufu zinawakera abiria ,kupotezea muda abiria na hii itafanya watafute shirika lingine ili waweze kusafiri.

Tunasafiri na ndege ili tuwahi...lakini inakera pale unafika na kuanzia asubuhi mpaka jioni na haujafika safari uendayo.

Kama Ikulu inakodi ndege ya shirika kumpeleka Rais ni vyema, walipie huduma ....ila kama yuko zanzibar na harudi siku hiyo hiyo basi ndege irudi Dar isaidie kuokoa jahazi....

Mhe Rais akitaka kuondoka zanzibar kuja dar basi iende kumchukua.

Hatuwezi kuiweka ndege pale Zanzibar isubirie ,kibiashara ndege haitakiwi kukaa chini muda mrefu.

Wasalaaaaam.

View attachment 1899405View attachment 1899406View attachment 1899407
Shirika linapata faida kweli?
 
Back
Top Bottom